NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Kumbe NMB hamtoi mkopo kwa dhamana ya Hati ya Nyumba Kama hauna Leseni ya Biashara?!

Hapo mie nashangaa kwani mtu anavyoomba mkopo wa kwa kutumia hati ya Nyumba 'collatelo' hivyo haruhusiwi kupatiwa mpaka awe na Leseni ya business, sasa kwani mini nilikuwa nataka mkopo wa biashara au wa ujenzi?

Kama ungekuwa ni wa biashara si ningeomba mkopo wa biashara! Embu rekebisheni hilo lisitukere wateja!
 
hivi kuhusu nmb mobile kama nikitaka kuibadili namba hio je ninahaja yakuenda bank au kuna menyu naweza baridi?


Maana namba nliosajilia before imefungiwa nasiihitaji tena.
 
Heko kwa kazi nzuri. Ila Nina lalamiko ninakatwa fedha yapata miezi mitatu hiu wa nne, nakura fedha zimekatwa, nikajaribu kutega, nikaacha kiwango kidogo ila baadae nikakuta Kuna fedha ndogo Sana, sasa nashindwa elewa tatizo nini?
 
Tu nashukuru kwa Huduma nzuri. Tunaomba Ushirika iliyopo Tukuyu Rungwe iwekewe ATM sababu watumiaji ni wengi sana ila hakuna Huduma hadi Tukuyu mjini
 
Boresheni mfumo wa mikopo kwa watumish wa umma. Mnatufanya Kama na sie Kama wababaishaji

Kweli kabisa mwalimu. Kuna branch ya NMB niliingia nikaishia kuwaona wa ajabu tu. Huduma zinasuasua na kasha kash kama zote.

Mbaya zaidi ni pale ukiomba mkopo. Watakuchelewesha weee mpaka utapata hasira na kutaka kuhama benki
 
Nmb toeni maelezo ya ukweli kwa wakulima tangazo lenu mnatoa mikopo kwa wakulima. Mkulima akienda kutaka mkopo wa kilimo mnaona jambo geni kwenu
 
Kero yangu kubwa ni pale ninapoomba mkopo nimetiza vigezo kuanzia kwa mwajiri mpaka benki, mwishoni mkopo utoke mnasema umekosea sahihi Ilhali mimi tangu nimefungua akaunti ni zaidi ya miaka 20, nitakumbuka kweli nilisaini vp, mnaboa sana na isitoshe mshahara unapitia kwenu!
 
NMB Tanzania mbona hamjibu hata maswali?

Je nikihitaji hiyo NMB MasterCard ni lazima niende kwenye tawi nililofungulia account?

USHAURI:Fanyeni mpango ili wastaafu wanaopata monthly payment kupitia bank yenu wawe wanapata SMS notification pesa ikiingia kama kipindi walipokuwa wanataarifiwa mshahara ukiingia walipokuwa kazini.

Wanaambiwa kwa sasa huo mfumo haupo.
 
Wataalamu naombeni msaada hapa NMB !!
Nina acc ya NMB chapchap niliifungua kwa lengo la kufanya saving na kwa kuwa huwa haina makato, sasa imefika mahala kiasi cha pesa iliyoko humo kimeshazidi mil 5 ambayo huwa ni ukomo wa hiyo acc je nifanyeje?

Na kuitoa nitaruhusiwa ili acc iendelee kuwa chapchap au itanilazimu niifanye personal acc?

Au nifanye transfer kuipunguza pesa iliyozidi?? Maana lengo langu ni kufanya saving na je kuna namna nyingine ya kutimiza hilo lengo langu?? Msaada TAFADHALI
 
Ninakibiashara chagu, nataka kujipanua kibiashara, nahitaji Mkopo nafata taratibu gani kuweza kupata mkopo, tawi Jirani Na biashara yangu ni NMB Korogwe. Vyuma vimekaza tuvilegeze kwa kujiboreshea investment ndogo kuwa kubwa.
 
Big up NMB BNAK Plc
 
Miezi zaidi ya sita (6) hamjibu comment za wateja, vipi mmekutwa na nini?
 
NMB boresheni huduma zenu za mobilebank , pia kila mara network iko down sasa kweli kwa mwendo huu mtaweza kuhudumia wateja amabo wanaweza kuongezeka hadi kufikia 50million?

tafadhali wekeni mitambo ya kisasa inayo endana na wakati na mahitaji ya sasa, mambo ya kuambiwa network iko chini ni ushamba.

mnakwasa mipango yetu ya biashara kwa kutokupata huduma kwa wakati, mnatutia hasara, mtu unataka kutoa fedha unakuta mtandao uko down, hakuna network dah.!
 
App yenu ya nmb mkononi Ina shida , huwezi kuitumia bila simcard , app inatakiwa ikusaudie kwenye mazingira ya internet , labda umesafiri nje ya nchi au nje ya network yako then ukipata connection yoyote unafanya muamala. Hii app yenu kila uki log in unataka sms verification kwa laini uliyosajilia , iki confirm ndo unaweza kufanya muamala , maana yake ni kuwa ukiwa nje ya network ya simcard uliyosajilia huwezi kupata huduma za nmb mkononi .

Wenzenu crdb app yao simcard inatumika wakati wa ku register tu , ukishamaliza kujisajili app inakuwa huru kutumia connection yoyote iliyopo bil hata kujali Kama simcard husika ipo hewani, popote utakwapokwenda ukipata net hata ya wifi , unafanya miamala.

Kwa maana halisi app ya nmb mkononi huwezi kutumia ukiwa nje ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…