NMB yawaburuza CRDB na wenzake kifaida chini ya Mwanamama Ms Ruth Zaipuna, huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt. Tulia mwingine ni huyu Mama

View attachment 2805767
MS Ruth Zaipuna Mkurugenzi Mkuu NMB.

======
Wasalaam Jf team,

Waswahili tunasema " Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake Mpeni "

Sote tunakumbuka baada ya NBC Bank kuvunjwa Mwaka 1997 na baadae kuanzishwa kwa Benki mpya ya Makabwera ya NMB na baadae Benki hiyo kubinafsishwa kwa Rabobank ya Uholanzi iliyomiliki hisa asilimia 49.

Wakati wote NMB PLC imekuwa ikiongozwa na watu kutoka nje ya nchi tu isipokuwa huyu Mkurugenzi wa Sasa Bi Ruth Zaipuna aliyekabidhiwa nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu rasmi mwaka 2020.

Kumbukumbu zinaonesha wakati mama huyu anaingia madarakani NMB bank ilikuwa na matawi yapatayo 100 tu nchi nzima na ATMs zipatazo 500 nchi nzima.

Leo NMB bank imefikisha matawi zaidi ya 200 na ATMs zaidi ya ATMs 1,000 nchi nzima hii ni sawa na kusema mama huyu ameikuza bank hii ya Makabwera kwa zaidi ya marambili, yaani ukuaji wa 100% au kwa lugha rahisi ni sawa na kusema NMB bank PLC imefika katika Kila Jimbo la Uchaguzi la kiserikali haba bara.

Kutoka katika tovuti ya NMB taarifa zinaonesha NMB bank ilikuwa na wateja wasiozidi 600,000 miaka kumi iliyopita na wakati huu wa Ruth Zaipuna banki hii imefikia wateja zaidi ya 2.5M nchi nzima,karibu mara nne zaidi.

Kuhusu Uzalendo & Uzawa Kunajambo la kujifunza kwa hawa wanawake watatu yaani Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Spika wa bunge la JMT na IPU Mhe Dkt Tulia Hassan na Mkurugenzi Ruth Zaipuna kwa namna wanavyoleta mabadiliko ya kasi kwenye taasisi wanazoziongoza,

Hebu tazama orodha hii ya faida kwa mabenki kumi ya Tanzania yaliyofanya vizuri katika robo ya tatu tu ya mwaka huu wa 2023 ndio utaelewa vizuri nachosema kuhusu huyu Mkurugenzi.

1. NMB Bank: TZS 398 billion

2. CRDB Bank: TZS 280 billion

3. Stanbic Bank: TZS 95 billion

4. StanChart: TZS 64 billion

5. NBC Bank: TZS 62 billion

6. Citibank TZS 44 billion

7. PBZ TZS 41 billion

8. Exim Bank TZS 40 billion

9. Absa Bank TZS 37 billion

10. KCB Bank TZS 35 billion

Taarifa zinaonesha faida ya Jumla kwa mabenki yote Tanzania ni shilingi trilioni moja katika robo hii ya tatu, Hii ni sawa na kusema NMB PLC pekee anamiliki 40% ya faida yote huku ikimpiku kwa mbali mshindani wake wa karibu CRDB bank kwa zaidi ya TZS 118 BL sawa na 70% ya faida yake.

Wakati Ruth Zaipuna anakuwa Mkurugenzi Mkuu Benki hii ilikuwa na wastani wa faida ya TZS 200BL baada ya kodi wakati Leo faida imekuwa na kufikia wastani wa karibu TZS 400BL kwa mwaka yaani sawa na marambili zaidi.

Pia,taarifa zinaonesha Benki ya NMB inashika nafasi ya sita kwa Ukubwa katika nchi zote Kusini mwajangwa la Sahara na ndio Benki pekee toka Tanzania inayoshindana kimataifa,

Watanzania tunalakujivunia toka kwa Mkurugenzi huyu mzawa akisaidiwa na management nzima ya NMB PLC pamoja na Bodi ya Wakurugenzi wa NMB PLC chini ya Dkt Edwin Mhede, Hakika Mmestahili Heshima.

Kwa matokeo haya, Huenda Ukimwacha Rais Dkt Samia na Spika Dkt Tulia mwingine ni huyu Ruth Zaipuna wa NMB PLC deserves better,
ila kusema ukweli Singida kuna vichwa vyenye akili na hawana arogance na kujitangaza km Hayas na chagas, hawa hasa Chagas wametuchosha na sifa za kijinga humu mtandaoni wakati they are just below normal.
 
Anafaa sana huyu Rais amwangalie kama atakubali kutoka NMB
 
Spika kijana Tulia na huyu Ruth ni hatari. Halafu ulivyoandika Ms ina maana hajaolewa? Ni mzuri hatari anaweza kwenda sawa hata na kina Jokate.
 
Sasa ,tunatamani kusikia ndoa yake ya Lini,umri huo anaitwa Ms ,JAMANI !

Ameolewa ni mama wa watoto wanne

Mlokole huyo enzi za udsm ndio walikuwa wale wadada praise team.

Alipiga zake first class akaajiriwa Big 4 PwC straight from chuo.

Ameolewa mapema sana kabla hajavuka 27. Na akazaa zake fasta fasta watoto wanne wa kiume.

Amefanya kazi kama Auditor PWC kwa miaka 10.

Kisha akahamia Standard chartered bank kwa cheo cha Chief Financial Officer. Amehudumia hicho cheo cha CFO standard chartered kwa miaka 6. Ndipo akahamia NMB bank na kuwa CFO kwa mwaka mmoja kabla hajapandishwa cheo na kuwa CEO
 
Please ukubwa in terms of what? Kama ni total assets CRDB ina Trillion 11.64 ila NMB ina Trillion 10.4!! Umetumia parameters zipi. Utusaidie kwa faida ya wote.
Ukabwa wa assets wakati mwenye asset ndogo zaidi yako anaweza zalisha faida kuliko mwenye asset zako ?CRDB mjitafakari saaana
 
Ameolewa ni mama wa watoto wanne

Mlokole huyo enzi za udsm ndio walikuwa wale wadada praise team.

Alipiga zake first class akaajiriwa Big 4 PwC straight from chuo.

Ameolewa mapema sana kabla hajavuka 27. Na akazaa zake fasta fasta watoto wanne wa kiume.

Amefanya kazi kama Auditor PWC kwa miaka 10.

Kisha akahamia Standard chartered bank kwa cheo cha Chief Financial Officer. Amehudumia hicho cheo cha CFO standard chartered kwa miaka 6. Ndipo akahamia NMB bank na kuwa CFO kwa mwaka mmoja kabla hajapandishwa cheo na kuwa CEO
Jamaa wanataka kuoa MD hahaa
 
Back
Top Bottom