Mkuu wameshaanza kutoa nenda ukakwajuke mkwanja...nmb wameanza kutoa mikopo kwa wafanyakazi wa serikali?
nyie NMB nyie sina hamu na nyie kabisa nlifungua account chap chap baada ya kuambiwa account ya mwanzo imefungiwa sasa namba yangu simu hamjaifuta toka mwezi wa saba mpaka sasa hivi haijafanyiwa chochote na yale mabarua mlionisumbua kuandika
Naomba kuuliza nilijiunga NMB mobile lkn line yangu ikapotea halafu nikarenew tena je hiyo nmb mobile itaendelea kufanya kazi?Ndugu wana JamiiForums,
Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.
Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.
Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:
1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG]; Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:
Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.
4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom