Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,896
- 4,058
Yanga inamatatizo mengi ya kiuchezaji ila kwa sababu ligi yetu haina timu zenye ubora wa kuiadhibu ndio huwa hawaadhibiwi.
1.Matatizo sehemu ya mabeki
Bangala licha ya ubora wake hana kasi hasa ikitokea kaunta.Pili Dickson Job ni mfupi hii ni hatari unapokutana na wachezaji warefu km wa Al hilal. Tatu,upande wa kulia Juma Shabani kuna mda anapanda sana na mbaya zaidi huwa anapoteza mipira kirahisi akiwa juu na kuhatarisha eneo la ulinzi.Nne upande wa kushoto bado kocha hajapata beki halisi. Kibwana ni beki mzuri lakini hawezi kushambulia hasa kupiga krosi kwa mguu wa kushoto. Leo mechi nzima km sijakosea hajapiga krosi hata moja.
2. Eneo la katikati
Aucho licha ya kuwa na uwezo mzuri wa kumiliki mpira anachangamoto ya kukosa speed kwa kuipeleka timu mbele au kuwahi kuzuia pindi timu inashambuliwa. Pili anacheza ki-father sana.
3. Pembeni upande wa kulia.
Moloko na Kisinda wote ni wakimbiaji lakini akili ya mpira ni ndogo. Wanahitajika mawinga wenye sifa km za Morrison.
4. Upande kushoto kwa Morrison
Kiuchezaji bado kocha hajui namna nzuri ya kumtumia. Morrison anapenda mpira wa kushambulia kwa kasi kwa staili ya nipe nikupe. Mara nyingi alikuwa anapewa mipira na kuachwa peke ake.
5. Mayele.
Jamaa anajua ila kuna muda anazidisha ubinafsi. Kwenye mechi za kimataifa lazima wachezaji mcheze kitimu na kimipango zaidi kuliko mtu mmoja mmoja.
6.Yanga inakosa Sharpness.
Sijui kwanini wachambuzi wengi hawalizungumzii hili tatizo. Yanga maranyingi wanacheza game zao kwa Temper ya chini na hawana Sharpness na uharaka wa pasi na maamuzi. Kwenye mechi kubwa Sharpness ni sifa muhimu sana.
7. Kocha Nabi.
Hana plan B pindi mbinu ya awali ikigoma. Kiuchezaji Yanga inatabirika sana. Diara ataanza mpira kwa Dickson Job,Job atampa Bangala. Bangala atampa Aucho na baadae kwa Juma Shabani. Juma ataurudisha kwa Diara ambae ataupiga mpira mbele.Pattern ya uchezaji ni ile ile mwanzo mwisho. Yanga wanaongeza kasi kidogo pale tu wanapovuka mstari wa katika. Kwa staili ya namna hii ni rahisi timu pinzani kuwazuia.