No body cares: Watu tupo bize mtandaoni, tume-lose touch na human connection

No body cares: Watu tupo bize mtandaoni, tume-lose touch na human connection

Kwahiyo Mkuu Tufanye Nini Kuboresha?
Ni ngumu kwa maisha ya sasa kuyaishi km zamani...ila tujitahidi walau kwa asilimia fulani. Tupate muda tukae na wapendwa wetu, tuwatembelee wapendwa wetu, tutoke na familia zetu kwenda kukagua ndugu, jamaa na majirani. Tutoke na wtt wetu walau kuzungukazunguka nao kufanya mazoezi au kwenda nao viwanjani kuangalia Michezo. Tushiriki nao kwenye ibada, n.k
 
Yan hata misibani kila mtu busy na simu Mfiwa hafarijiwi tena kama zamani..... Atajijua mwenyeweeee

Huzuni kuuu
Kuna clip moja niliiona jamaa yupo Umrah Makkah na simu yake anacheza game.
Familia mtatoka out vizuri mkifika sehemu kila mmoja na simu yake hamna hata maongezi ya kifamilia, vyakula vikisaviwa kwenye meza kabla kula watu wanapiga picha. Yaani zombies kwisha kazi.
 
Umeonaaa sasa... Yani siku hizi wanadamu tumekuwa wa ajabu...

Sasa sijui mfiwa atapata wapi nguvu ya kuona pole yake status...
hata likizo tunashindwa kwa kuwapeleka watoto,..maana kutembeleana siku hizi imegeuka kuchorana tu.... Watoto wanamalizia likizo kwenye TV na tuition..😞
 
Nachukiaga mtu ananikuta nimeakaa sehem au ktk gari ata asalimii anatoa msimu wake anaperuzi mwanzo mwisho nami nauchuna kimya, ukimkuta mtu msalimie zungumza then ndo uanze kuwa bize na simu
 
Kuna clip moja niliiona jamaa yupo Umrah Makkah na simu yake anacheza game.
Familia mtatoka out vizuri mkifika sehemu kila mmoja na simu yake hamna hata maongezi ya kifamilia, vyakula vikisaviwa kwenye meza kabla kula watu wanapiga picha. Yaani zombies kwisha kazi.
Nobody cares 🤣🤣 hapo kila mtu anawazia atapata likes ngap, za pizza anayo kula.
 
Ni ngumu kwa maisha ya sasa kuyaishi km zamani...ila tujitahidi walau kwa asilimia fulani. Tupate muda tukae na wapendwa wetu, tuwatembelee wapendwa wetu, tutoke na familia zetu kwenda kukagua ndugu, jamaa na majirani. Tutoke na wtt wetu walau kuzungukazunguka nao kufanya mazoezi au kwenda nao viwanjani kuangalia Michezo. Tushiriki nao kwenye ibada, n.k
Hakika kubalance social life ya maisha halisi. Watu hutake things for granted alaf baadae wanaanza kujihis wapweke. It's small things kama ulivyo eleza hapo ndo hu matter katkia maisha. Take time to make real connection with close people around you, not people you see on social media ambao probably you'll never meet.
 
Nachukiaga mtu ananikuta nimeakaa sehem au ktk gari ata asalimii anatoa msimu wake anaperuzi mwanzo mwisho nami nauchuna kimya, ukimkuta mtu msalimie zungumza then ndo uanze kuwa bize na simu
Alaf akipata shida ndo aanze Salam! Hakika kizaz cha nyoka hichi🤣
 
Kuna clip moja niliiona jamaa yupo Umrah Makkah na simu yake anacheza game.
Familia mtatoka out vizuri mkifika sehemu kila mmoja na simu yake hamna hata maongezi ya kifamilia, vyakula vikisaviwa kwenye meza kabla kula watu wanapiga picha. Yaani zombies kwisha kazi.
Eeh yani smartphones zimechukua nafasi kubwa sana kwenye maisha yetu...

Kazi kweli kweli
 
hata likizo tunashindwa kwa kuwapeleka watoto,..maana kutembeleana siku hizi imegeuka kuchorana tu.... Watoto wanamalizia likizo kwenye TV na tuition..😞
Siku hizi hayo mambo hakuna...

Hakuna tena issues za likizo kwenda kwa babu na bibi kijijini..
 
Umezungumza vizuri hayo ulotaja si mageni na yamekuwepo miaka nenda rudi huenda yameshamiri sababu ya kukua kwa tech. n.k

Lakini ninachomaanisha kuna baadhi ya mambo hatuwezi kuyaishi tena nyakati hizi, mf. Socialization iliyokuwepo zamani.

Au watu kuwa bize mtandaoni unadhani ni kazi rahisi kuwafanya wasiwe bize mtandaoni na wawe bize na mambo mengine, wangapi wataweza kwa mazingira tuliyopo?
Ni sawa; na sio rahisi tena na wala sio vyema kuwafanya au kuwabadilisha watu wasiwe bize mtandaoni. Ninachosema ni kwamba: Je, huko mitandaoni wanakuwa bize kwa lipi? Kuchati, kutumiana picha za porn, kujazana ujinga e.g. tutoroke twende Nchi za nje, kufanya utapeli wa kimtandao n.k.???. Ingependeza sana Watu wawe bize mtandaoni kufanya biashara halali, Kujifunza masomo na kujiongezea maarifa au kupeana taarifa za Fursa za kiuchumi, ajira n.k. Hayo nadhani ni matumizi chanya ya Mitandao na ndo Ku-socialize kidigitali badala ya kukutana physically. Hiyo ni sawa.
 
Eeh yani smartphones zimechukua nafasi kubwa sana kwenye maisha yetu...

Kazi kweli kweli
Ndo maana mtoto mmoja chekechea, alipoulizwa na mchungaji angependa baadaye kuwa nani (aseme vision /ndoto yake) akajibu Ningependa kuwa simu. Kwa mshangao huyo pastor akamwuliza tena kwa nini? Mtoto akajibu kwa sababu mama na baba wanatembea nazo, kuzibeba na kuongea nazo lakini mimi huniacha peke yangu wala hawazungumzi nami.:BANNED:
 
Pole sana, hii imetukumba wengi sana! Naweza kurelate na ww kuhusu kujitenga na kutengwa! Ina madhara mengi hasa psychological. Na tatizo la mitandao watu hawana sympathy hata kidogo na pia hawakujui hivyo hata ile kujali kua huyu ni mtu kama mm na anahisia kama mm inakua ngumu. Mm nahisi kwasabau ya kutengwa na kujiona wapweke imetusababisha wengi kuwa wahanga.

Jaribu kfatilia mada nzuri kama hizi hapa Jf achana na mada mbaya! Au hata ukifata hizo mada nenda kwa lengo la kujifurahisha. Usichukulie serious, hakuna anaejua unapitia nini hapa! Pia jaribu kuondoa mawazo mabaya kuhusu kutengwa ndo dunia ilivyo, watu hatujaliani kama zamaini.
Asante sana ndugu, uzuri pamoja na hayo yoote ninaamini katika kupuuzia chochote ninachokosa maslahi nacho.
 
Asante sana ndugu, uzuri pamoja na hayo yoote ninaamini katika kupuuzia chochote ninachokosa maslahi nacho.
Nanukuu: " ......ninaamini katika kupuuzia chochote ninachokosa maslahi nacho."
Je, kukitokea msiba kwa jirani yako huendi kutoa pole? Kama utakwenda hapo; kuna maslahi gani kwako?
 
Nanukuu: " ......ninaamini katika kupuuzia chochote ninachokosa maslahi nacho."
Je, kukitokea msiba kwa jirani yako huendi kutoa pole? Kama utakwenda hapo; kuna maslahi gani kwako?
Hapana ndugu yangu, si katika mambo ya kijamii, labda comment yangu ya kwanza kwenye uzi huu ndio ilinipelekea kusema hivyo.
 
Back
Top Bottom