CHARLES KIHOMBO
Member
- Feb 28, 2014
- 76
- 19
wazito sana katika huduma!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nmb mtwara baraka mwasandube jamani kaka yule mpeni ufanyakazi boraaa
maana anajituma hadi raha
Aaaghh
Rekebisheni Nmb mobile kuna muda haileti majibu ukituma pesa,
Nishawahi tuma pesa kwa mtu mara mbili ikala kwangu.
Then ukitoa pesa tu kwe atm ndo inaleta notification
Kwanini isiwe kila process inayofanyika kwe account yako unapata taarifa?mfano unapoweka pesa.
Majibu pls!!!!!
Ndugu wana JamiiForums,
Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.
Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.
Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe Siri)
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.
4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Hapo sio NMB anaefanya hivyo, ni moja ya vigezo na masharti yanayotolewa na bank kuu hivyo bank yoyote unapokwenda kuchukua mkopo lazima watoe 40% ya salaryNMB, Jamani Sisi tunamini kuwa ninyi ndo watu unaojua updates za kupanda kwa thamani ya fedha duniani, hivyo mnajua gharama za maisha. sasa kwa nini BADO MNANG'ANG'ANIA KIWANGO CHA 40% KWA MIKOPO YA WAFANYAKAZI? wakati gharama za maisha zimepanda? TUNAOMBA MUONGEZE MFANYAKAZI ACHUKUE MKOPO 60% YA MSHAHARA WAKE, Na Hii Ndio Itampa Fursa Hata Ya Kuchagua Muda Wa Marejesho Lakini Kwa 40% Inamlazimisha Mtu Achukue Miaka 5,maana Ukisema Uchukue Miaka 3, Utapata Hela Ndogo Sana. Alafu Nmb Tawi La "Kilombero" Tunaomba Huyo Afisa Wenu Mikopo Wa Kiume Huyo (jamaa)anaekaa Nyuma Ya Afisa "Dada Grace", Hasiusike Kabsa Kuwapigia Mahesabu Wafanyakazi Wa Kilombero Kwani Hajui Kabsa,ni Mzembe Anawakosesha W/kazi Na Kuwasababishia Kupata Hela Ndogo, Tunaomba Mikopo Ya "Salaried Workers Loan" Mfanyakazi Akatwe 60% Ya Mshahara Wake Na Sio 40%kama Ilvyo Sasa, Kama Vp Mseme Mmeshindwa Ili Benki Ya Crdb Ichukue Nafasi Tunajua Mmetoa Rushwa Kampuni Ili Crdb Wasipate Kibali. Naomba Kuwasilisha
Lini NMB mtaacha ubabaishaji na wizi .
Mtu ananunua LUKU kupitia NMB mobile halafu hatumiwi meseji ya umeme alionunua wakati pesa imekatwa?
Wizi huu wa money transfer ya kukata sh.3500/= kwenye NMB mobile kwa kununua umeme wa sh.5000/= utaisha lini ? Huu ni wizi mkubwa.
Kama serikali ingekua inafanyia kazi malalamko ya wananchi kuibiwa kwenye hii benki mpaka sasa ingetakiwa iwe imeshafungwa.
NMB badilikeni. Mnamapungufu makubwa sana.