NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Habari zenu wapendwa?

Naomba kuuliza kuhusu matumizi ya App ya NMB Tanzania yanakuwaje kwa sababu kila ninapojaribu kuuliza kuangalia salio langu kupitia NMB App nakuta salio limepungua kwenye Account yangu

Tena makato sio ya kitoto ni makubwa Sana najiuliza hii ni kwangu tu au kwa watumiaji wote wa NMB App. Msaada Tafadhali.

Pia naomba kufahamu kwa yeyote anaefahamu kuhusu Mambo haya,ni benki gani cheep zaidi katika swala zima la makato lipokuja swala la kutoa pesa au mikopo na riba zao? Msaada Tafadhali.
Hapo mwisho umeuliza vitu vingi kwa wakati.
Kukujibu kwa ufupi hakuna bank iliyokamilika kwa 100%
BANCABC hawana makato ya mwezi kabisa, kutoa pesa kwenye ATM zao bei chee. ila kwenye mikopo nasikia maumivu.
EQUITY kuuliza ralio bure, hawana makato ya mwezi, wana matawi machache.
CRDB mikopo riba ndogo, matawi mengi ila makato makubwa ya uendeshaji wa akaunti
 
Ndio. Fungua App. Bonyeza Taarifa ya Kielectroniki utaingiza Email na Muda chagua tu 1 month. Unatumiwa kwenye email dakika iyo iyo.
Baada ya kuipata hiyo statement nikaiprint naweza kuipeleka bank wakanisainia na kugonga mhuri, nataka kufanya hivyo ili kuepuka kupanga foleni ya kuomba bank statement.
 
Naomba kujua aina za makato ya bank ya nmb na gharama zake, yaani kwa mfano kutoa pesa kwenye ATM ni shilingi ngapi na makato ya kila mwezi (kama yapo) ni shilingi ngapi . Kwa ufupi natamani kujua makato yote kwenye account. Kiukweli nimeona hawa jamaa wanachukua hela nyingi sana kwenye account yangu ambayo sielewi inaenda wapi. Kwa mfano juzi nilikuwa na 335000/= nikatoa 330000 kwenye ATM lkn kuja kuangalia salio kupitia app yao nakuta 1700/= tu sasa inamaana kutoa hela inacost 3300??? Naombeni msaada juu ya hili. Na sio hivo tu yaani hawa jamaa ukiacha hela kwenye account ni lazima ipunguzwe
 
Hapo mwisho umeuliza vitu vingi kwa wakati.
Kukujibu kwa ufupi hakuna bank iliyokamilika kwa 100%
Naomba kujua aina za makato ya bank ya nmb na gharama zake, yaani kwa mfano kutoa pesa kwenye ATM ni shilingi ngapi na makato ya kila mwezi (kama yapo) ni shilingi ngapi . Kwa ufupi natamani kujua makato yote kwenye account. Kiukweli nimeona hawa jamaa wanachukua hela nyingi sana kwenye account yangu ambayo sielewi inaenda wapi. Kwa mfano juzi nilikuwa na 335000/= nikatoa 330000 kwenye ATM lkn kuja kuangalia salio kupitia app yao nakuta 1700/= tu sasa inamaana kutoa hela inacost 3300??? Naombeni msaada juu ya hili. Na sio hivo tu yaani hawa jamaa ukiacha hela kwenye account ni lazima ipunguzwe
 
Kwa nini nyie kufungua account mnacharge alfu kumi wakati bank zingine kufungua account ni bure.
 
NMB Tanzania naomba kuuliza mbona kwenye riba za fixed account kwenye website yenu kupitia FDR calculator mumeweka asilimia 9.5 lakini ukienda kufungua riba mnaweka asilimia 5
 
Nmb Tanzania, inachukua muda gani kutatuliwa kwa changamoto ya kubadili saini kwenye mfumo baada ya mhusika kukamilisha Taratibu zote?
 
NMB Tanzania Tawi la Mbezi Luis foleni ni ndefu dirisha linalotoa huduma ni moja msaada unahitajika tumechoka na foleni
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1.
Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Mbona sielewi haya makato ya takriba shilingi elfu sita ndani ya wiki moja kwenye akaunti yangu???? Yalijitokeza siku kadhaa zilizopita nikapuuza. Leo tena naangalia salio kupitia NMB mkononi nakuta tena mmekata elfu sita. Why?
 
Naomba kujua aina za makato ya bank ya nmb na gharama zake, yaani kwa mfano kutoa pesa kwenye ATM ni shilingi ngapi na makato ya kila mwezi (kama yapo) ni shilingi ngapi . Kwa ufupi natamani kujua makato yote kwenye account. Kiukweli nimeona hawa jamaa wanachukua hela nyingi sana kwenye account yangu ambayo sielewi inaenda wapi. Kwa mfano juzi nilikuwa na 335000/= nikatoa 330000 kwenye ATM lkn kuja kuangalia salio kupitia app yao nakuta 1700/= tu sasa inamaana kutoa hela inacost 3300??? Naombeni msaada juu ya hili. Na sio hivo tu yaani hawa jamaa ukiacha hela kwenye account ni lazima ipunguzwe
Haya maudhi yamenifika na mimi. Wananikata elfu sita kwa wiki sijui for what reason. Ngoja nimalize jambo langu niachane nao kabisa nirudi CRDB
 
NMB tunatambua mchango wetu ktk ustawi wa kijamii - tatizo pekee kwenu ni kuendelea kufanya kazi kwa kutumia njia nyingi za kizamani "kwa ukongwe wenu yafaa benki zingine ziwanyatie kwa mbali sana na itatokana na benki yenu itakavyowekeza ktk planning".

Endeleeni pia kuona uwezekano wa kuwekeza ktk kata zilizochangamka na kuimarika kwa mzunguko wa fedha.
 
Back
Top Bottom