Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sitaki kuingilia mabishano yenu, ila unapoenda mahakamani kama kuna sheria mahususi ya jambo husika.
Sheria mahususi na toleo la mwisho lina supersede sheria zingine zozote, kuna sheria ya ‘maafa 2022’ na imeeleza namna ya kukusanya misaada na imetamka mtu pia anaruhusiwa.
Kosa la Niffer kutokueleza michango ataikabidhi serikali, lakini kuchangisha watu kwenye maafa, kwa sheria husika hajavunja sheria. Upuuzi zaidi ni kujibizana na waziri mkuu mitandaoni hapo ni sawa na kununua ugomvi na serikali.
Sheria ipi hiyo inayosema unapewa kibali embu naomba nitajie hiyo sheria pamoja na hicho kifungu.Kapewa kibali na nani? Sheria inasema unapewa kibali na serikali. Yeye alipewa kibali na nani?
Lets start here
Yeye mwenyewe alisema ana mpango wa kwenda kupeleka misaada, hakuna sehemu alisema anapeleka serikalini.Hakuna kosa kama hilo eti la kutokusema nikichangisha fedha nitazikabidhi serikalini.
Kinachotakiwa ni kwamba ukishamaliza kukusanya michango hiyo ni kuiwasilisha tume ya maafa na si vinginevyo.
Ingetakiwa wamwache huyo binti akusanye hiyo michango halafu waone angefanya nini na hizo fedha .
Sasa hapo ndipo kungeweza kutokea kosa kama asingewasilisha michango hiyo kwenye kamati ya maafa.
Kwa sasa wamekurupuka na kuleta taharuki isiyo na ulazima kwenye jamii
Ni vyema kama unataka kuona vifungu
Kwa mfano:
Sheria ya Huduma za Kibinadamu (Charity Act): Inahitaji kuwa na usajili wa kisheria kwa taasisi zinazokusanya fedha kwa ajili ya misaada au huduma za kibinadamu. Kukusanya fedha bila usajili wa kisheria au vibali kutoka kwa mamlaka husika ni kinyume cha sheria.
Sheria ya Uhalifu wa Mtandao (Cybercrimes Act): Ikiwa kukusanya fedha kuna husiana na utapeli mtandaoni, kunaweza kumaanisha ukiukaji wa sheria za uhalifu mtandaoni.
Kuna..nyumayakeeSitaki kuingilia mabishano yenu, ila unapoenda mahakamani kama kuna sheria mahususi ya jambo husika.
Sheria mahususi na toleo la mwisho lina supersede sheria zingine zozote, kuna sheria ya ‘maafa 2022’ na imeeleza namna ya kukusanya misaada na imetamka mtu pia anaruhusiwa.
Kosa la Niffer kutokueleza michango ataikabidhi serikali, lakini kuchangisha watu kwenye maafa, kwa sheria husika hajavunja sheria. Upuuzi zaidi ni kujibizana na waziri mkuu mitandaoni hapo ni sawa na kununua ugomvi na serikali.
Possible, lakini kwa kuwa alikuwa open nadhani shida ni naivety zaidi. Binafsi nampa benefit of the doubt, alikuwa na nia njema.Kuna..nyumayakee
Hili ni janga la ghafla na linafahamika nchi nzima.... so cha kuhoji ni mapato na matumizi kuliko mkusanyajiTunao wachangia barabarani tunawakutaga na vibari na ata wakija kukuomba wanakuonyesha kibali yeye kabali kiko wapi
Sheria ya Udhibiti wa Fedha na Misaada (The Charitable Collections Act, 2009)Mbona hujataja hivyo vifungu sasa , au hata hujui sheria ni kitu gani na inatafsiriwaje.
Sheria yeyote imeundwa kwa vifungu mbalimbali ambavyo ndio vinatoa nguvu au katazo ..
Ungetakiwa utaje mfano kifungu namba flani cha sheria flani kinakataza kitu flani.
Tungeitafuta hiyo sheria na kwenda kwenye hicho kifungu na kukisoma.
Sasa sijui wewe hapa umeeleza kitu gani, ndugu inaelekea hufahamu hata kitu unachokielezea
Sheria ya Usimamizi wa Maafa ya mwaka 2022, inatoa mwongozo kuhusu kukusanya fedha kwa ajili ya maafa. Kifungu cha 21 kinakataza mtu yeyote kukusanya fedha bila kibali cha mamlaka husika. Aidha, kifungu cha 22 kinatoa adhabu kwa wale watakaokiuka masharti haya, ikiwa ni pamoja na faini au kifungo.Sheria ipi hiyo inayosema unapewa kibali embu naomba nitajie hiyo sheria pamoja na hicho kifungu.
Tafadhali acheni kukurupuka wengine sheria tunazijua na tunazisoma kila siku.
Sasa unaposema tu sheria bila kutaja ni sheria gani na kifungu gani mi nakuona wewe ni kama punguwani flani usiejielewa wala usiejua sheria ni kitu gani
Yeye mwenyewe alisema ana mpango wa kwenda kupeleka misaada, hakuna sehemu alisema anapeleka serikalini.
.
Kusema unakusanya tu mpaka mwisho halafu ndio upeleke serikalini bila ya kuwapa taarifa wahusika unakusanya kwa sababu gani huko ni kuwapa sababu ya kutafsiri vyovyote wanavyotaka motive zako, ikiwemo utapeli.
Talaka ya mahakama kabisaWalishaa achana?
Tumia akili tu. Kama huyo mwenzio angekuwa anachangisha pesa zake za kununulia pad au harusi wala si tatizo. Tatizo ni kutumia jambo la kitaifa kwa kuchangisha pesa kwenye account yake.nani anafuatilia kujua exactly alichopata na atakachotoa? Na yeye anachangisha kwa utaratibu upi mahsusi? Yaani ufiwe wewe kwako atokee jirani tu aanze kuchangisha michango from nowhere na wewe useme sawa?atumie msiba wako kuitisha michango we una akili kweli?apewe utaratibu.Nawaamkua nyote
Tarehe 17 Novemba 2024, Waziri Mkuu akiwa eneo la Kariakoo kukagua zoezi linaloeneelea la uokoaji wa waliokwama chini ya kifusi cha ghorofa iliyoanguka. Alitoa maagizo kwa jeshi la polisi kumkamata Mtanzania aitwaye Niffer ambaye kupitia mitabdaoni alitoa taarifa kuwa amechangisha pesa za za kuwahani wahanga wa ajali ya ghorofa. kuna mambo kadhaa ya kuangazia hapa
Naomba kufahamu, sheria gani imevunjwa ama kukiukwa na Niffer kuchangisha fedha ambapo si mara ya kwanza kuchangisha na kuwasilisha kwa walengwa?
- Niffer ametoa taarifa ya kuchangisha na kuelezea kiwango alichokikusanya
- Waziri Mkuu ameipokea taarifa ya Niffer kama vile anapokea briefings za kiuchunguzi
- Waziri Mkuu anatoa agizo la kukamatwa na kuhojiwa Niffer ili aeleze nani kamruhusu kuchangisha tarehe 17 Novemba 2024
- Tarehe 18 Novemba 2024, waziri Mkuu anaelekeza polisi wamhoji mmiliki wa jengo lililoanguka. Agizo hilo limekuja baada ya wananchi kuhoji alipo mmiliki wa jengo na kama hajakamatwa tangu siku ya jengo kuanguka.
- Jengo limeanguka ahsubuhi saa tatu halafu Mkuu wa Mkoa na vikosi vya uokozi wanafika eneo la tukio saa nane mchana. Hilo jambo halijamkera Waziri Mkuu
Naomba kufahamu. Ni michango gani ya wahanga iliyolusanywa kupitia serikali na ikawasilishwa kwa walengwa? Nakumbuka michango ya tetemeko la ardhi Kagera ilikusanywa na walengwa hawwkuambulia senti. Vivyo hivyo mafuriko Morogoro wahanga waliishia kusikia redioni michango ambayo haikuwafikia.
Waziri Mkuu atueleze. Matumizi ya fedha za dharurq na majanga chini ya ofisi yake zimetumikqje tangu aingie ofisini?
Kweli ITATUWEKA HURU
Hii ni common sense tu kawaidaTumia akili tu. Kama huyo mwenzio angekuwa anachangisha pesa zake za kununulia pad au harusi wala si tatizo. Tatizo ni kutumia jambo la kitaifa kwa kuchangisha pesa kwenye account yake.nani anafuatilia kujua exactly alichopata na atakachotoa? Na yeye anachangisha kwa utaratibu upi mahsusi? Yaani ufiwe wewe kwako atokee jirani tu aanze kuchangisha michango from nowhere na wewe useme sawa?atumie msiba wako kuitisha michango we una akili kweli?apewe utaratibu.
Sidhani km huyu binti alikuwa anajibizana na PMMsilete ushabiki kwenye mambo ya kisheria! Huyo Nifer hajaenda kuuawa bali anahojiwa na mamlaka zitaona nia yake ilikuwa nini. Mamlaka hazina bifu na huyo dada naamini ni ishu ya yeye kutoa ushirikiano tu ishu yake inaisha.
Sema kwa akili zake za mitandaoni ndo utaskia anapost kuwa ana strong arm hayo ndo yanaweza kumkost. Nadhan hajui serikali inavyofanya kazi yeye anajua kuuza bidhaa kutoka China basi. Anafikiri serikali ni kama konteina la bidhaa
Hiyo sheria nimeitafsiri kwa kingereza , nilimaanisha sheria inayohusiana na makusanyo ya fedha za umma inakabiliwa na vifungu vinavyokataza mtu binafsi kukusanya fedha bila kibali.Ndugu Tanzania hakujawahi kutungwa sheria inayoitwa Public Collection Act.
Embu naomba nijuze hiyo sheria ya public collection act unayoizungumzia wewe ilitungwa lini? Na ni cap ngapi
Acha kukurupuka ndugu unaonyesha jinsi ulivyo hujielewi
Sheria ya Udhibiti wa Fedha na Misaada (The Charitable Collections Act, 2009)
Kifungu cha 3 kinatoa maelezo kuhusu usajili wa taasisi au mashirika yatakayokusanya misaada, na kwamba taasisi hiyo lazima iwe na kibali cha kukusanya fedha.
Kifungu cha 5 kinatoa maelezo ya taratibu za makusanyo ya fedha, na matumizi ya misaada.
Kifungu cha 10 kinahusu adhabu kwa mtu au taasisi itakayokiuka sheria hii, ikiwa ni pamoja na adhabu za kifungo au faini kwa udanganyifu
Madhumuni ya Sheria:
Lengo kuu la Sheria ya Udhibiti wa Fedha na Misaada (2009) ni kudhibiti na kudumisha uwazi na usimamizi mzuri wa makusanyo ya misaada, kuhakikisha kuwa fedha hizo zinatumika kwa manufaa ya jamii na wahitaji, na kupunguza uwezekano wa matumizi mabaya au ulaghai.
Kwa kifupi, sheria hii inaweka wazi utaratibu wa kukusanya misaada na fedha za hisani, na inahitaji mtu yeyote anayetaka kukusanya fedha kwa ajili ya maafa au shughuli za kijamii kuwa na kibali na usajili kutoka kwa mamlaka husika.
Nadhani tungenza na Steve Nyerere kipindi cha msiba wa Kanumba kama fundisho yasingetokea yote hayaMitanzania mizezeta inaamuka tu huko inajiona yenyewe ndio inauchungu kuliko Serikali yenye watu.
Vitu basic kama hivyo mtu hajui.Huyo ilitakiwa awekwe ndani hata miezi 6 iwe fundisho.
Hiyo sheria nimeitafsiri kwa kingereza , nilimaanisha sheria inayohusiana na makusanyo ya fedha za umma inakabiliwa na vifungu vinavyokataza mtu binafsi kukusanya fedha bila kibali.
Kifungu cha 24 cha Sheria ya Fedha za Umma kinatoa miongozo kuhusu matumizi ya fedha za umma, huku kikiweka wazi kuwa ni lazima shughuli zote za ukusanyaji wa fedha zisimamiwe na mamlaka husika.
Sheria inasisitiza uwazi na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha, ili kuzuia matumizi mabaya na kuhakikisha kwamba fedha zinazokusanywa zinaelekezwa kwa malengo yaliyokusudiwa
Niko radhi kurekebishwa