NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Naomba kujulishwa taratibu za kampuni inavyoweza kufungua A/C katika NMB BANK PLC. Pia nitaomba mnitajie nyaraka zinazohitajika kuwasilishwa wakati wa ufunguzi wa akaunti.
 
Habari zenu wakuu.

Natumaini wote mko salama hapa. Leo nimekuja na malalamiko juu ya wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Mafinga mjini.

Wafanyakazi wa benki hii wanadharau sana wateja, hasa wale waliopo katika dawati la customer care.

Jana tarehe 22/1/2020 nimeenda kuchukua ATM card yangu, nikamkuta mama mmoja yupo pale, nikamwambia shida yangu. Akaniambia nisubiri. Basi nilisimama saa tatu nikisubiri achezee kompyuta yake ili anipatie kadi yangu ambayo ilikuwa kando tu na alipokuwa.

Nilisimama saa hizo na kadi sikuipata. Mwishowe nikaondoka kwa hasira.

Jamani, mpo hapo kwa ajiri yetu. Sisi ndio tunaowafanya mulipwe mishahara hapo. Kama mimi ni mteja mkubwa wa benki yenu. Basi tupeni thamani yetu kama wateja.

Msitunyanyase.

Nawasilisha.

Naitwa Six Man.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ukutendewa haki je ulimfata meneja wake umueleze
 
Natumia app ya nmb mkononi. Inaniapa notification kuwa USE ORIGINAL SIM CARD.
sijui hili ni tatizo langu au ni kwa woote.
Simu kadi nayotumia ndo niliosajilia nmb mobile na data nimewasha natumia ya sim card iliyokuwepo kwenye usajili wa nmb mobile.
Kulikoni wajuvi wa mambo
 
Uninstal kisha Install Upya App Yako
Sent using Jamii Forums mobile app
 
hivi ule mkopo wa jenga nyumba ya ndoto ya ndoto yako mnaotoa kwa watumishi na unalipwa kwa miaka 20, kama mtu hataki nyumba ya kukaa anataka kujenga sehemu ya kufanyia biashara kwa makubaliano hayohayo inawezekana?
 
Nimesahau namba yangu Siri ya nmb mobile nafanyaje jamani.
 
Nashauri card za ATM ziwe na no za simu za mteja
Nimepoteza card yangu ya ATM ya Nmb...naamini kama kadi zingekuwa zinaandikwa no zete za simu ingekuwa rahisi kuzipata pindi zinapopotea...kwani kwa MTU anaeokota akiona no ya simu kwenye kadi ni rahisi kupiga simu kwa mlengwa kuliko kuichukua na kuipeleka ofisi za Nmb


Sent using Jamii Forums mobile app
 



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…