NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Master card je naweza nunua ebay au amazon kwa kutumia card zenu
 
Mnachelewesha uingizwaji wa hundi mfano utakuta taasisi imesambaza hundi kwa benki tofauti kwa lengo la kuwalipa watumishi, utakuta wale walio katika benki nyingine wanawahi kupata pesa lakini tulio na akaunti NMB pesa inachelewa mno kuingizwa wakati hundi zote zimepelekwa siku moja kwa wakati mmoja hilo litawakosesha wateja msipokua active hasa matawi ya mikoani na wilayani
 
Hivi nmb kwanini mnafanya kazi kizamani sana?au viongozi wa matawi yenu ni majipu yanahitaji kutumbuliwa?mtu anaeonana na wateja mara kwa mara lazima awe na afya nzuri, kwenye matawi yenu ya Posta kuna mfanyakazi wenu wa kike hayuko sawa, hembu jiangalieni, unahudumiwa na mtu hata kusema vizuri hawezi, kila wakati kama ana kitu kimemkaba mdomoni, acheni mambo yenu bana.
 



MUUNGWANA NI VITENDO
nyie NMB mnatesa wateja wenu kwa kuwasimamisha foleni masaa mengi bila hata msaada wa viti ikumbukwe kuwa mna wateja wengi kuliko benki zingine hivyo msululu wa wateja ni mkubwa katika matawi yenu ila cha ajabu hakuna maboresho ya kuwa na hata viti na matokeo yake huduma inamchefua mteja kwakutojali kwenu.
nashauri kuwe na viti vya kutosha kwa kuwa kuna chanagamoto ya kuwahudumia wateja wenu kwa wakati.
fikiria kwa mfano nimetoka zangu vijijini nimechoka nafika benki nasimama masaa karibia manne, nachukia sana kitu hicho mbadilike.

kama hamna viti mboreshehuduma tusiwe tunakaa muda mrefu na usiozidi saa moja.
 
hivi kuchukua mkopo wa kutop up ni baada ya miezi mingapi...
mie nimeenda wameniambia ni miezi tisa tu. ila hapo awali ilikuwa mwaka mmoja. sema nao wanabadilika badilika bora uwahi wasijepeleka miaka 2.
 
Kwakuwa kuboresha huduma na kuongeza kasi mmeshindwa, sasa basi tumechoka kusimama na simu tutaongea tukiwa ndani maana hatuwezi kuwekana masaa Matano tumesimama bila mawasiliano.

Au wekeni mabenchi twende mstari kwa kujivuta kama hospital
 
Naomba mnielekeze kuhusu hilo ongezeko la VAT la 18% kwa kuanzia tarehe 1/7/2016 kutokana na badiliko la sheria ya kodi kwa mfano halisi. Nitashukuru
 
Nataka nikope NMB muwe munakata marejesho tshs.185,000/= kwa mwezi nataka mda uwe miezi 60. Nitapata shilingi ngapi? Naomba hesabu yenu ili nilinganishe na bank nyingine. Nawasilisha.
 
Naona mnauliza tu bila majibu. Kwa nini msiende hukohuko mana hapa ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Hakuna wa kuwajibu wakuu angalieni namna nyingine
 
NMB MOBILE huduma ya kujiunga Nmb mobile inashindikana n mwenzi sasa nataka kujiunga na HUDUMA HII LAKINI NAAMBIWA HAKUNA MAWASILIANO NIMEENDA HADi nmb HOUSE BADO INASHindika
 
baazi ya seemu zene ya brachi zenu muko powa hila seemu zingine tunatumia tu kwa sababu zisizo zuilika hila amko vizuli sana kikweli
 
Kiukweli huduma zenu zinachosha sana afu watoa huduma wanajickia sana mkumbuke hii ni biashara na cku xote mteja ni mfalme na msipokuwa makini mtapoteza wateja lukuki!
 
NMB MOBILE huduma ya kujiunga Nmb mobile inashindikana n mwenzi sasa nataka kujiunga na HUDUMA HII LAKINI NAAMBIWA HAKUNA MAWASILIANO NIMEENDA HADi nmb HOUSE BADO INASHindika
Hiyo sahau ndugu
Mie nina miezi minne,sijaipata nikitaka pesa inabidi niteseke kidogo hadi wilayani kwenye ATM
Hii ni benki ya makanjanja
 
NMB Tanzania hii branch ya Kisarawe inanishangaza sana, kuna madirisha manne ya kuhudumia Ila kila siku ukifika inakera Ni dirisha moja tu likowazi mengine Ni imefungwa Kwa muda , temporarily closed.
Hii inakera.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…