NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Vodacom ndio mfumo wao unachelewesha kumpatia mteja hela.Tigo hawacheleweshi maramoja muamala unasoma kama tigo wana tatizo ila kwenyehela ni zaidi ya haraka
 
Tatizo halipo NMB bali Mpesa, usijaribu kutuma pesa kupitia Mpesa ni wasumbufu sana, sio NMB mobile tu hata Sim banking kwa mpesa ni shida. Yaani hata ukinunua Luku kwa Mpesa ni usumbufu tu.

Hebu jaribu kutoa kupitia tigo pesa ni fasta kama haiwezekani muamala haufanyiki. Lakini Mpesa kama unalipia luku au king'amuzi wanakata pesa afu wanakaa kimya pumabavu Mpesa.
 
watakurudishia ila ndio hivyo tena ile charging hawatakurudishia. umekatwa wanachotaka na wanakurudishia salio lililokatwa. ndio ujinga walio nao. nilishawahi kusubiri hadi siku tatu ila wanarudisha na watakuletea msg kuwa muamala wako ulishindikana na wanakurudishia hela yako. sijui kama inakuwa automatic au kuna mtu anashughulikia hiyo mahsusi.
 
Mkuu unalipwa na tigo??
M Pesa wako vizuri tuu shida ni bank. Hamia CRDB.
 
Hyo namba ya customer care haipatikani wakuu nmepiga sana.. Nmetuma pesa kwenye mpesa haijafika
 
Namm yamenikuta.. Hyo namba haipatikani
 
Baadhi ya wafanyakazi wa NMB Tarime si waaminifu , unapokwenda kuchukua hela zaidi ya laki tano, usipo hesabia palepale, utajikuta unachukua hela pungufu.

Hii imenitokea wiki iliyopita nilichukua milioni mbili na nikawa nimepewa za noti ya tsh elfu mbili na zilikuwa zimefungwa kwa mipira/rubber band na zilichomolewa kutoka ndani ya droo. Nilipofika Nyumbani nilianza kuzigawa kulingana na matumizi yangu. Cha kushangaza mabunda ya katikati yalikuwa na pesa pungufu wkt Yale mawili ya pembeni yalikuwa na idadi zote za noti.

Hivyo, ninashauri kuwa ni vema wahudumu/ bank tellers wahesabu hela kwenye machine kabla ya kumpatia mteja wa NMB ili kuepuka tatizo hili. Tena uongozi wa NMB tarime uwasisitize watumishi wahakikishe wanakagua hela kwenye machine kabla ya kumlipa/ kumpatia mteja.
Mwaka Jana tatizo kama hili lilinipata Tena na nilirudi hadi benki na kumwambis MTU aliyenihudumia kuwa muamala aliokuwa amenifanyia hakutoa hela yote kwani naye alinipatia hela kwa imani kwamba zimekamilika lkn nilivyokuja kuhesabu,nilikutana zile hela ni pungufu.

Hivyo nimeamua kuweka wazi jambo hili LA kihuni linalofanywa na wafanyakazi wachache wahuni, wasiokuwa na maadili na wanaoipaka benki ya NMB tarime matope kwani watumishi wa aina hii wanajipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na pia wanasababisha sisi wateja kutofikia malengo yetu kwani pesa tunazozichukua benki hushindwa kukidhi matumizi lengwa/husika.
 
 
Toka nijiunge NMB 2009 mpaka leo,leo ndo nimeona nimepata huduma nzuri pale ILALA BOMA NMB.Kuna mfanyakazi aliyepewa ufanyakazi wa mwezi amenihudimia mpaka nikaridhika,nilitamani nihame bank ila huyo jamaa kanifanya nirudishe majeshi.​
 
Nyie nmb mungu anawaona,
mnajinasibu mteja ikitokea kafiwa na mkewe mnatoa rambirambi laki sita,mbona mimi mpaka leo kimya na taarifa zililetwa kupitia nmb tawi langu,mkuranga pwani,tena mrs nae alikua mteja wenu kibenki.
 
NMB: ATM card yangu ilianza kusumbua kufanya transaction, nikatengenezewa kadi nyingine. Cha ajabu sasa zimepita wiki 3 sasa card haifanyi lolote nikiitumia kwenye ATM machine.

Nimefuatilia kwa muda wote huo ktk tawi langu na kuambiwa bado card haijawa activated. Duh nimechoka sasa kwa sababu kila nikitaka huduma ya kutoa pesa lazima niingie ndani benki. Yupo rafiki yangu nae ana tatizo kama langu tawi hili hili.

Naomba kusaidiwa, tatizo ni nini hasa? Mteja, Tawi la Mafinga.
 
atm card zenu ni kama vitambulisho vya wanafunzi wa sekondari za kata,yani mmenipa visa card lakini haijapita hata miezi miwili lamination ishaanza kubanduka na naitunza kamamboni yangu ya jicho....mbaya ni kwamba ikiharibika mtanichaji 15,000/=..acheni hizo
 
kero yangu kubwa na maoni yangu ni transaction charge ya kuhamisha pesa kwa kutumia NMB mobile ni kubwa mno iwe inatoka nmb kwenda kwenye mitandao mfano Tigo pesa,yaani ukihamisha hata elfu 10 mnakata 2500, huu ni wizi, jaribuni kureview hizo charge zenu, mm nimesimama kabisa kutumia hiyo nmb mobile kutokana na huo uhuni, CRDB wenzenu tozo zao zipo chini sana hadi unafurahia na pia i think wenzenu wamekua wa kwanza kuintroduce hii huduma kwa wateja, na kingine tunaomba muongeze kiwango cha kuhamisha pesa kutoka account 1 ya NMB kwenda nyingine ya NMB iwe ml 5 hii inasaidia kupunguza mafoleni kwenye mabranch yenu na pia its more secure! wenzenu CRDB wanafanya hivyo!!

mimi nina account crdb na nmb lakini natumia sana CRDB sim banking sana kutokana na huduma zao nzuri na wamestandardize viwango vyao vya tozo za kutuma!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…