No hate, no fear. Very good slogan lakini mbona jamaa wanaendelea kuonesha hate kali dhidi ya hayati?

Wee mtoto, hii tabia na desturi mbaya namna hii nani kakufundisha. Kumbuka mheshimiwa raisi amesema huwa anapita humu Jf. Pia na mwenyekiti wako Mh. Mbowe naye huwa anapita humu kila siku.
unapoteza uhuru wako kwasababu unaogopa unasomwa na nani?
 
Usihitaji kujua saana! Ila waweza endelea tu kutoa matusi vile utakavyo mkuu
Usirudie tena kuita wapiga dili na vilaza watu ambao wamedhurumiwa stahiki zao. Jifunze kuheshimu struggles za watu
 
Na 2025 wataipata tena fresh kwani mama anaupiga mwingi kuendeleza aliyoyaanzisha mtangulizi wake. Salama yao itakuwa ni kususa uchaguzi mkuu kwa kisingizio cha katiba mpya.

Eti Katiba Mpya, si wasubiri hadi watakaposhika dola ndipo watuletee hiyo katiba mpya wanayoitaka. Hawajui kuwa hata taifa kubwa la USA katiba yao ni ya tangu wapate uhuru kutoka kwenye utawala wa Muingereza tarehe 4 July 1776. Huwa wanaifanyia tu updates na upgrades mara kwa mara kuendana na matakwa ya wakati. Hadi as late as 1920s (takribani miaka 150 baada ya uhuru) katiba ya USA ilikuwa hairuhusu wanawake kupiga kura wala kushika cheo cho chote cha kisiasa. Sisi tuna miaka 62 tu baada ya kupata uhuru.

Hawa jamaa hawajui kwamba nchi ya Uingereza iliyowahi kutawala karibu dunia nzima, yenyewe haina katiba ye yote ya nchi. Uingereza ndiyo iliyoyataka yaliokuwa makoloni yake yawe na katiba ya utawala wa nchi ambayo itaziongoza kutokutunga sheria za kijinga. Wao waingereza hawahitaji katiba kwani ni waelewa (siyo wajinga) na hivyo hawawezi kutunga sheria za kijinga. Sasa hawa jamaa zetu wanataka tuitupe kabisa katiba yetu kwenye dustbin badala ya kuendelea kuifanyia updates na upgrades pale panapohitajika.

Eti hizo updates na upgrades wao wanazifananisha na kuweka viraka kwenye suruali! Wanafikiri hata hiyo mpya kama itapatikana haitakuwa inawekewa hivyo viraka. Hawaoni kuwa hata nchi jirani yetu katiba mpya yao ndani ya kipindi cha miaka miaka takribani mitano tayari imeshawekewa viraka kibao. Hata hiyo ya Warioba waliyoipenda saa hizi wanasema imepitwa na wakati, inahitaji kuwekewa viraka kabla ya kwenda nayo.
 
Uwepo wa Magufuli umesaidia tumewajua wapinzani feki.
 
Yaani watu wanasonga mbele wanazungumzia katiba wewe bado unaongelea watu ambao hatunao🤔 mbumbumbu
Katiba mpya ilishazungumzwa sana. Maamuzi yanasubiriwa. Kuendelea kuimba wimbo huo ni kukosa hekima na unaweza kuharibu maridhiano. Kinachotakiwa ni kutoa mapendekezo ya mambo unayoyaona yaingizwe kwenye katiba, be it a new or old katiba. Siyo kuimba tu kama kasuku kwamba unataka katiba mpya. It doesn't make sense my dear.
 
Dr lalama subiri. Yaani wewe ni Dr ambaye kazi ni kulaumu tu wewe unafanya nini kama kweli ni Dr na usomi wako badala ya kulalama. Ulitaka wapinzani wafanye nini? Wewe ungeenda kuandamana au tu ni kujificha mitandaoni. Hawa ni watanzania ambao wanajitolea pesa, muda, na maisha yao kwasababu ya taifa hili halafu tuna Madaktari fake wanabaki kulalama kila siku.
 
JPM atabakia kuwa ndiye kiongozi aliyewahi kupendwa saana na watu wa kati na daraja la mwisho!

Mafisadi na vilaza nyie endeleeni kutoa nyongo zenu tuone mwisho wenu!
Mwisho wetu au mwisho wake...
 
Mhhh ndiyo uelewa wako unapoishia? Your argument is too shallow and you've no point at all. Endelea tu kuimba kama kasuku, ' tunataka katiba mpya .... watanzania wanataka katiba mpya ...... as if your a spokesman ya hao watanzania, halafu weye ulishakimbilia ughaibuni kutafuta green pasture. Usitake kutuingilia mambo yetu ya kujenga nchi yetu. Usitake kuingilia maridhiano yetu wewe uliyekimbia nchi kwa kukosa uzalendo. You know very little about our country currently. Wala usitake kujua mimi ni nani.
 
Kukosoa ni tofauti na hate
 
JPM atabakia kuwa ndiye kiongozi aliyewahi kupendwa saana na watu wa kati na daraja la mwisho!

Mafisadi na vilaza nyie endeleeni kutoa nyongo zenu tuone mwisho wenu!
Labda dalaja la mwisho la kigoma[emoji3061]
 
Ni kweli hawakuamini kilichotokea kama Teeth wangeingilia uchaguzi na kuweka kura bandia.
 
Sifa kubwa ya kuwa Chadema ni kuwa na chuki kali dhidi ya mtu yeyote anayetia urambaji asali wao.
 
Mpaka kesho Waisraeli wanamlaani Reich Fuhrer Adolf Hitler japo kajifia miongo mingi iliyopita.
Hata Yuda Iscariot karne zaidi ya mbili haja samehewa wala kusauliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…