NMB wagoma kurudisha hati ya nyumba, japo deni lao limeshalipwa lote

Status
Not open for further replies.
Lengo la benki wanakulazimisha ukope tena kwao hiyo tabia ni kawaida sanaa kwa benki za bongo, wanakopesha ili wakufilisi kwa kushindwa kulipa sasa hapo wakutegemea kama utamaliza, hati utapewa ila baada ya kuisotea .
 
Si kuna utaratibu wa kurejesha hatii? Kama ilivyo kwa kupeleka hati ili kulinda mkopo?
Sasa kama utaratibu haujafanyika na Hati haijarudishwa ndio hivyo unaandika barua ya kuhoji na sio kuongea ongea tu bila records zozote, nina uhakika hata katika kurudishiwa hati / kuomba hati ni kwamba uliandika barua kwamba umemaliza deni hivyo unaomba hati yako... Hivyo vyote vinakuwa on record.

Na kama bado unakumbushia na kuuliza kwanini hio Hati haijarudi... Unakuwa na Kumbukumbu zote...
 

Bro ni miaka minne tangu deni liwe written off. Ninachojua ukimaliza mkopo kuna fomu za kisheria za ku discharge mkopo. Iwapo mkopo kama ulisajiliwa. Hakuna cha kuandika barua wala nini hapo. Watoe hati ya watu. Maana wana tabia ya kuazimisha hati za watu kwa mikopo ya watu wengine. Ndiyo maana hapo nimewaambia waende takukuru inshu ifike mwisho.
 
Akiwauliza wanasema tatizo nini ? Imepotea, Imeliwa na Panya ? Hakuna Records ? Hajamaliza Deni au ni kitu gani ?; Sababu bila kujua jibu analopewa ni vigumu kuelewa..., Na popote watakapoenda lazima kutakuwa na mawasiliano (communication) na communication nzuri ni ya kimaandishi ambayo yanakuwa on record..., Kuandika barua sio kwamba mtu unapenda sana uandishi au pesa za kupoteza ni kufuata mtiririko na kuwa na record ili lolote likitokea liweze kueleweka... Ni muda mrefu umepita na Hati ni Haki yake sasa kama Hajapewa Sababu ni nini ? Hata huko Takukuru atakapokwenda wataamuuliza ni jibu gani amepewa...
 
Unaweza kuta nyumba walishauza maana walijua hataweza toboa malipo! Hapo aandike barua kwa meneja wa benki au branch kuomba hati, kama asipopewa jibu zuri basi atafute wakili matata! Hapo ni kesi anafungua na kuomba fidia ya usumbufu!

Pia akishaandika barua asipopewa majibu mazuri anaweza peleka TAKUKURU wa eneo hilo then takukuru watamuita yeye pamoja na meneja wa benki atoe ufafanuzi!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…