NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Habari, mm naomba muongozo WA kufungua akaunt nmb ,nipo buguruni rozan dar ,lkn Kitambulisho cha uraiya bado kupata.naomba kama inawezekana nijibiwe mp

Sent using Jamii Forums mobile app
W
 
Baadhi ya BENKI zimetangaza KUPUNGUZA kiwango Cha RIBA hadi 14%.

Ni lini NMB mtapunguza RIBA?
 
ADVANCED SALARY.

Tunawashukuru wadau wa NMB kwa kutuanzishia hii huduma ya Advanced Salary, ni msaada mkubwa kwa wateja wenu.

Huku mtaani ukimkopa mtu riba ni kubwa sana zinafika hadi asilimia 30. Yaani umkopa mangi laki moja unalipa laki na thelasini, mwisho wa Mwezi. Wakati nyie ni asilimia sita tu.
 
HABARI.....?..
wanahitajika madalali tufanye biashara ya magodoro moja kwa moja kutoka kiwandani ,,na mchakato wao mkubwa utakuwa ni kuleta wateja wa jumla na reja reja,,, na watapata malipo kama kawaida punde wanapoleta mteja...
kwa mawasiliano zaidi 0692449416
 
Hivi kama slip yangu ya Benki ya mwaka jana imefutika maandishi, nikienda Benki kuomba kopi ya malipo niliyoyafanyakwenye slip hiyo natakiwa kulipia?
 
Ni sababu gani inafanya mteja asafiri hadi mkoa alikofungulia akaunti?

System ya bank inashindwa nini kufanya mawasiliano na tawi ambalo mteja amefungulia akaunti halafu wanarenew kadi hapohapo kwenye tawi alipo mteja?

Nmb hawaoni huu usumbufu kwa mteja?

Kama hayo yote hayawezekani basi mteja aletewe kadi bure kwasababu imeisha muda, haijapotea.
 
Card yangu ilimezwa ijumaa asubuhi nikiwa katia harakati za kutoa pesa nikalipe ada ya mtoto pale Nmb Ubungo

wale wahudu wawili pale mhuduma kwa mteja walijitahidi kunisaidia kuifutilia card yangu kule ndani bila mafanikio huwezi amnini sikupewa ile card mpaka nimeondoka pale saa tisa jioni bila mafanikio.

Nawauliza shida ni nini?wanajibu Kule atm sijui kwa ndani haruhusiwi kuingia mtu mmoja...hivyo mmoja wapo aliyepaswa kuingia yupo bize sana huwezi kusaidiwa.

Nilikasirika nikamwambia yule mama aliyenijibu kuwa nwenzangu yupo bize nyie wabaya sana nikaondoka bila kuhudumiwa
 
Ni usumbufu mkubwa sana! Mwisho wasipokuwa makini wateja wataikimbia hii bank!
Halafu kwenye kutumia NMB mobile ukibofya namba *150*66# ili kuhamisha pesa kwa njia ya simu hupati huduma mara moja, ni hadi upige hiyo namba mbili au tatu ndio inakubali.
Sasa ile mara au ya pili unajibiwa huduma haipatikani lakini gharama unakuwa umekatwa kama vile umepata huduma!
Hapo naona kama tunaibiwa.
Huduma haijapatikani, kwanini nikatwe gharama? Huwa nahisi wameseti makusudi ili wapate pesa ya bure!
 
Naomba kujua utaratibu wa kufungua child account
 
Changamoto kubwa tembeleeni Vituo vya NMB vilivyo karibu nanyi.
 
Kadi inapoisha muda wake, mteja apewe/atengenezewe kadi kwenye tawi lolote sehemu alipo kwa wakati huo.
Sio kuelekeza mteja aende mkoa alikofungulia akaunti au kudai alipie pesa kadi iletwe, huo ni usumbufu mkubwa kwa mteja.
Ni kutothamini wateja! Kadi imeisha muda haijapotea, kwanini mnidai tena pesa kupata kadi mpya?
 
NBC ndivyo wanavyofanya, kadi ikiisha tawi lolote unapewa kadi mpya, NMB Mnakwama wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…