NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

nmb mtwara baraka mwasandube jamani kaka yule mpeni ufanyakazi boraaa
maana anajituma hadi raha

Kuna mwingine alikuwa tawi la Morogoro rd huku dar sijui aliishia wapi,alikuwa anajituma kiasi kwamba unagundua watanzania tunapungukiwa uwajibikaji. Kama aliachishwa kazi basi ni sababu ya majungu!
 
Lini NMB mtaacha ubabaishaji na wizi .
Mtu ananunua LUKU kupitia NMB mobile halafu hatumiwi meseji ya umeme alionunua wakati pesa imekatwa?

Wizi huu wa money transfer ya kukata sh.3500/= kwenye NMB mobile kwa kununua umeme wa sh.5000/= utaisha lini ? Huu ni wizi mkubwa.

Kama serikali ingekua inafanyia kazi malalamko ya wananchi kuibiwa kwenye hii benki mpaka sasa ingetakiwa iwe imeshafungwa.

NMB badilikeni. Mnamapungufu makubwa sana.
 
NMB,wanaboa sana,NMB handeni ni moja kati ya matawi ya NMB yenye Huduma poor niliowahi kuyaona,siku 1 nilihitaji kutoa pesa million 2,nilikutana na urasimu wa hali ya juu eti wanasema sahihi hawaiamin nirudi mpaka karatu,NMB nilipofungulia akaunt ,niliwachukia sana Hawa watu,nitoke handeni niende KARATU can you imagine?
 

uNATAKA UJUE mshahara ukiingia eeeh
 
Mbona hao NMB mliowasifia hawajibu maswali ya watu
 
Naomba msaada watu wa nmb,
Kwanini leo asubui nimetuma nimetuma pesa kutoka kwenye acc yangu ya m-pesa kwenda nmb,cha kushangaza ikarudishwa je nini tazizo??
 
NMB, Jamani Sisi tunamini kuwa ninyi ndo watu unaojua updates za kupanda kwa thamani ya fedha duniani, hivyo mnajua gharama za maisha. sasa kwa nini BADO MNANG'ANG'ANIA KIWANGO CHA 40% KWA MIKOPO YA WAFANYAKAZI? wakati gharama za maisha zimepanda?

TUNAOMBA MUONGEZE MFANYAKAZI ACHUKUE MKOPO 60% YA MSHAHARA WAKE, Na Hii Ndio Itampa Fursa Hata Ya Kuchagua Muda Wa Marejesho Lakini Kwa 40% Inamlazimisha Mtu Achukue Miaka 5,maana Ukisema Uchukue Miaka 3, Utapata Hela Ndogo Sana. Alafu Nmb Tawi La "Kilombero" Tunaomba Huyo Afisa Wenu Mikopo Wa Kiume Huyo (jamaa)anaekaa Nyuma Ya Afisa "Dada Grace", Hasiusike Kabsa Kuwapigia Mahesabu Wafanyakazi Wa Kilombero Kwani Hajui Kabsa,ni Mzembe Anawakosesha W/kazi Na Kuwasababishia Kupata Hela Ndogo,

Tunaomba Mikopo Ya "Salaried Workers Loan" Mfanyakazi Akatwe 60% Ya Mshahara Wake Na Sio 40%kama Ilvyo Sasa, Kama Vp Mseme Mmeshindwa Ili Benki Ya Crdb Ichukue Nafasi Tunajua Mmetoa Rushwa Kampuni Ili Crdb Wasipate Kibali. Naomba Kuwasilisha
 

nauliza vp kuhusu manunuzi ya hisa hapo NMB na utaratibu mzima wa bei, interest ambazo mantra na ni katika mda gani mnafanya mahesabu yenu katika share izo
 
Shida yenu kubwa ni ATM mobile, wakati mwingine unatoa hela yako toka bank kwenda m pesa, unakuta kwenye account imeshatoka, na kwenye m pesa haionekani. kama basi tatizo ni Network, inakuaje muda mwingine Inaisha zaidi ya wiki bila tatizo kutatuliwa? na ukipiga cm muda mwingine haipokelewi na wahudumu? sasa kama una tatizo la haraka inakuaje kupata msaada kwenu? MM NI OTH MAN MIRAJI, WA ARUSHA.
 
NMB naipenda ni bank ninayo iaminin sana. But kuna wafanyakazi wake wengi wanaona kama tunaenda bank yao kwa sababau tunashida sana. Altutude zao mbaya sana .

Kuna wadada msasani br wapo kwenye balance, wanajibu hovyo hovyo watu. so sad na kuna wadada pia wa MOROGORO RD vidada vidogo vidogo vipo juu navyo balaa take it positively ili iwasaidie Junior member
 
Last edited by a moderator:
Mtandao wenu [coverage ya matawi]ni mzuri ila tu hamna huduma ya VIZA card,mngekuwa na hiyo hakuna benki ambayo ingewafikia hapa Tanzania
 
Niko masomoni mbali kwahiyo nashindw kupata hati zangu za mshahara,nauliza kama nlikopa nmb milioni 2 mwaka 2013 mwezi wa 7,na kuupata mwezi Wa 8 na mwezi huyo Wa nane makato yalianza, je makato ya mkpo huu yatakoma lini?
 
Hapo sio NMB anaefanya hivyo, ni moja ya vigezo na masharti yanayotolewa na bank kuu hivyo bank yoyote unapokwenda kuchukua mkopo lazima watoe 40% ya salary
 
Hongereni kwa kuwa wawazi kwan sisi ndo wateja wenu.

naomba kuwashauri kwanini msianzishe dilisha maalum kwa kuingia mkataba na watumishi wanaotaka kwenda kusoma na mkawa mnawalipia ada moja kwa moja tofauti na hii ya kukopa na kupeleka mwenyewe, yaani mboleshe mikopo ya elimu kwa watumishi

naomba kukomea hapo
 

Kununua Umeme kwa NMB mobile ni bure, kama umeshawahi kukatwa pesa yoyote kwa nunua umeme weka hapa bank statement tuone ..

hilo swala la kutopata msg za luku hata mimi huwa linanikera sana ila ukiwapigia simu zao wanakusaidia kuzipata
 
NMB badilisha kadi zenu ziwe za VISA ili kuongeza huduma pia kwa Tanga mjini ongezeni huduma za ATM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…