NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB Tanzania Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

NMB mobile ni kero kubwa kwa wateja! Programme ya huduma hii imeandaliwa kuibia wateja! Kwa nini namba ya siri inaombwa kabla ya process za kutaka huduma fulani hazijaanza badala ya mwisho wa process kwa kuwa hata kama hujakamilisha simu inakata pesa zake na benki pia inakata!!

Tafadhali rekebisheni hili!
 
Maafisa mikopo wao wanapenda rushwa hao. Kama ngudu mwanza pale ukimaliza kujaza fomu afisa mikopo anakwambia subir Kama wk mbili au mwez au unaweza usipate kbs maana kukupa mkopo ni hiyar yao.

Ukimpa 30 anasema hapo yake 20, afsa utumishi 10 hivyo meneja bado. Yani bila kutoa elfu 40 au 50 hupat mkopo. Mtu unakuta unashida ya maana unamtafuta mtumishi mwingine akukope 50 ya kuhongea ukishapata mkopo umrudishie.

Mkopo unakopwa kwa riba kubwa ila unanyanyaswa Kama wanakupa msaada, ngoja benk ya walimu ianze ndio mtajua kujiendesha kibiashara
 
Meneja wa NMB TAWI LA MUHIMBILI CHUONI INABIDI ACHUNGUZWE NIDHAMU YAKE NA IKIBIDI ACHUKULIWE HATUA KALI,,,,

Haiwezekani sisi benki yao imetuibia pesa zetu tunafuatilia analeta lugha za ajabu na kejeli zisizo kuwa za msingi,,, ilitubidi tuanze kuzifuatilia makao makuu,wenyewe NAOMBA MAMLAKA WAMWAJIBISHE
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.


Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Hongereni Kwa kuwa na mawazo mapana endelevu kwa kusikiliza malalamiko ya wateja.

Hata hivyo bado mnahitaji kujituma katika kumlinda mteja na mali yake pindi anapo fika benki. Hali ya usalama wa mali zetu wateja siku hizi umepungua hususani siku za tarehe za mwisho wa mwezi kuanzia tarehe 27 hadi 30 kuna wizi wa simu na baiskeli na watoa huduma wenu ndio wanachangia.

Mtu unapanga mstari kwenda kulipia ada watoto unatumia hadi masaa mawili kupata huduma hiyo. Unatoka nje unakuta simu yako tayari umesha ibiwa au baiskeli yako imesha ibiwa na wafanyakazi wenu hawana msaada hata wa kusikiliza malalamiko na kuyafanyia kazi ikiwemo zile sehemu tunazopaki baiskeli si salama wezi wanachukua kama zao.

Jamani sisi wanyonge tubaki na nini au wenye magari tu ndio wanaumuhimu. Fatilieni NMB Kilombero branch mkoa wa Morogoro yani ni shida watu wanalia kuibiwa baiskeli kila kukicha.
 
hoja yangu ni kwamba sisi was kanda ya kaskazini hususani wilaya za babati Karatu ATM ziko chache mfana halmashauri ya babati ATM iko mjini tu na Karatu pia iko moja pale mjini tu sasa inatuwia vigumu MTU kusafiri mwendo mrefu mngeweka ATM kwenye raasisi kubwa kwa mfano pale babati mngeweka DAREDA ili watu was bashnet na vjiji vya karibu vipate huduma kwa karibu na Karatu mngeweka endabash kidogo inakuwa na manufaa kwa vijij vya karibu halafu pale MTO wa mbu hakuna ATM makuyuni inahitaji ATM ebu tazame maeneo yenye uhitaji mkubwa kwa sababu karibu aslimia 70 za wafanyakazi was serikali wanatumia benk yenu asanteni kwa huduma
 
NMB tawi la tegeta kuna tatizo kwenye uongozi hasa meneja tawi.

Nmeongea na staff wa pale nmegundua tatzo juu ya meneja,mimi ni mteja mzoefu pale
 
Hivi nyie NMB baada ya kujaza fomu ya mkopo na kuikusanya natakiwa kusubiri kwa muda gani ili kuweza kuupata mkopo huo
 
kwakweli Nmb mnakera,Mimi tangu nifungua account mwaka Jana 2015 November hadi Leo eti bado kadi hazijatoka,hivi sisi wateja tuwaonaje????
 
Kwa nini kila mwisho wa mwezi kuna foleni kubwa kwenye matawi ya NMB ikiwa ni pamoja na kwenye ATM? kwa nini tatizo hili liwe NMB pekee? najua majibu yanaweza kuwa rahisi tu kwamba ni benki yenye wateja wengi, lakini si kweli pia kwamba benki yenye wateja wengi ndiyo inayopaswa pia kuwa na huduma bora zaidi? NMB nayo ibadilike jamani.
 
Ni muda gan ukpta bla ku2mia a/c unafungiwa?yan kuweka/kutoa!!
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu mliyoweka hapa juu ya huduma mnazo pata kwenye matawi yetu nchini kote, NMB inafanyia uchunguzi maoni na malalamiko yenu na tuna wahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki dhidi ya wafanyakazi waliotajwa na wengine wenye tabia kama hizo.

Ndugu wana jukwaa, NMB inajipambanua kwa kusimamia maadili moja wapo ikiwa ni uaminifu kwa wafanyakazi wake.
NMB pia inapenda kuwa hakikishia wateja na jamii kwa ujumla kwamba itaendelea kusimamia sera zote za benki ikiwa ni pamoja na kutovumilia wafanyakazi wasio waadilifu.

Kama kutatokea umepata huduma isiyo ridhisha au ufanyaji kazi usiofuata maadili, uaminifu na uadilifu, tafadhali toa taarifa kupitia njia zifuatazo:

1. Kupitia tovuti: http://www.nmbtz.com
2. Kupitia e-mail maalumu: whistleblower@nmbtz.com
3. Kwa posta – Unaweza kutuma barua kwa Afisa Mtendaji kama ifuatavyo:

Afisa Mtendaji Mkuu (Bahasha iandikwe "Siri")
Makao Makuu ya NMB,
P. O. Box 9213,
Azikiwe/Jamhuri Street,
Dar es Salaam, Tanzania.

4. Au kwa kupiga simu zifuatazo:
0658 751 000 Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom
Mtaweza kutunza siri za mteja?
 
Mtaweza kutunza siri za mteja?
Hapo bahasha iandikwe Na hiyo icon tuweke je hata kwa kuichora Na mkono hiyo icon bahasha itapokelewa Na muhusika

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 
Baadhi ya branch za Nmb hasa Dsm zinanyanyasa ndugu zetu wanaofanya kazi kwenye bank hzo, kuna tawi moja liko Dsm jina naliweka kapuni haliwatendei haki ndgu zetu wanaofanya kazi hapo, kila siku wanalalamika, kuna mameneja nasikia wanajifanya waungu watu, wao kazi yao ni kuweka double standard katika shughuli zao za kila siku.

najua mnapitia haka ka uzi ili kupata update za kila siku, kama hamtajirekebisha tutaweka majina yenu hapa tena matatu ili jamii ijue kuwa hamuwatendei haki wafanyakazi wenu hasa wa ngazi za chini
 
Kuna huduma inatolewa na benki ya Posta nimeifurahia sana. Yani mtu akikuwekea pesa au pesa ikitolewa kwenye account napata text sms on the spot.

Sipati shida ya kujua kama ka salary kangu kameingia, NMB igeni muwahudumie wateja wenu.
 
Habari za leo? Naitwa Godfrey I. Kessy. Kuna fedha ambazo nilitakiwa kuzipokea kutoka kwa Linous Nicholaus Melkiory tarehe 25/12/2014 alizokuwa ametuma kwa NMB Mobile tarehe hiyo hapo juu.

Kwa bahati mbaya alikosea akaunti namba yangu. Badala ya kutuma kwenye akaunti yangu(Godfrey I. Kessy) namba 31210003191 alituma kwenye akaunti namba 31210003121. Alikosea namba moja. Badala ya namba 9 akaandika namba 2. Nimejaribu kuwasiliana na Branch manager wa Magu nikaambiwa alikuwa anahama.

Nikafanikiwa tu kuwapata wenye akaunti fedha zilikotumwa ambao ni SHISHANI CO-OPERATIVE SOCIETY. Nikawaomba kwa maandishi wanirejeshee hizo fedha wakaniambia akaunti yao ilishafungwa. Pia waliandika barua kwa manager kuthibitisha kuwa hizo fedha ziliingia kwenye akaunti yao kimakosa. Namba ya simu aliyotumia Linous Nicholaus Melkiory kutuma hiyo fedha ni 0719103278 ambayo mkiwasiliana nae mtampata. Namba ya muamala ni Ref. No: 2KrKOhrDu48. Muamala huu ulifanyika saa 12:25:02.

Tumeshahangaika sana kupata fedha hii lakini hakuna mafanikio. Pamoja na ndugu Linous Nicholaus Melkiory kuandika barua kwa manager kuthibitisha kuwa alikosea namba ya akaunti bado hatujarejeshewa fedha hizi. Naomba msaada wenu Makao makuu. Mimi Godfrey I. Kessy 0767151519.
 
Back
Top Bottom