NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Hapo mwisho umeuliza vitu vingi kwa wakati.
Kukujibu kwa ufupi hakuna bank iliyokamilika kwa 100%
 
Ndio. Fungua App. Bonyeza Taarifa ya Kielectroniki utaingiza Email na Muda chagua tu 1 month. Unatumiwa kwenye email dakika iyo iyo.
Baada ya kuipata hiyo statement nikaiprint naweza kuipeleka bank wakanisainia na kugonga mhuri, nataka kufanya hivyo ili kuepuka kupanga foleni ya kuomba bank statement.
 
Naomba kujua aina za makato ya bank ya nmb na gharama zake, yaani kwa mfano kutoa pesa kwenye ATM ni shilingi ngapi na makato ya kila mwezi (kama yapo) ni shilingi ngapi . Kwa ufupi natamani kujua makato yote kwenye account. Kiukweli nimeona hawa jamaa wanachukua hela nyingi sana kwenye account yangu ambayo sielewi inaenda wapi. Kwa mfano juzi nilikuwa na 335000/= nikatoa 330000 kwenye ATM lkn kuja kuangalia salio kupitia app yao nakuta 1700/= tu sasa inamaana kutoa hela inacost 3300??? Naombeni msaada juu ya hili. Na sio hivo tu yaani hawa jamaa ukiacha hela kwenye account ni lazima ipunguzwe
 
Hapo mwisho umeuliza vitu vingi kwa wakati.
Kukujibu kwa ufupi hakuna bank iliyokamilika kwa 100%
 
Kwa nini nyie kufungua account mnacharge alfu kumi wakati bank zingine kufungua account ni bure.
 
NMB Tanzania naomba kuuliza mbona kwenye riba za fixed account kwenye website yenu kupitia FDR calculator mumeweka asilimia 9.5 lakini ukienda kufungua riba mnaweka asilimia 5
 
Nmb Tanzania, inachukua muda gani kutatuliwa kwa changamoto ya kubadili saini kwenye mfumo baada ya mhusika kukamilisha Taratibu zote?
 
NMB Tanzania Tawi la Mbezi Luis foleni ni ndefu dirisha linalotoa huduma ni moja msaada unahitajika tumechoka na foleni
 
Mbona sielewi haya makato ya takriba shilingi elfu sita ndani ya wiki moja kwenye akaunti yangu???? Yalijitokeza siku kadhaa zilizopita nikapuuza. Leo tena naangalia salio kupitia NMB mkononi nakuta tena mmekata elfu sita. Why?
 
Haya maudhi yamenifika na mimi. Wananikata elfu sita kwa wiki sijui for what reason. Ngoja nimalize jambo langu niachane nao kabisa nirudi CRDB
 
NMB tunatambua mchango wetu ktk ustawi wa kijamii - tatizo pekee kwenu ni kuendelea kufanya kazi kwa kutumia njia nyingi za kizamani "kwa ukongwe wenu yafaa benki zingine ziwanyatie kwa mbali sana na itatokana na benki yenu itakavyowekeza ktk planning".

Endeleeni pia kuona uwezekano wa kuwekeza ktk kata zilizochangamka na kuimarika kwa mzunguko wa fedha.
 
Mbona hamjibu maswali ya wadau? au mjibu hoja yuko likizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…