NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Safi inaboa sana hii
 
NMB mtandao wenu kila siku uko down tatizo ni nini? malipo yanachelewa sana unapo fanya kutoka sehemu nyigine kwenda NMB, ukiuliza unaambiwa hakuna mtandao!!! inakataisha tamaa, shughuli nyingi za malipo zinachelewa kutokana na tatizo hilo, kweli kwa mwendo huu wa network ya nmb kuwa chini karibu kila siku kweli tutaifisha nchi yetu katika uchumi wa kati?!
jamani hebu badilikeni rekebisheni matatizo hayo
 
NMB Magomeni huduma mbovu mno. Nilizungushwa zaidi ya wiki kufungua akaunti nikaamua kwenda NMB Ilala ikanichukua chini ya lisaa kupata akaunti. NMB Magomeni wachunguzwe na kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu kuanzia boss hadi yule wa chini kabisa.
Duuh . . . yaani NMB magomeni mlivyo njiani hapo bado mnafanya ujinga hivyo
 
Pumzika baba askofu
 
Hivi inakuaje mnaweka fees kwenye kufanya replacement ya kadi..
Kadi haijapotea
Haijaaharibika ila mmeamua kufanya mabadiliko wenyewe kwa lazima tena alafu mnatucharge ..kiaje !?
Na kwenye ATM mmetupiga pin aisee!
 
Mi siwaamini kwa kila Kitu kuanzia Huduma zenu na mpk Wafanyakazi, Baadhi ya wafanyakazi wenu wana Dharau sana,
Acheni kutudharau wateja sisi ndo Mabosi wenu.
 
Msisina JANA NILIWAFATA WANIPE MKOPO WA 6M, WANAULIZA NINA LESENI,TIN,OFISI,TRA CLEARNCE FORM
nikajibu hivyo vyote Sina Ila
Nina dhamana isiyohamishika na wadhamini wapo na Nina uwezo wa kurejesha hiyo pesa.WAKASEMA SIWEZ KUKOPESHWA NIKASEMA ok NIKASEPA.
 
Mm hivyo vyote ninavyo lkñ huu mwezi Wa pili bila bila
 
Nahitaji mkopo wa million 3, vip nahitajika vitu gani na gani, Mali isiyohamishika kiwanja.
 
hivi kuhusu nmb mobile kama nikitaka kuibadili namba hio je ninahaja yakuenda bank au kuna menyu naweza baridi?


Maana namba nliosajilia before imefungiwa nasiihitaji tena.
Unaweza kubadili mwenyewe katika ATM. Chagua NMB Mkononi kisha fuata maelekezo.
 
Mbona cjawai kuona hao NMB Bank Plc wakijibu humu [emoji53][emoji53]
 
Kinachoniuzi NMB hakuna manu ya kununua muda wa maongezi moja kwa moja toka kwa akaunti ya benki kama ilivyo kwa crdb. Badilikeni sio lazima mtu aweke mpesa,tigopesa nk ndo anunue muda wa maongezi.
 
Kinachoniuzi NMB hakuna manu ya kununua muda wa maongezi moja kwa moja toka kwa akaunti ya benki kama ilivyo kwa crdb. Badilikeni sio lazima mtu aweke mpesa,tigopesa nk ndo anunue muda wa maongezi.
Piga *150*66# then fungua kwa pin yako then nenda no 3 pay bill, the no 1buy airtime, then hapo utachagua mtandao wako. Simple.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…