Aramun
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 461
- 2,213
Baada ya hospitali ya Agakhan kujitoa kwenye kuwahudumia wateja "Executive" wa NHIF, mashirika makubwa ya umma yanayotumia NHIF nayo yanajiandaa kutoongeza mkataba wao na NHIF.
Kama ilivyokuwa zamani haya mashirika yalikuwa yanatumia mifuko mingine ya bima za afya kama Strategis na Assemble(Zamani AAR). Hayati Rais JPM alipoingia madarakani ndipo akafanya mpango mashirika yote ya umma yakaanza kutumia NHIF.
Haya mashirika yapo category ya "NHIF Supplimentary Benefit Scheme" ambapo michango ya wanachama ni mikubwa kulinganisha na watumishi wengine ambao wao hukatwa 3% tu ya mshahara ghafi.
My take: Serikali kama imeshindwa kuiendesha NHIF, iruhusu watumishi wawe na uhuru wa kuchagua mifuko ya bima ya afya mingine wanayoitaka. Hawa NHIF wanapata kiburi cha kufanya madudu wanayofanya kwa sababu hawana mshindani kwenye soko.
Soma Pia: Kinachoendelea NHIF ni reflection ya Incompetence za Viongozi, Wivu na Ushauri Mbovu kwa Waziri wa Afya
Kwa sasa NHIF haipo kumsaidia mteja wake, bali wamejikita katika kubana matumizi yasiyo na uhalisia wa gharama zilivyo kwa sasa. Kwa akili ya kawaida kabisa sote tunaelewa gharama za maisha hazijawahi kushuka duniani kote, zinapaa siku hadi siku, na hii inajumlisha pia gharama za matibabu, sasa inakuwaje leo NHIF wanafosi kujipangia bei ambazo haziakisi uhalisia wa vitu na huduma zinazotolewa huko mahospitalini?
Ni kwa nini NHIF walifosi kujipangia gharama zao bila kuwasikiliza wadau wake?
Mteja hawezi kulipa bima ya "Executive Level" kisha unampangia mahali pa kutibiwa! Huu mfuko kwa sasa serikali isipoingilia kati unaenda kujifia kibudu.