NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Nimepewa cheque na GEPF ambapo inatakiwa nilipwe hela yangu nikaenda NMB Kenyatta road Mwanza nikaambiwa lazima niwe na account ili malipo yafanyike kwa kuwa Nina account CRDB nikawaeleza basi wakanambia nipeleke cheque CRDB itafanyiwa kazi.

nkapeleka cheque tarehe 6/9/2017 nikaambiwa nisubir had alhamis ya tarehe8/9/2017 hela itakuw tayar lakin mpaka sasa hela haijaingizwa na Nimeishiwa pesa kabisa naomba msaada wenu
 
Naomba unielekeze jinsi ya kufungua account ambayo nitakuwa naweka pesa kwa mtindo wa Standard order unipe charge zake na interest kwa mwaka maana mshahara wangu unapitia kwenu
 
Jeuri ndo ilokuponza kwa nini hukufungua akaunti ya chap chap... gharama yake 5500 kila kitu unapewa apo apo, na cheque ya bank ambayo ndiyo unaakaunti haichukui ata nusu saa kuingia. Lkn kama ni bank tofauti tayar hapo inasimama clearing house katkat sasa you can imagine itachukua muda gani saana huaga 72hrs lkn ikibounce ndo shughuli kama hizi. Haieleweki ni GEPF, ni NMB, ni clearing house, ni CRDB au ni wewe mwenyewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa jibu lako, nifungue acc nyingine wakati sina pesa za kuweka huko itakuwa na maana gan na hela ninayotakiwa kulipwa ni ndogo tu huoni kama itaishia kwenye shughuli hzo za kufungua acc. pia Mimi sina uelewa na shughuli za kibenki
 
Naomba namba zenu za huduma kwa mteja
 
Jamani muongeze wafanyakazi kwenye matawi yenu, alafu hao waliopo wasifanye kazi kwa mazoea na kwa kujiskia tu.

Nadhani hilo ndilo jambo mhimu kwangu
 
Tatizo linabaki kwa wafanyakazi wa serikali, tunakaribia benki 50 so ukiona wankuzingua mara paaaap unahimia kwingine
 
NMB MOBILE UKITAKA KU TRANSFER INAANDIKA -FAILED TO PURCHASE TOKEN- KWAN MIM NANUNUA LUKU?

NA RAFIKI YANG WA MANYARA KANIPIGIA NLIJUA MI MM PEKEE, WE HAVE FACED THE SAME PROBLEM!!!

MASTERCARD APLICATION FEE IMEKUWA 15,000??

NMB MOBILE APP HAIFANY KAZ MWAKA SASA, MNANINI??
 
Nmb anziasheni salary advance ,kwa kuwa na mfumo maalum utakao wasaidia watumishi na benki itapata kiasi Fulani cha faida
 
Nyie Nmb faken sana kama kwenye huduma ya mobile kuna tatizo kwa nini msituhabarishe sisi watumiaji badala yake mnakaa kimya kila MTU anaponfanya transaction ikikaribia mwisho inafeli na mnakata amount kama sio wizi ninini?acheni ujanjaujanja bana huo ni utapeli
 
Hivi akaunti ya ChapChap inaweza kufanywa kuwa ya kupokelea mshahara au mpaka ifunguliwe ya Personal A/c?
 
Hivi akaunti ya ChapChap inaweza kufanywa kuwa ya kupokelea mshahara au mpaka ifunguliwe ya Personal A/c?
Unapokelea tu ndg ilimradi uwe chini ya 5mil. Kama upo dar mcheki kwa namba 0717667790 anakufungulia chap popote.
 
Unapokelea tu ndg ilimradi uwe chini ya 5mil. Kama upo dar mcheki kwa namba 0717667790 anakufungulia chap popote.
kwa hiyo unaruhusiwa ila muamala usizidi 5mill sio? ina maana akiba inaweza kuwa ya kiwango chochote mfano 10mill na kuendelea?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…