Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Baada ya uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2019 huku kukiwa na kumbukizi ya kufutwa kiharamu Kwa uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2015, watanzania wengi wenye akili timamu walisema kuwa hawatashiriki kupiga kura tena kwenye maisha yao labda kama Sheria za uchaguzi zitarekebishwa.
Lakini mwaka 2020 Kwa ahadi za uongo za CCM kuwa hawatafanya uharamia kwenye uchaguzi, baadhi ya watanzania wakaamua kushiriki uchaguzi.
Lakini kama ilivyokuwa mwaka 2019 kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, ndivyo mwaka 2020 CCM ilifanya tena uharamia na kuuiba uchaguzi mzima.
Baada ya mwaka 2020 hata wale watanzania walioghilibiwa na CCM nao akili zikawarudia na kurudia msimamo wao wa awali kuwa kama mfumo wa uchaguzi hautarekebishwq na wao hawatashiriki kwenye chaguzi zijazo.
Mwaka 2024 uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na kuwa na idadi ya chini kabisa ya watanzania kushiriki, lakini bado ukavurugwa na CCM.
Baada ya uchaguzi wa Serikali za mitaa wa mwaka 2024, asilimia tisini na tisa (99%) ya watanzania wenye akili timamu wakajiapiza kuwa hawatashiriki tena kupiga kura labda mifumo ya kiuchaguzi ibadilishwe kisheria.
CHADEMA kwa kuwa inategemea nguvu ya umma kuendesha siasa zake, ikawa haina njia nyingine zaidi ya kukubali kufuata matakwa ya watanzania wenye akili timamu kuwa No reforms No election.
Kwa ivo No reforms No election ni takwa la watanzania wenye akili timamu wanaoipenda nchi yao na wala siyo njia ya CHADEMA kujitafutia umaarufu wa kisiasa!!