NMB, NAOMBA MNIPE MAELEZO NA SULUHISHO LA TATIZO HILI

OgaBoy

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2022
Posts
4,031
Reaction score
6,156
Nimekuwa nikitumia NMB Mkononi kwenye simu yangu ya zamani. Kwa bahati mbaya, simu hiyo iliharibika. Baada ya kupata simu mpya, nime-install NMB Mkononi na kujaribu kuingia kwenye akaunti yangu, lakini nimekuwa nikishindwa.

Nimekuwa nikijaribu kwa takribani miezi mitatu, lakini bado sijafanikiwa kutumia huduma yangu kwenye simu mpya.

Nilipofika NMB kuomba msaada, nikaelezwa kwamba ili niweze kutumia NMB Mkononi kwenye simu mpya, ni lazima niwe na simu yangu ya zamani kwa ajili ya verification.

Hapa ndipo ninapopata changamoto.

Simu ya zamani ikiwa imeharibika kabisa, mteja afanye nini?
Mimi ni yuleyule mwenye akaunti. Taarifa zangu zipo kwenye mfumo wa NMB, namba yangu ya simu ipo, akaunti yangu ipo, na taarifa nyingine za utambulisho nilizotumia kufungua akaunti zipo.

Pia kwenye NMB Mkononi kuna fingerprint kama njia mbadala ya password, na fingerprint hiyo inahusishwa na matumizi ya huduma ndani ya mfumo wa NMB Mkononi. Kwa hiyo ninashindwa kuelewa kwa nini mteja mwenye simu mpya asiweze kuthibitishwa kwa kutumia njia nyingine salama zinazopatikana kwenye mfumo wa benki.

Naelewa kabisa kwamba NMB lazima iwe na usalama mkubwa ili kulinda akaunti za wateja. Lakini usalama haupaswi kumfanya mteja halali ashindwe kupata huduma yake kwa sababu simu yake ya zamani imeharibika au haipo tena.

Nimekuwa nikijaribu kupata suluhisho kwa muda mrefu bila mafanikio, na kwa kweli hali hii imenipa usumbufu mkubwa.

Naomba NMB mnisaidie kupata suluhisho la kutumia NMB Mkononi kwenye simu yangu mpya bila kutegemea simu yangu ya zamani ambayo haipo tena.

Mteja akibadilisha simu, huduma ya benki inapaswa kuwa na utaratibu salama wa kumtambua na kumruhusu kuendelea kutumia akaunti yake kwenye kifaa kipya.

NMB TAWI LA XXX MALL MNAFUKUZA WATEJA KWA KUWEKA CUSTOMER CARE WASIOJIELEWA KAMA HII SI SHIDA ANGALIENI CUSTOMER CARE WENU.

Nmb
 
Mimi cjabadilisha cm wala kurenew line, mara zote uwa natumia nmb mkononi lakini ni muda sasa inaniandikia hivi pia nikipiga *150*66# menu haifanyi kazi. Nimeenda NMB branch XXX kama mara tatu ivi, wameahindwa kusolve. Nimepata usumbufu mkubwa sana. Kibaya zaidi nilishaachaga kutumia card muda mrefu sana hadi ikawa imeexpire na ckufatilia nyingine. Sasa changamoto ilipojitokeza imekuwa usumbufu sana any time natemana na bank hii.
IMG_20261002_153908_390.jpeg
 
Attachments

  • IMG_20261002_153908_390.jpeg
    IMG_20261002_153908_390.jpeg
    51.1 KB · Views: 4
Mimi cjabadilisha cm wala kurenew line, mara zote uwa natumia nmb mkononi lakini ni muda sasa inaniandikia hivi pia nikipiga *150*66# menu haifanyi kazi. Nimeenda NMB branch XXX kama mara tatu ivi, wameahindwa kusolve. Nimepata usumbufu mkubwa sana. Kibaya zaidi nilishaachaga kutumia card muda mrefu sana hadi ikawa imeexpire na ckufatilia nyingine. Sasa changamoto ilipojitokeza imekuwa usumbufu sana any time natemana na bank hii .

Mimi cjabadilisha cm wala kurenew line, mara zote uwa natumia nmb mkononi lakini ni muda sasa inaniandikia hivi: ACCOUNT ALREADY TAKEN pia nikipiga *150*66# menu haifanyi kazi. Nimeenda NMB branch XXX kama mara tatu ivi, wameahindwa kusolve. Nimepata usumbufu mkubwa sana. Kibaya zaidi nilishaachaga kutumia card muda mrefu sana hadi ikawa imeexpire na ckufatilia nyingine. Sasa changamoto ilipojitokeza imekuwa usumbufu sana any time natemana na bank hii .
 
Attachments

  • IMG_20261002_153919_906.jpeg
    IMG_20261002_153919_906.jpeg
    58.8 KB · Views: 7
Hao watu pumbavu sana ,wanashindwa akili na Airtel,voda ,yas app.Hata ukiifuta huo mlolongo wa kuirudisha mpaka uende bank tena inakuwaje makampuni ya simu yanaweza ,Bank inashindwa .Maform kibaooo .Badilikeni shenzi.
 
Nimekuwa nikitumia NMB Mkononi kwenye simu yangu ya zamani. Kwa bahati mbaya, simu hiyo iliharibika. Baada ya kupata simu mpya, nime-install NMB Mkononi na kujaribu kuingia kwenye akaunti yangu, lakini nimekuwa nikishindwa.

Nimekuwa nikijaribu kwa takribani miezi mitatu, lakini bado sijafanikiwa kutumia huduma yangu kwenye simu mpya.

Nilipofika NMB kuomba msaada, nikaelezwa kwamba ili niweze kutumia NMB Mkononi kwenye simu mpya, ni lazima niwe na simu yangu ya zamani kwa ajili ya verification.

Hapa ndipo ninapopata changamoto.

Simu ya zamani ikiwa imeharibika kabisa, mteja afanye nini?

Mimi ni yuleyule mwenye akaunti. Taarifa zangu zipo kwenye mfumo wa NMB, namba yangu ya simu ipo, akaunti yangu ipo, na taarifa nyingine za utambulisho nilizotumia kufungua akaunti zipo.

Pia kwenye NMB Mkononi kuna fingerprint kama njia mbadala ya password, na fingerprint hiyo inahusishwa na matumizi ya huduma ndani ya mfumo wa NMB Mkononi. Kwa hiyo ninashindwa kuelewa kwa nini mteja mwenye simu mpya asiweze kuthibitishwa kwa kutumia njia nyingine salama zinazopatikana kwenye mfumo wa benki.

Naelewa kabisa kwamba NMB lazima iwe na usalama mkubwa ili kulinda akaunti za wateja. Lakini usalama haupaswi kumfanya mteja halali ashindwe kupata huduma yake kwa sababu simu yake ya zamani imeharibika au haipo tena.

Nimekuwa nikijaribu kupata suluhisho kwa muda mrefu bila mafanikio, na kwa kweli hali hii imenipa usumbufu mkubwa.

Naomba NMB mnisaidie kupata suluhisho la kutumia NMB Mkononi kwenye simu yangu mpya bila kutegemea simu yangu ya zamani ambayo haipo tena.

Mteja akibadilisha simu, huduma ya benki inapaswa kuwa na utaratibu salama wa kumtambua na kumruhusu kuendelea kutumia akaunti yake kwenye kifaa kipya.

NMB TAWI LA XXX MALL MNAFUKUZA WATEJA KWA KUWEKA CUSTOMER CARE WASIOJIELEWA KAMA HII SI SHIDA ANGALIENI CUSTOMER CARE WENU.

Nmb
Broo nenda kwenye ATM AINGIZA CARD YAKO WEKA PASSWORD THEN HUDUMA NYINGINE CHAGUA WEZESHA NMB MKONONI INGIZA NAMBA YA SIRI AFU CONFIRM then nenda kwenye simu yako download nmb app fata procedure itakubali.
 
Wabadilike mbona app za mitandao ya simu ,tunafuta tunarudisha hakuna usumbufu.Ila mabenki milolongo kibao mara jaza hiki mara nenda ATM .
 
Fanya ivyo mkuu technology inabadilika kila saa nadhani pengine ni mambo yakiusalama labda.
 
  • Thanks
Reactions: EEX
Back
Top Bottom