KERO NMB, kwanini mtumie saa 24 kushughulikia muamala ambao HAUJAKAMILIKA?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nilikuwa natoa hela bila card (PESA FASTA) kwenye ATM ya NMB DODOMA leo, baada ya kumaliza kutoa kwenye simu nikawa nasubiria meseji ya namba ya siri ili iniwezeshe kutoa kwa kwenye ATM lakini nilisubiria kwa zaidi ya dakika 15 lakini sikupata Meseji.

Nikawapigia huduma kwa wateja wakaniambia nisubiri masaa 24 hela zangu zitarudishwa kwenye Account yangu. Sasa shida yangu mimi ni Namba ya siri ambapo nilitegemea angeniambia kwamba kunachangamoto ya mtandao ila namba ya siri inakuja sasa hivi badala yake naambiwa nisubiri baada ya Masaa 24 ndio hela yangu itarudi kwenye Accout.

Inamaana hela hazipo kwangu na wamezishikilia kana kwamba hela ni zao mpaka wananiambia watazirudisha baada ya masaa 24 hii kisheria imekaaje?

Sasa katika kipindi kama hiki ambapo mtu hutembei na cash unategeme hela ipo benki inapokukuta changamoto kama hii inakuwa kero ndipo najiuliza kwanini itumie masaa 24 kushughulikia muamala ambao haujakamilika, na hili pia lipo hata kwenye makampuni ya simu. Kimsingi hawatutendei haki sisi matumiaji wao.
 
Seran naomba msaada
 
Back
Top Bottom