NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

NMB tuoneeni huruma, kiwango mnachokata baada ya kuomba risiti ni sh10,000 -- ni kubwa mno

Benki ya makabwela lkn inawanyonya mwakabwela.
wakati ukwasi iliyo upata umetokana na hao hao makabwela.
rudisheni fadhila kwa makabwela.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiomba risiti kuna pesa unakatwa lakini ni ndogo sana tofauti na madai ya mleta mada! CRDB kwa mfano, wao wanakata Sh. 300/=.
hebu fafanua vizuri,hivi kuna huduma ya kuomba risiti kwenye ATM au ukitoa pesa risiti inatoka automatic na kama hutaki kuchukua kuna option ya kudeny?
 
hebu fafanua vizuri,hivi kuna huduma ya kuomba risiti kwenye ATM au ukitoa pesa risiti inatoka automatic na kama hutaki kuchukua kuna option ya kudeny?
Haitoki automatic! Ukisha-click kiwango unachotaka kutoa, utaulizwa ikiwa unahitaji risiti! Kwahiyo risiti itatoka endapo utajibu "ndiyo"! Lakini sio tu hadi utoe pesa, pia unaweza kuomba risiti bila kutoa pesa kama service utayochagua ni kuangalia balance! Hapa pia utaulizwa ikiwa unahitaji risiti au utaangalia balance kwenye screen pekee.
 
Hiyo ni ada ya risiti au stetement, sijakuelewa vizuri, unaombaje risiti kwenye ATM wakati ukitoa hela risiti huwa inatoka automatic hela zikisha toka!
Wewe unazingua sasa, NMB risiti haitoki automatic hadi uombe na kuna charge za kupata risiti
 
Niende moja kwa moja kwenye mada,

leo nimekwenda kuchukua fedha kwenye ATM zao na nikaomba risiti, kiwango kilichokatwa nikikubwa mno (sh 10,000). Hii gharama ya huduma ya kibenki ni kubwa mno, sikuamini macho yangu, ilibidi niangalie mara mbili kama ni sh 10,000 au 1,000.

Nawashauri NMB waangalie upya makato hayo. Labda kama hawa "encourage" huduma hiyo kutumiwa na wateja wengi.

Nilikuwa naomba kujua makato yakoje kwenye benki zingine kwa huduma kama hiyo wakuu.
Makato hayo umesoma wapi?
Kwenye ATM slip inaandikwa kiasi ulichotoa, actual amount na available amount. Wapi umeona wameandika withdraw charge 10,000?
 
Uwongo!

Hawana MasterCard/Visa ambayo ungeweza kutoa PESA benki yoyote?

Mbona mnajivunia sana UJINGA!
Hakuna namna unaeza itumia Mastercard au visa card ndani ya benki nyingine
Cards zinaishia nje kwenye Atm tu, ambapo limit ni milion moja i tu, kwa benki nyingi.
 
Mkuu usipokuwa makini humu kuna watu kazi yao siyo kuchangia ila ni kutengeneza burudani 😀 [emoji1787]
Yeye ndo mtoa burudani, kwamba ati una Mastercard ya nmb ndo uingie crdb bank ndani ukatoe pesa kutoka nmb? Umeona wapi hiyo?
 
Makato hayo umesoma wapi?
Kwenye ATM slip inaandikwa kiasi ulichotoa, actual amount na available amount. Wapi umeona wameandika withdraw charge 10,000?

Makato hayo umesoma wapi?
Kwenye ATM slip inaandikwa kiasi ulichotoa, actual amount na available amount. Wapi umeona wameandika withdraw charge 10,000?
kwenye screen ya mashine, mara zote mashine huandika kiasi kilichokatwa kwenye huduma uliyoipata, lakini baadaye nilifanya hesabu kwa kuwa nilikuwa nimetoa fedha kama siku 3 zilizopita kabla, roundfigure nilikuwa naijua nikajiridhisha ni kweli walikuwa wamekata, labda ni monthly charge ndiyo ilikuwa imekatwa hapa bado sina uhakika lakini nilichokishuhudia kwenye screen ni 10,000
 
Niende moja kwa moja kwenye mada,

leo nimekwenda kuchukua fedha kwenye ATM zao na nikaomba risiti, kiwango kilichokatwa nikikubwa mno (sh 10,000). Hii gharama ya huduma ya kibenki ni kubwa mno, sikuamini macho yangu, ilibidi niangalie mara mbili kama ni sh 10,000 au 1,000.

Nawashauri NMB waangalie upya makato hayo. Labda kama hawa "encourage" huduma hiyo kutumiwa na wateja wengi.

Nilikuwa naomba kujua makato yakoje kwenye benki zingine kwa huduma kama hiyo wakuu.
bado unatumia haya mabenk ya mwendazake?
wajinga ndio waliwao, tumia benk za kigeni, Equity, Exim, ABSa, nyingine
 
Nilichojifunza kwenye huu mkeka
  • Kuna tuvipengele tudogodogo twingi usipokuwa makini unaliwa kichwa
  • Mabenki washindani wa NMB watautumia kuwapiga kibuti
  • Kuna mambo wateja hawaambiwi wanapofungua akaunti ila wanakutana na vibweka wakishakuwa wateja
KWA MUJIBU WA "NMB TARIFF GUIDE" YA MWAKA 2021.

1. Ukienda NMB kutoa pesa, ila ukaomba wakupe CHENJI CHENJI ZA COIN.
-Utakatwa sh. 1180 kwenye account yako kwa kila LAKI MOJA ya COIN utakazopewa.

Mf: ukiomba chenji za 500 za million 1, utakatwa 11,800 kwenye account yako.

Note: Hiyo elfu 11,800 ni nje ya ile 6500 unayokatwa kwa kutolea dirishani.

Kwaiyo usipokua makini,
unaweza jikuta karibu elfu 18 imekatwa kwa kutoa muamala mmoja dirishani.

2. Ukienda NMB kuweka kwenye account yako PESA ZA COIN,
utakatwa 10% ya pesa zote ulizopeleka kwenye account yako.

Mf: ukipeleka coin za 100,000 , kitakachoingia kwenye account ni 90,000[emoji2][emoji116]
2021-06-26-10-58-19.jpg
2021-06-26-10-57-50.jpg
 
Mkuu Tafadhali cheki vizuri....mbona umenitisha sana???
 
Usiamini kirahisi uzushi wa huyu jamaa, kwa wakala ndo makato makubwa ni kama kutolea pesa dirishani…. ATM haijawahi kufika huko.

Let alone tozo ya risiti.
Hata dirishani, unamchajije mtu kwa kutoa hela yake? Kama makato yapo yalitakiwa kuwa ya kuhifadhi hela tu ingawa nayo hayana maana sababu hela hiyo wenye mabenki wanazalishia faida kwa mikopo. Sasa unamkataje mtu hela eti sababu anachukua hela yake??
 
Back
Top Bottom