NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

Hata dirishani, unamchajije mtu kwa kutoa hela yake? Kama makato yapo yalitakiwa kuwa ya kuhifadhi hela tu ingawa nayo hayana maana sababu hela hiyo wenye mabenki wanazalishia faida kwa mikopo. Sasa unamkataje mtu hela eti sababu anachukua hela yake??
Makato kutoa pesa dirishani ni makubwa kwa sababu wana discourage foleni, na watanzania hatuna desturi ya kujiongeza .
Kuweka pesa kwa wakala ni bure kabisa lakini utakuta mtu anakomaaa na foleni za benki kwa masaa, kulipa ada za shule au tozo za serikali
 
Hivi nani aliletaga huu uongo kwamba ukiomba risiti kuna gharama?

Gharama ni moja tu ya kutumia ATM basi unakatwa kila unapotumia na haizidi sh 2000 labda kama utumie huduma zile za MasterCard/Visa

Hii ya elfu kumi sijawahi kuisikia na siamini mpaka nitakapothibitishiwa
Possibly ametumia atm tofauti na ya benki yake kupitia Visa card au MasterCard yake ndio maana makato ni makubwa, Mimi walinikata 12,000/=
Ila for sure hizi benki zetu local ukitumia atm tofauti wanakata sana sijui kwanini wakati ni ishu ya local interbanking systems ile tiss [emoji26]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
KWA MUJIBU WA "NMB TARIFF GUIDE" YA MWAKA 2021.

1. Ukienda NMB kutoa pesa, ila ukaomba wakupe CHENJI CHENJI ZA COIN.
-Utakatwa sh. 1180 kwenye account yako kwa kila LAKI MOJA ya COIN utakazopewa.

Mf: ukiomba chenji za 500 za million 1, utakatwa 11,800 kwenye account yako.

Note: Hiyo elfu 11,800 ni nje ya ile 6500 unayokatwa kwa kutolea dirishani.

Kwaiyo usipokua makini,
unaweza jikuta karibu elfu 18 imekatwa kwa kutoa muamala mmoja dirishani.

2. Ukienda NMB kuweka kwenye account yako PESA ZA COIN,
utakatwa 10% ya pesa zote ulizopeleka kwenye account yako.

Mf: ukipeleka coin za 100,000 , kitakachoingia kwenye account ni 90,000[emoji2][emoji116]View attachment 1830524View attachment 1830525
Duh mkuu umenifungua macho sikuwa nayajua haya, wameweka vikolokolo vingi kutulevya maboya
 
Hiyo ni ada ya risiti au stetement, sijakuelewa vizuri, unaombaje risiti kwenye ATM wakati ukitoa hela risiti huwa inatoka automatic hela zikisha toka!
Haitoki automatic unaulizwa unahitaji receipt unaponyeza yes au No
 
Hivi gharama zipoje kwa
Anayetoa ndani kwa Bank teller?
Anayetoa kwenye ATM
anayetoa kwa wakala
Anayeivuta kwenye simu kutoka Bank
Anayetoa kwenye ATM gharama ni nafuu kuliko hizo njia nyingine mkuu!!
 
Niende moja kwa moja kwenye mada,

leo nimekwenda kuchukua fedha kwenye ATM zao na nikaomba risiti, kiwango kilichokatwa nikikubwa mno (sh 10,000). Hii gharama ya huduma ya kibenki ni kubwa mno, sikuamini macho yangu, ilibidi niangalie mara mbili kama ni sh 10,000 au 1,000.

Nawashauri NMB waangalie upya makato hayo. Labda kama hawa "encourage" huduma hiyo kutumiwa na wateja wengi.

Nilikuwa naomba kujua makato yakoje kwenye benki zingine kwa huduma kama hiyo wakuu.
Kuomba risiti huwa ni bure gharama huwa ni Ile withdrawal fee ambayo ni Kama buku tu...nenda bank kaombe statement watakuelewesha hyo elfu imekatwa ya nini
 
Niende moja kwa moja kwenye mada,

leo nimekwenda kuchukua fedha kwenye ATM zao na nikaomba risiti, kiwango kilichokatwa nikikubwa mno (sh 10,000). Hii gharama ya huduma ya kibenki ni kubwa mno, sikuamini macho yangu, ilibidi niangalie mara mbili kama ni sh 10,000 au 1,000.

Nawashauri NMB waangalie upya makato hayo. Labda kama hawa "encourage" huduma hiyo kutumiwa na wateja wengi.

Nilikuwa naomba kujua makato yakoje kwenye benki zingine kwa huduma kama hiyo wakuu.
First year huyo ashajua kutumia ATM bas shida tupu,makato huwa ni 1,000 tu,acha uongo!!
 
Bado nalia hivi vyama vya wafanyakazi, hili limo ndani ya uwezo wao lakini wameuchuna kama hawaoni kinacho endelea
 
Back
Top Bottom