Njooni tumuombe msamaha Mo kwa yote yaliyotokea

Njooni tumuombe msamaha Mo kwa yote yaliyotokea

Nani anaumia we utopolo?

Au unasoma msg za fb na insta ndio unajidanganya ni wana Simba hao?
Mbona wengi ni wauza papuchi tu wanajisemea tu wanavyojisikia!
Wana Simba wa kweli wamefurahi tu kwani wameamini maneno ya viongozi wao yalikuwa kweli
Naona wanasimba tumepanic kipuuzi kisa Manara kuhamia Yanga. Hakuna kitu kipya.

Ukweli ni kuwa, Manara amekuwa mwajiriwa wa GSM kwa miaka kadhaa, GSM ndio wafadhili wa Yanga, na leo GSM wamempangia kazi pale Jangwani.

Pili Manara alishaondolewa Simba, hana mkataba na Simba, leo amekwenda Yanga kama mtu huru. Anapambana na maisha yake, tusiumie sana.
 
Mwisho wa siku Manara naye anahitaji hela ili aishi mjini..
Aendeleze unazi halafu aishije?
Inawezekana kweli anaipenda Simba zaidi lakin kwa Sasa hayuko Simba aendelee kukaa bila kazi wakati Yanga wanamhitaji..
Usemaji ni kazi kama kazi nyingine..
 
Manara aliacha kazi huku akiichafua Simba.Kama aliona Simba hakuna maslahi,si angeondoka kimya kimya mapeema kabisa
Nan kakwambia njaa nzuri, kama ambavyo wewe ukipata dili nono utakacha kazi unayoifanya ndivo ambavyo manara amefanya mwacheni ajitafutie riziki pale anapoona pana maslahi bora nayeye
 
Ule msemo wa kuwa Siasa haina rafiki au adui wa kudumu naomba leo uhamie kwenye soka!

Mimi binafsi naomba Mo unisamehe, niliaminishwa maneno kuwa wewe ni mbaya na jamaa fulani ila leo nimeamini tulidanganywa!

Kweli muda ni mwalimu mzuri sana!
Kageuza Simba timu yake binafsi hilo ni kosa tatizo wahindi hawapendi kuwaona watu weusi kuwa bora
 
Walitaka awe ombaomba
Ila binadamu bwana 😂, yani mtu alifukuzwa Simba Sc Sasa katafuta kibarua Ili mkono uende kinywani bado mnamuwekea kiwingu? Kuna shabiki yoyote wa Simba sc humu ambaye angempelekea msosi nyumbani kwake? Mnataka aendekeze ushabiki usio faida kwake?

Yani mlitaka akae bila kazi, aadhirike Ili mpate maada za kumjadili, kwenye team ya SIMBA SC aliashaacha kazi na baadhi ya watu walimtukana humu , kwasasa ukaamua kutafuta ugali wake pembeni achaneni nae.
 
Mie sio fan wa Mpira wa Tanzania but nachojua kutokea kwa tukio moja linaweza kubadilisha muelekeo wa tukio lifuatalo.
Yawezekana kabisa Mo akawa chanzo cha Manara kuondoka Simba,sasa sijui baada ya kuondoka mlitaka akae bila kazi? I'll athibitishe kuwa anaipenda Simba.
ushaambiwa huyo alijiita Simba damu damu hata iweje hawezi kuihama Simba hayo ni maneno yake mwenyew Manara sasa leo inapotokea kafanya tukio la kushangaza kama hili wana Simba wengi wanajiuliza inakuweje waliishi na ndumila joka jeusi ndani ya nyumba kumbe lingeweza kuwadhuru pa kubwa kama timu

kumbuka Manara si mchezaji ,kama angekuwa hivo wala haina shida maana wachezaji hutazama maslahi yao yaliyo bora jambo ambalo ni jema kbs lkn kwa kiongozi ni jambo geni kabisa halijawahi kutokea kila mtu anashangaa hata hao Yanga
 
Mwisho wa siku Manara naye anahitaji hela ili aishi mjini..
Aendeleze unazi halafu aishije?
Inawezekana kweli anaipenda Simba zaidi lakin kwa Sasa hayuko Simba aendelee kukaa bila kazi wakati Yanga wanamhitaji..
Usemaji ni kazi kama kazi nyingine..
Alichokosea manara ni kutoa shit dhidi ya uongozi wa simba.

Kwani angeondoka kwa kusema hawajakubaliana mktaba/maslahi kulikuwa na ugumu gani.
 
Wabongo tuna ubinafsi.

Emanuel Okwi , Juma Kaseja wote wamecheza timu hizi mbili.

Kwanini Haji Manara kijana wa Kitanzania ashindwe kupata ugali wake na familia yake kisa kuitumikia Simba ?
Haji ni Mchezaji? wa timu gani?
 
ushaambiwa huyo alijiita Simba damu damu hata iweje hawezi kuihama Simba hayo ni maneno yake mwenyew Manara sasa leo inapotokea kafanya tukio la kushangaza kama hili wana Simba wengi wanajiuliza inakuweje waliishi na ndumila joka jeusi ndani ya nyumba kumbe lingeweza kuwadhuru pa kubwa kama timu

kumbuka Manara si mchezaji ,kama angekuwa hivo wala haina shida maana wachezaji hutazama maslahi yao yaliyo bora jambo ambalo ni jema kbs lkn kwa kiongozi ni jambo geni kabisa halijawahi kutokea kila mtu anashangaa hata hao Yanga
Tena aliapa mbele ya camera za waandishi wa habari .

OVER MY DEAD BODY..siwezi kwenda yanga..
Hata nipewe PESA zote za bank kuu sihami.

Kiko wapi sasa?

Ninaamini manara atafifia kama alivyofifia MZEE YUSUPH baada ya kurejea kwenye nyimbo za taarab.

hatoshine kama simba..
Tena ataondolewa kwa aibu kubwa..
 
Ule msemo wa kuwa Siasa haina rafiki au adui wa kudumu naomba leo uhamie kwenye soka!

Mimi binafsi naomba Mo unisamehe, niliaminishwa maneno kuwa wewe ni mbaya na jamaa fulani ila leo nimeamini tulidanganywa!

Kweli muda ni mwalimu mzuri sana!
Na mkimaliza kumuomba Msamaha Mo Dewji Wewe na Wenzako hapa JamiiForums mniombe Radhi na Mimi Mightier a.k.a Gifted Intellectually, Knowledgeable, Challenger and Well Informed kwani nakumbuka nilikuja na Threads mfululizo hapa hapa nikiwaambia Usaliti mkubwa na Unafiki wa Haji Manara kwa Simba SC mkanidhihaki na hata Kunidharau pia ila leo Maono yangu yamejihidhirisha rasmi.
 
Mwenzio akinyolewa we tia maji yalowakuta simba vivo hivyo na kwa yanga Manara ni mnafiki wa team na si msemaji wa team kama tunavyodhani ni muda tu utasema ukweli
 
Naona wanasimba tumepanic kipuuzi kisa Manara kuhamia Yanga. Hakuna kitu kipya.

Ukweli ni kuwa, Manara amekuwa mwajiriwa wa GSM kwa miaka kadhaa, GSM ndio wafadhili wa Yanga, na leo GSM wamempangia kazi pale Jangwani.

Pili Manara alishaondolewa Simba, hana mkataba na Simba, leo amekwenda Yanga kama mtu huru. Anapambana na maisha yake, tusiumie sana.
umeongea ukweli mtupu jamaa....hao wanaomlaumu Haji wajaribu kujiweka wao kwenye nafasi yake halafu waseme wangechukua uamuzi gani,binafsi nimeumia Haji kuondoka Msimbazi lkn nimefarijika kusikia ataendelea na kazi yake niliyomzoea nayo haijalishi atahamia wapi ilimradi tu awepo kwenye mpira wa Tanzania.Haji ndo binadamu pekee aliyenishawishi kuanza kufatilia soka la nyumbani kutokana na hamasa zake japokua amehamia kwa majirani zetu katu sitaweza kuihama timu lkn pia kamwe sitaweza kumchukia Haji kwangu ataendelea kuwa ICON kwa upande wa usemaji wa mpira wa Tanzania.
 
Ule msemo wa kuwa Siasa haina rafiki au adui wa kudumu naomba leo uhamie kwenye soka!

Mimi binafsi naomba Mo unisamehe, niliaminishwa maneno kuwa wewe ni mbaya na jamaa fulani ila leo nimeamini tulidanganywa!

Kweli muda ni mwalimu mzuri sana!
Manara kwenda yanga si sababu ya Mo kusafishika mkuu...kama alizingua alizingua tu.
 
Ule msemo wa kuwa Siasa haina rafiki au adui wa kudumu naomba leo uhamie kwenye soka!

Mimi binafsi naomba Mo unisamehe, niliaminishwa maneno kuwa wewe ni mbaya na jamaa fulani ila leo nimeamini tulidanganywa!

Kweli muda ni mwalimu mzuri sana!
Umefanya hekima kubwa
Screenshot_20210825-061921.jpg
 
Back
Top Bottom