Njooni tusemezane. Sheria gani inakataza watu kuchangishana? Waziri Mkuu yupo sahihi kumkamata Niffer?

Njooni tusemezane. Sheria gani inakataza watu kuchangishana? Waziri Mkuu yupo sahihi kumkamata Niffer?

Waziri mkuu anadili na michango ya misiba? Kweli hii nchi watu wote ni wendawazimu
 
Sitaki kuingilia mabishano yenu, ila unapoenda mahakamani kama kuna sheria mahususi ya jambo husika.

Sheria mahususi na toleo la mwisho lina supersede sheria zingine zozote, kuna sheria ya ‘maafa 2022’ na imeeleza namna ya kukusanya misaada na imetamka mtu pia anaruhusiwa.

Kosa la Niffer kutokueleza michango ataikabidhi serikali, lakini kuchangisha watu kwenye maafa, kwa sheria husika hajavunja sheria. Upuuzi zaidi ni kujibizana na waziri mkuu mitandaoni hapo ni sawa na kununua ugomvi na serikali.

Hakuna kosa kama hilo eti la kutokusema nikichangisha fedha nitazikabidhi serikalini.
Kinachotakiwa ni kwamba ukishamaliza kukusanya michango hiyo ni kuiwasilisha tume ya maafa na si vinginevyo.
Ingetakiwa wamwache huyo binti akusanye hiyo michango halafu waone angefanya nini na hizo fedha .
Sasa hapo ndipo kungeweza kutokea kosa kama asingewasilisha michango hiyo kwenye kamati ya maafa.
Kwa sasa wamekurupuka na kuleta taharuki isiyo na ulazima kwenye jamii
 
Kapewa kibali na nani? Sheria inasema unapewa kibali na serikali. Yeye alipewa kibali na nani?

Lets start here
Sheria ipi hiyo inayosema unapewa kibali embu naomba nitajie hiyo sheria pamoja na hicho kifungu.
Tafadhali acheni kukurupuka wengine sheria tunazijua na tunazisoma kila siku.
Sasa unaposema tu sheria bila kutaja ni sheria gani na kifungu gani mi nakuona wewe ni kama punguwani flani usiejielewa wala usiejua sheria ni kitu gani
 
Hakuna kosa kama hilo eti la kutokusema nikichangisha fedha nitazikabidhi serikalini.
Kinachotakiwa ni kwamba ukishamaliza kukusanya michango hiyo ni kuiwasilisha tume ya maafa na si vinginevyo.
Ingetakiwa wamwache huyo binti akusanye hiyo michango halafu waone angefanya nini na hizo fedha .
Sasa hapo ndipo kungeweza kutokea kosa kama asingewasilisha michango hiyo kwenye kamati ya maafa.
Kwa sasa wamekurupuka na kuleta taharuki isiyo na ulazima kwenye jamii
Yeye mwenyewe alisema ana mpango wa kwenda kupeleka misaada, hakuna sehemu alisema anapeleka serikalini.

Pili sheria ipo clear unakusanya kwa niaba ya serikali so wahusika lazima wajue intentions zako mapema. Team ya serikali pekee ndio ina panga mipango ya intervention wengine mnaingia kwa muongozo wao.

Kusema unakusanya tu mpaka mwisho halafu ndio upeleke serikalini bila ya kuwapa taarifa wahusika unakusanya kwa sababu gani huko ni kuwapa sababu ya kutafsiri vyovyote wanavyotaka motive zako, ikiwemo utapeli.
 
Ni vyema kama unataka kuona vifungu

Kwa mfano:

Sheria ya Huduma za Kibinadamu (Charity Act): Inahitaji kuwa na usajili wa kisheria kwa taasisi zinazokusanya fedha kwa ajili ya misaada au huduma za kibinadamu. Kukusanya fedha bila usajili wa kisheria au vibali kutoka kwa mamlaka husika ni kinyume cha sheria.

Sheria ya Uhalifu wa Mtandao (Cybercrimes Act): Ikiwa kukusanya fedha kuna husiana na utapeli mtandaoni, kunaweza kumaanisha ukiukaji wa sheria za uhalifu mtandaoni.

Mbona hujataja hivyo vifungu sasa , au hata hujui sheria ni kitu gani na inatafsiriwaje.
Sheria yeyote imeundwa kwa vifungu mbalimbali ambavyo ndio vinatoa nguvu au katazo ..
Ungetakiwa utaje mfano kifungu namba flani cha sheria flani kinakataza kitu flani.
Tungeitafuta hiyo sheria na kwenda kwenye hicho kifungu na kukisoma.
Sasa sijui wewe hapa umeeleza kitu gani, ndugu inaelekea hufahamu hata kitu unachokielezea
 
Sitaki kuingilia mabishano yenu, ila unapoenda mahakamani kama kuna sheria mahususi ya jambo husika.

Sheria mahususi na toleo la mwisho lina supersede sheria zingine zozote, kuna sheria ya ‘maafa 2022’ na imeeleza namna ya kukusanya misaada na imetamka mtu pia anaruhusiwa.

Kosa la Niffer kutokueleza michango ataikabidhi serikali, lakini kuchangisha watu kwenye maafa, kwa sheria husika hajavunja sheria. Upuuzi zaidi ni kujibizana na waziri mkuu mitandaoni hapo ni sawa na kununua ugomvi na serikali.
Kuna..nyumayakee
 
Kuna..nyumayakee
Possible, lakini kwa kuwa alikuwa open nadhani shida ni naivety zaidi. Binafsi nampa benefit of the doubt, alikuwa na nia njema.

Apewe elimu ya taratibu za kukusanya na onyo waziri mkuu akitoa amri ajibiwi kishamba mitandaoni.
 
Tunao wachangia barabarani tunawakutaga na vibari na ata wakija kukuomba wanakuonyesha kibali yeye kabali kiko wapi
Hili ni janga la ghafla na linafahamika nchi nzima.... so cha kuhoji ni mapato na matumizi kuliko mkusanyaji
 
Ukitaka kutengeneza barabara kiwango cha vumbi wala hutasumbuliwa ila ukishaanza kufikiria kiwango cha lami hapo huwezi kujiamulia utahitaji kibali maalumu. Kuna sababu za msingi. Sio kila jambo unaloliona lina faida kwa jamii uku huru kulifanya. Kuna ukomo wa uhuru
 
Mbona hujataja hivyo vifungu sasa , au hata hujui sheria ni kitu gani na inatafsiriwaje.
Sheria yeyote imeundwa kwa vifungu mbalimbali ambavyo ndio vinatoa nguvu au katazo ..
Ungetakiwa utaje mfano kifungu namba flani cha sheria flani kinakataza kitu flani.
Tungeitafuta hiyo sheria na kwenda kwenye hicho kifungu na kukisoma.
Sasa sijui wewe hapa umeeleza kitu gani, ndugu inaelekea hufahamu hata kitu unachokielezea
Sheria ya Udhibiti wa Fedha na Misaada (The Charitable Collections Act, 2009)

Kifungu cha 3 kinatoa maelezo kuhusu usajili wa taasisi au mashirika yatakayokusanya misaada, na kwamba taasisi hiyo lazima iwe na kibali cha kukusanya fedha.

Kifungu cha 5 kinatoa maelezo ya taratibu za makusanyo ya fedha, na matumizi ya misaada.

Kifungu cha 10 kinahusu adhabu kwa mtu au taasisi itakayokiuka sheria hii, ikiwa ni pamoja na adhabu za kifungo au faini kwa udanganyifu

Madhumuni ya Sheria:
Lengo kuu la Sheria ya Udhibiti wa Fedha na Misaada (2009) ni kudhibiti na kudumisha uwazi na usimamizi mzuri wa makusanyo ya misaada, kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa manufaa ya jamii na wahitaji, na kupunguza uwezekano wa matumizi mabaya au ulaghai.

Kwa kifupi, sheria hii inaweka wazi utaratibu wa kukusanya misaada na fedha za hisani, na inahitaji mtu yeyote anayetaka kukusanya fedha kwa ajili ya maafa au shughuli za kijamii kuwa na kibali na usajili kutoka kwa mamlaka husika.
 
Sheria ipi hiyo inayosema unapewa kibali embu naomba nitajie hiyo sheria pamoja na hicho kifungu.
Tafadhali acheni kukurupuka wengine sheria tunazijua na tunazisoma kila siku.
Sasa unaposema tu sheria bila kutaja ni sheria gani na kifungu gani mi nakuona wewe ni kama punguwani flani usiejielewa wala usiejua sheria ni kitu gani
Sheria ya Usimamizi wa Maafa ya mwaka 2022, inatoa mwongozo kuhusu kukusanya fedha kwa ajili ya maafa. Kifungu cha 21 kinakataza mtu yeyote kukusanya fedha bila kibali cha mamlaka husika. Aidha, kifungu cha 22 kinatoa adhabu kwa wale watakaokiuka masharti haya, ikiwa ni pamoja na faini au kifungo.

Hii inahakikisha kwamba michango yote inasimamiwa na mamlaka ili kuzuia udanganyifu na matumizi mabaya ya fedha za msaada.
 
Yeye mwenyewe alisema ana mpango wa kwenda kupeleka misaada, hakuna sehemu alisema anapeleka serikalini.

.

Kusema unakusanya tu mpaka mwisho halafu ndio upeleke serikalini bila ya kuwapa taarifa wahusika unakusanya kwa sababu gani huko ni kuwapa sababu ya kutafsiri vyovyote wanavyotaka motive zako, ikiwemo utapeli.

Mkuu ni kwamba sheria inaelekeza mtu akikusanya hizo fedha sharti aziwasilishe kwenye kamati ya maafa.

Embu nitajie ni kifungu kipi cha sheria ya maafa kinaeleza hivi ,nimekunukuu

"Pili sheria ipo clear unakusanya kwa niaba ya serikali so wahusika lazima wajue intentions zako mapema. Team ya serikali pekee ndio ina panga mipango ya intervention wengine mnaingia kwa muongozo wao"
Hi ni kwa mujibu wa kifungu kipi cha sheria hiyo au umejitungia tu maneno yako unavyojisikia.

Halafu mkuu mahakamani kuna kanuni muhimu sana kiingereza inaitwa "proof beyond reasonable doubt"
Yaani kosa lazima lionekane na lithibitishwe limefanyika .
Sasa unaposema "unawapasababu ya wao kutafsiri vyovyote wanavyotaka"

Sasa huo utakuwa ni uhayawani unajitafsiria tu unavyotaka wewe ili mradi umtie mtu hatia hata kama hana kosa .
Hiyo sio sawa.
Ukweli uelezwe kilichotakiwa ni huyo binti aachwe akusanye hiyo michango hadi mwisho na kumwangalia angefanya nini na hizo fedha .
Endapo ingetokea hajaziwasilisha serikalini kazitumia tofauti na sheria inavyoelekeza ndipo angekamatwa na kupelekwa mahakamani kushtakiwa kwa mujibu wa sheria..
Waziri Mkuu kakurupuka kaonyesha yupo yupo hajielewi .
Kwa mtazamo wangu huyo bint angwekewa surveillance chini ya financial intellegence unite , hawa jamaa wangejua amekusanya kiasi gani na amekitumiaje.
Sasa ndio angekamatwa.
Moja wapo ya mbinu za kijasusi za kukabiliana na uhalifu ni kuruhusu uhalifu ufanyike huku ukiwa unaufatilia.
Unapata taarifa kuna mtu anaelekea kufanya uhalifu flani sasa ili kupata ushahidi beyond reasonable doubt inabidi umuache hadi atekeleze uhalifu huo ndio unamkamata .
Mbinu hii ingeweza kabisa kutumika kwa Huyu binti ilitakiwa awekewe mtego wa namna hii. (mbinu hii inatumika kwenye makosa ya utapeli na wizi mdogomdogo)
Lazima angeingia kwenye 18 ila kwa hivi wameharibu ushahidi na wamemnasua.
 
Nawaamkua nyote

Tarehe 17 Novemba 2024, Waziri Mkuu akiwa eneo la Kariakoo kukagua zoezi linaloeneelea la uokoaji wa waliokwama chini ya kifusi cha ghorofa iliyoanguka. Alitoa maagizo kwa jeshi la polisi kumkamata Mtanzania aitwaye Niffer ambaye kupitia mitabdaoni alitoa taarifa kuwa amechangisha pesa za za kuwahani wahanga wa ajali ya ghorofa. kuna mambo kadhaa ya kuangazia hapa
  1. Niffer ametoa taarifa ya kuchangisha na kuelezea kiwango alichokikusanya
  2. Waziri Mkuu ameipokea taarifa ya Niffer kama vile anapokea briefings za kiuchunguzi
  3. Waziri Mkuu anatoa agizo la kukamatwa na kuhojiwa Niffer ili aeleze nani kamruhusu kuchangisha tarehe 17 Novemba 2024
  4. Tarehe 18 Novemba 2024, waziri Mkuu anaelekeza polisi wamhoji mmiliki wa jengo lililoanguka. Agizo hilo limekuja baada ya wananchi kuhoji alipo mmiliki wa jengo na kama hajakamatwa tangu siku ya jengo kuanguka.
  5. Jengo limeanguka ahsubuhi saa tatu halafu Mkuu wa Mkoa na vikosi vya uokozi wanafika eneo la tukio saa nane mchana. Hilo jambo halijamkera Waziri Mkuu
Naomba kufahamu, sheria gani imevunjwa ama kukiukwa na Niffer kuchangisha fedha ambapo si mara ya kwanza kuchangisha na kuwasilisha kwa walengwa?

Naomba kufahamu. Ni michango gani ya wahanga iliyolusanywa kupitia serikali na ikawasilishwa kwa walengwa? Nakumbuka michango ya tetemeko la ardhi Kagera ilikusanywa na walengwa hawwkuambulia senti. Vivyo hivyo mafuriko Morogoro wahanga waliishia kusikia redioni michango ambayo haikuwafikia.

Waziri Mkuu atueleze. Matumizi ya fedha za dharurq na majanga chini ya ofisi yake zimetumikqje tangu aingie ofisini?

Kweli ITATUWEKA HURU
Tumia akili tu. Kama huyo mwenzio angekuwa anachangisha pesa zake za kununulia pad au harusi wala si tatizo. Tatizo ni kutumia jambo la kitaifa kwa kuchangisha pesa kwenye account yake.nani anafuatilia kujua exactly alichopata na atakachotoa? Na yeye anachangisha kwa utaratibu upi mahsusi? Yaani ufiwe wewe kwako atokee jirani tu aanze kuchangisha michango from nowhere na wewe useme sawa?atumie msiba wako kuitisha michango we una akili kweli?apewe utaratibu.
 
Hii ni common sense tu kawaida

Kifungu cha 8 cha Kanuni ya Adhabu kinabainisha kuwa kutokujua sheria hakumwondolei mtu hatia.
 
Msilete ushabiki kwenye mambo ya kisheria! Huyo Nifer hajaenda kuuawa bali anahojiwa na mamlaka zitaona nia yake ilikuwa nini. Mamlaka hazina bifu na huyo dada naamini ni ishu ya yeye kutoa ushirikiano tu ishu yake inaisha.

Sema kwa akili zake za mitandaoni ndo utaskia anapost kuwa ana strong arm hayo ndo yanaweza kumkost. Nadhan hajui serikali inavyofanya kazi yeye anajua kuuza bidhaa kutoka China basi. Anafikiri serikali ni kama konteina la bidhaa
Sidhani km huyu binti alikuwa anajibizana na PM
Kabla ya kauli ya PM kwamba akamatwe kulikuwa na kurushiana vijembe na watesi wake hasa wale wanaofanya biashara kama yake, huku wakidai ni tapeli hzo pesa haziendi kwa wahusika zinaenda mfukoni kwake
Mbaya zaidi hapo ametoka kuzindua duka Lake jipya..

So kupost vijembe vile vilikua sio kwa PM bali kwa wale wapinzani wake,
Sasa unajua sisi wabongo tupe sentensi moja hayo maelezo mengine tutajazia wenyewe,ndio wapinzani wake wakapata nguvu ya kumsagia kunguni kuwa kamjibu PM vibaya
 
Ndugu Tanzania hakujawahi kutungwa sheria inayoitwa Public Collection Act.
Embu naomba nijuze hiyo sheria ya public collection act unayoizungumzia wewe ilitungwa lini? Na ni cap ngapi
Acha kukurupuka ndugu unaonyesha jinsi ulivyo hujielewi
Hiyo sheria nimeitafsiri kwa kingereza , nilimaanisha sheria inayohusiana na makusanyo ya fedha za umma inakabiliwa na vifungu vinavyokataza mtu binafsi kukusanya fedha bila kibali.

Kifungu cha 24 cha Sheria ya Fedha za Umma kinatoa miongozo kuhusu matumizi ya fedha za umma, huku kikiweka wazi kuwa ni lazima shughuli zote za ukusanyaji wa fedha zisimamiwe na mamlaka husika.

Sheria inasisitiza uwazi na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha, ili kuzuia matumizi mabaya na kuhakikisha kwamba fedha zinazokusanywa zinaelekezwa kwa malengo yaliyokusudiwa

Niko radhi kurekebishwa
 
Sheria ya Udhibiti wa Fedha na Misaada (The Charitable Collections Act, 2009)

Kifungu cha 3 kinatoa maelezo kuhusu usajili wa taasisi au mashirika yatakayokusanya misaada, na kwamba taasisi hiyo lazima iwe na kibali cha kukusanya fedha.

Kifungu cha 5 kinatoa maelezo ya taratibu za makusanyo ya fedha, na matumizi ya misaada.

Kifungu cha 10 kinahusu adhabu kwa mtu au taasisi itakayokiuka sheria hii, ikiwa ni pamoja na adhabu za kifungo au faini kwa udanganyifu

Madhumuni ya Sheria:
Lengo kuu la Sheria ya Udhibiti wa Fedha na Misaada (2009) ni kudhibiti na kudumisha uwazi na usimamizi mzuri wa makusanyo ya misaada, kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa manufaa ya jamii na wahitaji, na kupunguza uwezekano wa matumizi mabaya au ulaghai.

Kwa kifupi, sheria hii inaweka wazi utaratibu wa kukusanya misaada na fedha za hisani, na inahitaji mtu yeyote anayetaka kukusanya fedha kwa ajili ya maafa au shughuli za kijamii kuwa na kibali na usajili kutoka kwa mamlaka husika.

Hiyo sheria inazihusu taasi sio mtu binafsi.
Na charitable organization zinajishughulisha na mambo.mengi na mengine sio ya kimaafa .
Wewe jamaa utakuwa hujielewi unachanganya madesa
Huyo binti sio charitable organization kwa hiyo hahusiki na hiyo sheria .
Hiyo sheria imeundwa mahsusi kuzibana NGO zinazopokea fedha na kuzitumia tofauti.
 
Hiyo sheria nimeitafsiri kwa kingereza , nilimaanisha sheria inayohusiana na makusanyo ya fedha za umma inakabiliwa na vifungu vinavyokataza mtu binafsi kukusanya fedha bila kibali.

Kifungu cha 24 cha Sheria ya Fedha za Umma kinatoa miongozo kuhusu matumizi ya fedha za umma, huku kikiweka wazi kuwa ni lazima shughuli zote za ukusanyaji wa fedha zisimamiwe na mamlaka husika.

Sheria inasisitiza uwazi na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha, ili kuzuia matumizi mabaya na kuhakikisha kwamba fedha zinazokusanywa zinaelekezwa kwa malengo yaliyokusudiwa

Niko radhi kurekebishwa

Acha kuchanganya madesa .
Nakuelewesha kwa kifupi kwani umeenda sipo.
Fedha ya umma ni fedha yeyote ambayo lazima ikaguliwe na mkagudhi na mdhibiti wa mahesabu ya serikali (CAG) hii ni sifa kuu ya fedha ya umma.
Hii michango anayokusanya huyu binti haiwezi kwa namna yeyote kukaguliwa na CAG .
Hizi fedha huyo binti wakati anazikusanya hazina sifa za kuitwa fedha za umma. (public finances ) kama sheria inavyoeleza maana ya public finances.
Hizi fedha huyo binti akishakwenda kuzikabidhi kwenye kamati ya maafa hapo ndio zinakuwa fedha za umma .
Unajichanganya sana ndugu unanifanya nielewe watanzania wengi kweli ni mambumbumbu wa sheria hata kama wanazijua hizo sheria hawajui zinatumikaje na wapi na katika muktadha upi.
Yaani kabisa una husisha public finances act na fedha anazochanga huyo binti.
Mkuu umeishusha hadhi sana public finance act hilo li lidude likubwa sana linalotoa muongozo wa fedha zote za serikali
 
Back
Top Bottom