NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Walinzi wao wanakera jamani, ole wako akuone unasoma msg kwenye simu utajuta kuzaliwa, MBNA mabenki mengine hawako hivyo.
 
NMB hii siyo sawa. Eti ili nipate faida kwenye akaunti yangu ya savings mpaka ni-maintain kiasi cha milioni 5 kwa mwaka.

Are you real serious? Ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kubakiza milioni 5 kwenye akaunti kwa mwaka? Kama nabakiza milioni kila mwezi imo mpaka mwisho wa mwaka ninyi mkiikopesha mnapata 180,000 kama si 240,000 kwa mwaka.

Zaidi ya hapo kila mwezi mnatukata 1500 na kila nikichukua pesa kwenye ATM mnakata 800 na 3000 kama nachukua kwa kaunta. Hii siyo halali kabisa mnatuibia.

Badilikeni vinginevyo nitahama au nitakuwa nakomba pesa zote za mshahara zikiingia na kuhamishia benki nyingine.
 
Nimelusha pesa kutoka benki kuja mpesa toka jana hamana kituuu duuu sijuii kwanini yaani hudumaaa
 
Duuu hapo nmb bank, umechemsha,mimi nilirusha hela toka nmb bank kwenda mpesa toka june mpaka leo sijapata majibu,nimefatilia mpaka leo,kila siku naahidiwa kesho, mpaka sasa
 
1.Foleni kila uchao.
2.ATM nako foleni.
3.Vyumba 5, Ila waliomo vyumbani ni wawili.
"Foleni kama.......
"
R.O.M.A"2012/3
 
Punguzeni gharama zenu za uendeshaji wa account zetu maana hadi najuta kwa nini nilisomea ualimu.

Hasa gharama za kumuona teller na nmb mobile ni shida sana.
Tunaumizwa sana wenzenu mtuonee huruma
 
Mnaboa sana pale mnapochelewesha kuniwekea bum langu kwa wakati, na nmb mobile kwa mtandao wa voda kwann haifanyi kazi bila airtime kama mitandao mingine?
 
Mafoleeeeni. Ila afazali mlivyonibadilishia ATM kuwa master card sasa hivi natoa pesa benki yeyote. Na nikitaka kuweka natumia tigo pesa tu vinginevyo ningeshaifunga na account yenyewe
 
Mimi ninahoja binafsi kama ifuatavyo!

Pamekuwa na usumbufu mkubwa kwenye mashine za ATM has a kukosa pesa kwa nyakati za weekend, kipindi ambacho wateja ndo wanahitaji huduma hii kwa wingi, inakuwaje pawepo na matatizo haya sugu huku mmeandika huduma ni kwa masaa24 matawi yote?
 
Tumefungua account nmb tawi la igunga toka mwezi wa tano 2015 (ajira mpya waalimu) mpaka leo wameshindwa kutupa kadi kwa kisingizio mashine mbovu! That is shame
 
NMB juzi mlifungua makao makuu mapya katika jengo la Nyumba Ya Sanaa . Ni vizuri kwa branding ni mahala au sehemu strategical kabisa kwa branding.

lakini juu ya hayo wasi wasi wangu ni gharama za kukodi jengo hilo lote . jee risk mangers na budget planner wenu kweli wamzingatia cost ya kukodo jengo lote ?
jee hapa faida ya bank yote inaenda kwenye kodi ?

hili jengo nathani lina gorofa 5 na kwa wastani kila floor ni wastan wa sqmts 1200 ambapo kodi ya kawaida ya CBD ni $ 23sqmt so 23x1200x5 =138,000 x 12 =1,656,000

kwa miaka mitano =$ 8,280,000.
sasa kibiashara hizi pesa ni nyingi mno na ufujaji hizi hapa Mjini unapata Kiwanja kwa bei ya chini ya $2-3m na mnaweza kujenga jengo la kwenu pekee kwa anothe $ 2-3 m hivyo na chengi inabaki.

uamuzi wenu sio biashara labda kama hilo jengo mume kodi $ 5/sqmt !!!!!
 
Natumai mnaendelea na kazi vizuri. Nina dukuduku langu kuhusu utoaji wa mikopo kwa watumishi kama mimi, kwani nimeomba mkopo katika bank yako na kukamilisha taratibu zote na kuwasilisha fomu kwa Afisa Mikopo tangu 23/09/2015 hadi sasa sijapata.

Ni ajabu kwamba inachukua muda mrefu kiasi hicho hadi kuondoa na kupoteza mana nzima ya kuomba mkopo huo kwani kusudio lake inaelekea nimepoteza.

Kama mtanijibu na kuhitaji details nitawapa, lakini inakera kwani mkumbuke mna washindani wengi na sisi wateja tunaotaka muendelee kutuhudumia ni lazima mtutendee haki na kwa wakati!
Kazi njema..
 
Back
Top Bottom