NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Nataka mkopo.. na je mna Contract financing ?
 
Ahsanteni sana kwanza kwa huduma nzuri mnazizitoa kwa wateja na jamii kwa ujumla.

Ni jambo la kuwapongeza pia kwa juhudi na uendelezaji wa technology katika benki yenu.

Ila nina machache tuu ya kuwapa ushauri kama maoni yangu binafsi mimi kama mteja wenu mkubwa wa muda mrefu sana tangu mwaka 1999.

1. Wateja wapya wa mikopo mikubwa wamekuwa wenu wengi tena idara ya mikopo mikubwa waliopo head quater dsm wamekuwa na tamaa sana ya rushwa kutoka kwa wateja kwa kuwashinikiza wale wafanyakazi wenzao wa matawini watengeneze mazingira ya kuweza kupata hongo pindi mikopo yao inapoletwa HO kwa ajili wa kupata idhini.

2. Wamekuwa na tabia ya kufunga safari kutoka dsm kuja mikoani ili kutengeneza mazingira ya rushwa kwa mteja husika, bila ya aibu wanapokuwa wamesafiri na kuja huku kukagua biashara na dhamana wamekuwa na tabia za ajabu sana za kuagiza vitu kama Michele,samaki, mafuta ya kupikia,kuku n.k na hata kujibaraguza kipindi cha kulipa bili kana kwamba walipotoka huko hawajulipwa pesa za kujikimu.

3. Wengine bila hata ya aibu wamekuwa na tabia ya kupenda kulala kwenye hotel za kifahari na kutengeneza mazingira ya sisi wateja kuwalipia na kana kwamba usiopowakarimu kama wapendavyo mkopo wako utakuwa kwenye mazingira magumu sana kufanikiwa.

4. Na pindi mkopo unapotoka tuu simu huwa ni nyingi sana mteja hupigiwa au hutembelewa tena ili kuweza kupata rushwa kwa kazi ambayo analipwa nayo mshahara.huu sio uungwana kabisa.

5. Kwa ushahidi kamili nimetuma majina ya wafanyakazi hao kwa mkurugenzi mkuu barua ya siri kwa njia ya ems kufafanua ufedhuli wao.

Mimi ni Mteja wenu.
Nmb Bank
Katika matawi ya kenyata mwanza na kaitaba Bukoba
Simu namba 06133879074
 
nyie NMB nyie sina hamu na nyie kabisa nlifungua account chap chap baada ya kuambiwa account ya mwanzo imefungiwa sasa namba yangu simu hamjaifuta toka mwezi wa saba mpaka sasa hivi haijafanyiwa chochote na yale mabarua mlionisumbua kuandika
Aisee
 
Matajiri.

Mmeshaanza kutoa mikopo kwa wafanyakazi au bado izo system zinazingua.
 
kwa kuwa NMB ndio Benki ya watumishi wa umma hivyo basi haina budi kuwa saidia watumishi wa umma kwa kuwapa mikopo maalum ya kukopa Magari au pikipiki (vyombo vya moto) ambavyo vitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

NMB mnaweza kuingia mkataba na Makampuni yanayo uza magari/vyombo vya moto maalum kwa watumishi kama vile Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania linavyo fanya kwa wabunge.au njia nyingine iliyo bora, lengo ni kuwakwamua kiuchumi.
 
Branch yenu Bukoba mjini Customer Service wamekaa tu. Mteja baadala asaidiwe wao ni kutaja tu achukue form gani. Je kama mteja ni mara yake ya kwanza anaingia benki au hajui kusoma
 
Yule wakala wenu mwizi wa Lugarawa mmeshindwa kumwajibisha kwa kumfutia uwakala? NMB mnafeli wapi?
 
Duh.. huogopi kuchawiwa mkuu. Maana wengine ni walozi sana na wanakalia hizo nafasi kwa ulozi.

Pole sana.
 


Hivi mnaona malalamiko ya wananchi au mmekaa kimya kwakuwa tumegundua wizi wenu

Someni hapa mtoe majibu vinginevyo tunaanza kuwahama

 
Hii bank nataka kuhama soon nimeenda kwa shida moja leo siku ya tatu nazungushwa tu.
 
Nmb Leo nimetoa pesa kupitia pesa fasta tokea saa7 mchana mpaka Sasa hivi hawajutuma namba ya Siri ya kutolea fedha.
 
NMB Tawi la Ubungo kitengo Cha Huduma kwa mteja mkiangalie aisee wasumbufu Sana alafu hawamuelekezi Mteja
 
Nikitaka niweze kutoa zaidi ya 800k katika ATM, nifanyeje?
 
Hivi hamna fixed account za sisi wenye viwango vidogo vya pesa kama 50k ...
 

.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…