NMB "Mshiko Fasta" ilitakiwa ifanye kazi kama Songesha na ''Nipige Tafu" za makampuni ya simu. Mnafeli wapi?

Mnawatakia nini warahisishe mambo kiasi hicho?
 
Ungeuliza riba ndogo kulingana na nani???

Wale pesa x,unachukua 30,000 unarudisha 60,000
Riba ni riba

Tunajadili kilichopo hapa.. hizo za kina X sizijui
 
Tulitarajia benki hasa hii ya wanyonge wawe na riba nafuu, na wenyewe wameungana na wale wa mkopo kausha damu ili kuendelea kunyonya damu za watanzania wanyonge.....yaani mkopo elfu 30, riba karibu buku 3!
 
Pesa X nilikua siijui sasa kuna binti fulani akachukua hela na kuniweka kama mdhamini ,kiukweli niseme wale jamaa wana mikwara sijawahi ona kabisa mara tuna rb zenu,mara mtakufa vibaya nyie na utapeli wenu hujakaa sawa unafungua whatsap haoo hadi whatsap wanatimba profile picha wameweka makomandoo hahahaa wale watu wa pesa x balaa hapo nimewekwa udhamini mwenyewe sijui
 
Sikuhiz ukiwa na kitambulisho tu unafungua account
 
Sijajua hata maana leo ndo kwa mara ya kwanza baada ya kunasa haswa nikaone nijaribu huku

Ikumbukwe juzi salary advance tayari nilichukua kiasi kadhaa na ikatiwa chini ya pua yote
Wafanyakazi wengi ni masikini kwa sababu ya mabenk,
 
Kama umeshindwa kulipa kwenye simu ndo utaweza bank
 
Sasa wakituma meseji wanasema hamna riba tena mpaka unaeza kopa laki 5 bila riba yoyote? Mimi nilijua ni sms za kutengeneza za mitandaon kumbe ni mkopo wa NMB.
 
Sasa wakituma meseji wanasema hamna riba tena mpaka unaeza kopa laki 5 bila riba yoyote? Mimi nilijua ni sms za kutengeneza za mitandaon kumbe ni janjajanja ya NMB.
Jamani nashukuru huku tunapeana ufahamu Wa mambo .
Mambo kama haya yangekuwa yanajadiliwa fb public Ili na wahusika wajue kwamba watz wanaelewa wanachofanya niujanja ujanja uleule kama kausha damu kwanini kama wanataka kutusaidia watu wachin baadhi ya mambo hayako wazo? Kunani hapo!
Nilidhani hata mtu unapotoa au kuweka ilitakiwa waonyeshe makato na salio lililobaki Sasa wao salio hd uulize wakukate pesa duu kweli mambo ya pesa hayana huruma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…