No Reforms No Elections: Kama kweli itatokea ni nini kitawakabili Lissu na CHADEMA

Tueleze unazungumzia "uchaguzi" gani wa kidemokrasia Tanzania unao lindwa na Katiba.
Hivi katiba hii mnaikumbuka wakati mnapojitafutia maslahi na wakati mwingine mnaiona kuwa ni "vikaratasi" tu!

Kinacho shangaza ni watu wanao onekana kuwa na akili timamu kabisa, halafu wanajifanya kujisahaulisha wanacho kizungumzia, wakitegemea na watu wengine wote wafikiri wanavyo fikiri wao!
Ni katiba ipi Tanzania inayolinda uchafuzi wa kura za wananchi kila wakati!
Ni katiba ipi iliyo halalisha uchafuzi wa serikali za mitaa ambao viongozi wote ndani ya CCM wanajitangazia kupata ushindi mnono!
Katiba hiyo hiyo ya mwaka 1977 iliheshimiwa hata na JKN mwenyewe. Na amini hata waliomfuata akina AHM, Mkapa na Kikwete waliiiheshimu.

Tatizo lilianza mwaka 2020 na Magufuli aliyetaka mpaka kujiongezea muda wa kutawala, lakini Mungu akatusaidia kumuondoa duniani.

Chaguzi za mwaka jana za S/Mitaa nazo zilikuwa na hangover ya yale yaliyotokea kipindi cha 2019/20.

Ila haya mambo yanaongeleka, siyo ya kupeleka wananchi barabarani
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na sheria za nchi, uchaguzi ni msingi wa demokrasia na haki ya kikatiba (Kwa mfano, Katiba ya Tanzania ya 1977, Kifungu cha 5 na 21).

Kutoa vitisho vya "kuharibu uchaguzi" au kuanzisha "uasi" ni uvunjifu wa sheria za Tanzania, kama vile:
(1) Kanuni ya Jinai (Penal Code): Vifungu namba 38 (kuchochea fujo- sedition), 40 (kuchochea machafuko-inciting unrest), au 41 (kuashiria kusudi la kuvunja utulivu wa umma-conspiracies to breach public peace) vinaweza kutumika kuwashitaki wanaotangaza mambo hayo.

(2) Sheria za Usalama wa Taifa: Kuchochea uasi kunaweza kuchukuliwa kama udhalilishaji wa mamlaka ya Serikali, na kusababisha kukamatwa, mashtaka, na hukumu ya jela ikiwa wata patikana na hatia.

(3) Msajili wa Vyama vya Siasa, Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa (Namba 5 ya 1992), ana wajibu wa kuhakikisha vyama vinazingatia Katiba na sheria za nchi. Ikiwa chama au wanachama wake kinatangaza mambo yanayokiuka Katiba (kama vile kukataa uchaguzi kwa njia za vurugu), Msajili anaweza:
  • Kutoa onyo la kisheria
  • Kufuta chama kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Kifungu cha 11(2)(e), ikiwa kinaendelea kukiuka masharti ya kikatiba.

ANGALIZO:-
Hata hivyo, haki ya kukosoa na kuomba mabadiliko kwa njia za amani ni haki za kikatiba (Kifungu cha 18 na 20). Hivyo, msimamo wa Tundu Lissu unahitaji kutofautishwa kati ya:
  • Kutaka mabadiliko kwa amani (halali)
  • Kutishia kutumia nguvu (kinyume cha sheria).

Hitimisho:
Ikiwa Tundu Lissu na wafuasi wake watatumia njia za vurugu au kuchochea machafuko, wanaweza kukabiliwa na hatua za kisheria. Msajili wa Vyama vya Siasa ataweza kuchukua hatua ikiwa chama kitakiuka masharti ya kisheria. Hata hivyo, mazungumzo ya mabadiliko kwa njia za amani yanaweza kuendelea kwa kuzingatia Kanuni za Katiba.
Umma wa watanzania wakiamua hakuna wa kuwazuia hivyo ondoa uharo wako ulioharisha hapa.
 
Katika andiko lote ulilo wasilisha, sikuona popote unapo wahimiza CCM na vyombo vyake vyote kufuata sheria katika chaguzi zote; na wala huzungumzi chochote juu ya HAKI za wananchi kuwachagua viongozi wanaowataka bila ya kuvurugwa na CCM na vyombo vya dola!
Hayo mazungumzo unayo yasema hapa yatakuwa ni ya nini iwapo kwa maoni yenu sheria zote za uchaguzi zinafuatwa bila ya upendeleo wowote?
You are right mkuu hapa nilijikita kuonyesha tu kuwa kama ikitokea kweli Tundu na watu wake wakafanya uasi kama wanavyojitapa, ni nini kitatokea.

All in all nathamini mchango wako kwenye hoja ya CCM ambavyo imekuwa inasimamia uchaguzi na kudhulumu haki za watu za kuchagua viongozi wao.
 
Ni sawa ila kwanini serikali ya ccm isifanye hayo mabadiliko kwenye Sheria za uchaguzi Ili kuepusha hayo unayosema! Wewe unaona ni sawa kushiriki uchaguzi wkt wasimamizi wote wa uchaguzi ni makada na wateuliwa wa Rais ambaye ni mwenyekiti wa ccm huku akiwa naye ni mgombea!? Kitakuwa na haki hapo!?
Siyo sawa. Hili halibishaniki
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na sheria za nchi, uchaguzi ni msingi wa demokrasia na haki ya kikatiba (Kwa mfano, Katiba ya Tanzania ya 1977, Kifungu cha 5 na 21).

Kutoa vitisho vya "kuharibu uchaguzi" au kuanzisha "uasi" ni uvunjifu wa sheria za Tanzania, kama vile:
(1) Kanuni ya Jinai (Penal Code): Vifungu namba 38 (kuchochea fujo- sedition), 40 (kuchochea machafuko-inciting unrest), au 41 (kuashiria kusudi la kuvunja utulivu wa umma-conspiracies to breach public peace) vinaweza kutumika kuwashitaki wanaotangaza mambo hayo.

(2) Sheria za Usalama wa Taifa: Kuchochea uasi kunaweza kuchukuliwa kama udhalilishaji wa mamlaka ya Serikali, na kusababisha kukamatwa, mashtaka, na hukumu ya jela ikiwa wata patikana na hatia.

(3) Msajili wa Vyama vya Siasa, Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa (Namba 5 ya 1992), ana wajibu wa kuhakikisha vyama vinazingatia Katiba na sheria za nchi. Ikiwa chama au wanachama wake kinatangaza mambo yanayokiuka Katiba (kama vile kukataa uchaguzi kwa njia za vurugu), Msajili anaweza:
  • Kutoa onyo la kisheria
  • Kufuta chama kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Kifungu cha 11(2)(e), ikiwa kinaendelea kukiuka masharti ya kikatiba.

ANGALIZO:-
Hata hivyo, haki ya kukosoa na kuomba mabadiliko kwa njia za amani ni haki za kikatiba (Kifungu cha 18 na 20). Hivyo, msimamo wa Tundu Lissu unahitaji kutofautishwa kati ya:
  • Kutaka mabadiliko kwa amani (halali)
  • Kutishia kutumia nguvu (kinyume cha sheria).

Hitimisho:
Ikiwa Tundu Lissu na wafuasi wake watatumia njia za vurugu au kuchochea machafuko, wanaweza kukabiliwa na hatua za kisheria. Msajili wa Vyama vya Siasa ataweza kuchukua hatua ikiwa chama kitakiuka masharti ya kisheria. Hata hivyo, mazungumzo ya mabadiliko kwa njia za amani yanaweza kuendelea kwa kuzingatia Kanuni za Katiba.
Ccm na serekali yake wakubali tu kufanya hizo reform kwani si ni kwa ajili ya vyama vyote. Ccm na serekali wanajua kabisa bila hila hawawezi kashinda kwenye Sanduku la kura...
Acha Mh Lissu awanyooshe.
 
Chaguzi za mwaka jana za S/Mitaa nazo zilikuwa na hangover ya yale yaliyotokea kipindi cha 2019/20.

Ila haya mambo yanaongeleka, siyo ya kupeleka wananchi barabarani
Kwani "kuongeleka" unako kuzungumzia nani anakupiga chenga, au hujui? Kwani mambo haya yameanza na CHADEMA ya Tundu Lissu au ACT-Wazalendo jana?
Sasa ifahamike kwamba, endapo ulaghai wa mazungumzo unatumiwa kupoza na kuendelea na ubovu uleule wa hiyo miaka uliyo itaja, ulaghai huo unakataliwa.
Onyesha dhati ya kutaka mabadiliko ya kweli, yatakayo liinua taifa zima, na sio ujanja ujanja wa kuiendeleza CCM madarakani.
 
Katiba hiyo hiyo ya mwaka 1977 iliheshimiwa hata na JKN mwenyewe. Na amini hata waliomfuata akina AHM, Mkapa na Kikwete waliiiheshimu.

Tatizo lilianza mwaka 2020 na Magufuli aliyetaka mpaka kujiongezea muda wa kutawala, lakini Mungu akatusaidia kumuondoa duniani.

Chaguzi za mwaka jana za S/Mitaa nazo zilikuwa na hangover ya yale yaliyotokea kipindi cha 2019/20.

Ila haya mambo yanaongeleka, siyo ya kupeleka wananchi barabarani
Jecha ni wa kipindi kipi
 
Ungeongelea hatua zinazochukuliwa chama kinapobainika kuiba kura na kunahisi uchaguzi,

Halafu we kijana ufahamu kuwa, Baba wa familia Leo akiamua kutoa AMRI kuwa
" Pasipikwe chochote Leo nyumba hii, Amri hiyo inatekelezwa bila swali lolote."

Na baba wa familia hiyo SI Lisu wala serikali ya ccm, baba ni " Wananchi wa Tanzania".

Wananchi wako juu ya katiba,

Wananchi ndio wenye mamlaka ya kuzuia uchaguzi.
 
Hakuna sheria unayoijua wewe isipokuwa umeshiba viazi na mihogo.
Mleta mada ni mjinga, mtupu kabisa wa masuala ya sheria na katiba.

Hajui kuwa katiba inasisitiza uwepo wa uchaguzi huru na haki. Tunatakiwa kupambana kulinda katiba. Viongozi wa CHADEMA ni wazalendo wa kweli wanaopambana kulinda katiba dhidi ya manyang'au wanaovunja katiba na kupora mamlaka ya wananchi.
 
Ajuwe Tanzania haiwezi kuchezewa kama jamhuri za ndizi. Ajiandae kupambana na matokeo. Nimemuwekea options zote kwenye post #1
Post #1 inawahusu zaidi wasio na passport kuliko TAL, wajue kabisa ili wakiamua waamue wakijua wameamua kwa option za matokeo wanayoelewa.
 
Katiba ambayo hairuhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani

Back
Top Bottom