NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

Ninavyojua ukiomba risit kwa ATM za nmb hakuna makato yyte..

Sasa sijui Ni mm ndo sielewi
 
hebu fafanua vizuri,hivi kuna huduma ya kuomba risiti kwenye ATM au ukitoa pesa risiti inatoka automatic na kama hutaki kuchukua kuna option ya kudeny?
Ndio kwa CRDB wanauliza unataka risiti? Ndio au Hapana? Unachagua.
 
Nimekutana nayo Leo
Nilikuwa na 29000 Nikatoa 20000 nashangaa risit inasema nimebakiwa na 1500 tu.
Ikabidi niingie ndani kuwauliza, wakaniambia nimekatwa vutu vingine vingi
quarterly card fee 4000, makato ya VAT kama aina nne

Sijawaelewa vizuri ila sikuwana chakuwafanya
 
Bado nalia hivi vyama vya wafanyakazi, hili limo ndani ya uwezo wao lakini wameuchuna kama hawaoni kinacho endelea
Vyama vya wafanyakazi haviathiriki wewe kunyonywa. Msingi wao uko kwenye basic salary ni hazina inawasaidia kukata juu kwa juu. Pato lao lipo wanafyonza kilaini tu. Ole wako mtumishi huna mtetezi !!
 
Kwa mtu ulie mji mkubwa wenye bank nyingi.

Kutumia crdb na nmb ni ujinga, maana wana makato ya ajabu mengi sana, benki sahihi ni equity bank ama bank zingine za kigeni
Kwenye equity bank hapo upo sahihi kabisa
 
IMG_5622.jpg

Tumia hii
 
Niende moja kwa moja kwenye mada,

leo nimekwenda kuchukua fedha kwenye ATM zao na nikaomba risiti, kiwango kilichokatwa nikikubwa mno (sh 10,000). Hii gharama ya huduma ya kibenki ni kubwa mno, sikuamini macho yangu, ilibidi niangalie mara mbili kama ni sh 10,000 au 1,000.

Nawashauri NMB waangalie upya makato hayo. Labda kama hawa "encourage" huduma hiyo kutumiwa na wateja wengi.

Nilikuwa naomba kujua makato yakoje kwenye benki zingine kwa huduma kama hiyo wakuu.
...Seriously, Mkuu? Alfu 10 kwa risiti tu ya Muamala wangu?
Hii si Huduma inayopaswa kuwa Bure baada ya Mteja kutoa Hela Yake??
 
Hivi nani aliletaga huu uongo kwamba ukiomba risiti kuna gharama?

Gharama ni moja tu ya kutumia ATM basi unakatwa kila unapotumia na haizidi sh 2000 labda kama utumie huduma zile za MasterCard/Visa

Hii ya elfu kumi sijawahi kuisikia na siamini mpaka nitakapothibitishiwa
Si ndiyo umeisikia au ulitaka usikie wapi
 
Nimekuwekea hapa tariff guide ya mwaka 2021 ya hao NMB,ukiangalia Kipengele cha ATM withdrawal charges utaona kwa kiwango ulichotoa wewe unapaswa kukatwa sh 1,400.

Sasa hio 10,000 inatoka wapi?vinginevyo omba statement uangalie tatizo ni nini?au una mkopo?

Kama kweli umekatwa basi naamini kuna tatizo lingine na sio makato ya ATM.View attachment 1829424
naomba itume tena boss hii
 
Juzi nimetuma elfu 5 kutoka bank ya NMB kwenda bank ya CRDB nimekuja kuangalia makato yake ni elfu 8,500/= niliishiwa nguvu.
Mkuu I wish ningeiona hii comment yako mapema.
Juzi Nlikuwa najisikia vibaya nikashindwa kwenda ATM na nlitakiwa nimtumie mtu hela. Nikasema for the first time ngoja nijaribu kutumia App yao NMB mkononi, Nlituma 70k kutoka NMB kwenda CRDB. Walikata 15K nlisikia kuzimia.

Nikajuta Bora hata ningechukua boda inisubirie [emoji24][emoji24]

Benki Equity tu, sema shida hawana ATM nyingi.
 
Huu ni uzushi tu, au ugeni wa huduma za kibenki, wewe ni wa kupuuzwa tu.
Hakuna bank inayokata zaidi ya 1800 kwa Kila muamala wa ATM..na hata ukitumia ATM za bank nyingine hawakati zaidi ya 3500....aache upotoshaji
 
Hivi nani aliletaga huu uongo kwamba ukiomba risiti kuna gharama?

Gharama ni moja tu ya kutumia ATM basi unakatwa kila unapotumia na haizidi sh 2000 labda kama utumie huduma zile za MasterCard/Visa

Hii ya elfu kumi sijawahi kuisikia na siamini mpaka nitakapothibitishiwa
NMB hawana huduma ya bure. Ni njaa kwa kwenda mbeleee
 
Back
Top Bottom