NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Kuna baadhi ya matawi yenu mfano Ngudu Kwimba kulikuwa na tabia mbaya, mf. Mtu akitaka kuchukua mkopo alikuwa anazungushwa sana ili atoe rushwa, na wakiona hujiongezi wanakwambia waziwazi. Sijui kama hiyo tabia wameacha au bado inaendelea.
 
Pokeeni simu za Wateja wenu , kuna mhamala nimefanya haujakamilika.Napiga customer care for almost 2 hrs there is no
 
Aisee noma sana
 
Aisee 800 parefu ningekua mzazi sijui ningekuelewaje?
 
Leo nimekoma kutumia nnb mobile, hela yangu na mateso napata Mimi.Mpaka sasa hamtaki kupokea simu yangu amnanisubirisha tu.Juzi mmenikomoa kwenye DART hivyo hivyo.
 
NMB jirekebisheni. Mlinikata laki 2 kwenye akaunti yangu kwa uzembe kwenye tawi la Wami Morogoro. Nilipowadai, mkasema niandike barua makao makuu. Kwani mliponikata, mlipata order toka makao makuu? Acheni hizo bhana.
 
NMB Mbarali,wanalazimisha watu wakachukue hela mtaani kwa wakala wao,huku wakiwa wameharibu ATM machine zao makusudi!

NMB acheni kufanya biashara kwa mazoea,halafu nyinyi wafanyakazi acheni ushamba wa kujiona mmesoma kuliko wateja wenu,kiufupi uwezo wenu ni mdogo ndomana mmeajiliwa,mngekua na akili mngefungua miradi yenu ili msaidie ndugu zenu vijijini.
 
Hapo nilishakutana na majibu mpk leo sitapasahau...
 
Hacha uongo nmb mbarali atm zao zipo vizuri sanaaaaa,,,,kama uongo njoo lugelele hapa
 
Punguzeni Riba kwenye mikopo ya watumishi na processing and insurance fee
 
Kweli kabisa mkuu, wafanyakazi wa NMB Bank [emoji542]. Wanazingua sana, inafikia kipindi unaogopa hata kuwa na izi mobile [emoji336] bank [emoji542]. Maana wanaweza Wakaamisha hata pesa awa
 
Leo jumatatu nawapigia hampokei tens, ngojea niwaibukie huko ofisini kwao baada ya shughuli zangu.Poor u NMB na nimejifunza , sirudii tena Huduma yenu ya nmb mobile.
 
Nimesikia hii habari lakini sijui ina faida ipi kwa mkulima, na inafanyaje kazi. Kwa ujumla napenda mwenye kujua kwa undani kuhusu eKilimo anifafanulie tafadhali.
Natanguliza shukrani.
 
Jaribuni kuwa na huduma nzuri kwa wateja sio mteja mnamzungusha mpka anaamua kuwahama kwenda benk nyingine
 
Hawa jamaa nimewavulia kofia, kuna jamaa kakopa 10m eti anatakiwa arudishe 17m! NMB mungu anawaona.
 
hata mimi nimekopa 8m na narudisha 13m..

hawa jamaa ni walafi vibaya mnoooo..

sina hamu nao... wanavigharama vya kijinga kijinga na unalipa mtejaaaa

Hawa jamaa nimewavulia kofia, kuna jamaa kakopa 10m eti anatakiwa arudishe 17m! NMB mungu anawaona.[/QUOTE
 
Huduma zenu kwenye junior account ni F, kama hiyo Huduma haipo bora muwe wakweli...
Nlijaza standing order mwaka jana, nmejaza tena mwaka huu muwe mnakata hela kwenye account yangu kila mwisho wa mwezi mnaweka kwenye junior account cha ajabu huduma sipati nikija bank bla bla mara nijaze tena fomu, mnakera
NMB Tanzania NMB Tanzania
 
naona humu maswali ni mengi kuliko majibu...account owner kimya
 
NMB hamna mfumo mzuri na salama wa kuchukua fedha kutoka kwenye mashine zenu za ATM, hii imepelekea kuwasababishia hasara ya kupoteza fedha baadhi ya wateja wenu mmoja kati yao nikiwa mimi mwenyewe nilie poteza fedha kiasi cha shilingi laki mbili kutokana na matatizo ya kiufundi mashine zenu
 
Ivi kwa nini? Katika NMB bank [emoji542] kusiwe na huduma ya kuweka fedha kupitia ATM [emoji763] mashine kuliko kupanga foreni ndani wakati wa kuweka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…