No Reforms No Elections: Kama kweli itatokea ni nini kitawakabili Lissu na CHADEMA

No Reforms No Elections: Kama kweli itatokea ni nini kitawakabili Lissu na CHADEMA

Hakuna Watanzania wa hivyo. 99% wako busy na kupambania uchumi wapate kipato cha kuendesha maisha yao.
Nakubaliana na wewe. Na CCM inalijua hili fika na inalitumia kikamilifu i.e wanajua kabisa watanzania wengi ni mafukara, kukicha wanaamka kuhemea kama kuku wa kienyeji na hawana muda wa kufuatilia uwajibikaji wa serikali. Na pia wengi wanadhani ufukara wao ni majaliwa ya Mungu. Watu wa aina hii ni hatari sana na ndiyo maana nikasema kuna siku kila mtu atashangaa.
 
Hakuna jipya chini ya jua.

Lissu hatokuwa mwanasiasa wa kwanzq kupewa kesi yoyote ya jinai kama ya uhaini.

Miaka ya 90 NCCR ikiwa ya moto bara na CUF ikiwa ya moto Visiwani wanasiasa kadhaa walipewa kesi ya uhaini kwa hila za serikali ya ccm
Kwa hiyo unategemea kupewa kesi ya uhaini kwa Lissu ndiyo ufanikishe maisha yako? Utasubiri sana
 
TAL alisema ni uasi wanajiandaa kuufanya maana hakuna namna.
Damu za wananchi zinamwagika kila uchaguzi, kura feki na wizi wa kura. Kukataa haya ndipo penye uasi. Kwa wanachofanya CHADEMA ni kujadili namna ya kuwa na Uchaguzi wa haki pasipo mauaji,ni engagement kwa kila mtu hata wewe.Katiba ya 1977,ibara ya 18 na 20 na mamlaka ya wananchi ibara ya 8,hata Mwalimu Nyerere alitoa tamko la kisiasa la Azimio la Arusha kwamba,Tumeonewa kiasi cha kutosha,Tumenyonywa kiasi cha kutosha. Sasa CHADEMA inatoa tamko lake kwamba,NO REFORMS NO ELECTION 2025.
 
Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na sheria za nchi, uchaguzi ni msingi wa demokrasia na haki ya kikatiba (Kwa mfano, Katiba ya Tanzania ya 1977, Kifungu cha 5 na 21).

Kutoa vitisho vya "kuharibu uchaguzi" au kuanzisha "uasi" ni uvunjifu wa sheria za Tanzania, kama vile:
(1) Kanuni ya Jinai (Penal Code): Vifungu namba 38 (kuchochea fujo- sedition), 40 (kuchochea machafuko-inciting unrest), au 41 (kuashiria kusudi la kuvunja utulivu wa umma-conspiracies to breach public peace) vinaweza kutumika kuwashitaki wanaotangaza mambo hayo.

(2) Sheria za Usalama wa Taifa: Kuchochea uasi kunaweza kuchukuliwa kama udhalilishaji wa mamlaka ya Serikali, na kusababisha kukamatwa, mashtaka, na hukumu ya jela ikiwa wata patikana na hatia.

(3) Msajili wa Vyama vya Siasa, Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa (Namba 5 ya 1992), ana wajibu wa kuhakikisha vyama vinazingatia Katiba na sheria za nchi. Ikiwa chama au wanachama wake kinatangaza mambo yanayokiuka Katiba (kama vile kukataa uchaguzi kwa njia za vurugu), Msajili anaweza:
  • Kutoa onyo la kisheria
  • Kufuta chama kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Kifungu cha 11(2)(e), ikiwa kinaendelea kukiuka masharti ya kikatiba.

ANGALIZO:-
Hata hivyo, haki ya kukosoa na kuomba mabadiliko kwa njia za amani ni haki za kikatiba (Kifungu cha 18 na 20). Hivyo, msimamo wa Tundu Lissu unahitaji kutofautishwa kati ya:
  • Kutaka mabadiliko kwa amani (halali)
  • Kutishia kutumia nguvu (kinyume cha sheria).

Hitimisho:
Ikiwa Tundu Lissu na wafuasi wake watatumia njia za vurugu au kuchochea machafuko, wanaweza kukabiliwa na hatua za kisheria. Msajili wa Vyama vya Siasa ataweza kuchukua hatua ikiwa chama kitakiuka masharti ya kisheria. Hata hivyo, mazungumzo ya mabadiliko kwa njia za amani yanaweza kuendelea kwa kuzingatia Kanuni za Katiba.

Pale HAKI inaposhindikana kupatikana kwa njia za amani na za Kidemokrasia, basi Vita huwa inakuwa ndio silaha ya mwisho kabisa katika kupatikana kwa hiyo HAKI. Hakuna njia nyingine yoyote mbadala zaidi ya hiyo.

Mwanafalsafa Jeffs O'Brien aliwahi kusema kwamba "Njia pekee ambayo Wananchi wataitumia katika kuzungumza au kujadiliana na Watawala wao ambao ni Madikteta ili kufikia muafaka wenye maslahi kwa pande zote mbili ni kwa KUPITIA MTUTU WA BUNDUKI."

[Ufafanuzi umeongezwa]


Mfano mzuri zaidi uliotokea siku za hivi karibuni kuhusiana na masuala kama haya ni kule nchini DRC, katika Mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.
Kutokana na kukosekana kwa HAKI, Watu/Wapiganaji wa M23 walikuwa wanaomba mazungumzo na Utawala wa nchi yao hiyo kwa muda mrefu Sana (tangu zamani miaka ya 2012) lakini bila mafanikio yoyote yale. Utawala wa nchi hiyo ya DRC daima ulikuwa unakataa kukutana na hao watu wa M23. Lakini mara tu Wapiganaji hao wa M23 walipoanzisha vurumai dhidi ya Utawala wao, mara moja Rais wa nchi hiyo ya DRC sasa amekubali kukutana na Watu wa M23 ili wazungumze na kumaliza tofaufi zao.
Je, unafikiri mazungumzo hayo kati ya M23 na Rais wa DRC Felix Tsishekedi yangewezekana kufanyika endapo kama Watu wa M23 wasingechukua maamuzi magumu na hatua kali kama hizo walizochukua huko Goma na Bukavu? Ingewezekana kweli?
 
Damu za wananchi zinamwagika kila uchaguzi, kura feki na wizi wa kura. Kukataa haya ndipo penye uasi. Kwa wanachofanya CHADEMA ni kujadili namna ya kuwa na Uchaguzi wa haki pasipo mauaji,ni engagement kwa kila mtu hata wewe.Katiba ya 1977,ibara ya 18 na 20 na mamlaka ya wananchi ibara ya 8,hata Mwalimu Nyerere alitoa tamko la kisiasa la Azimio la Arusha kwamba,Tumeonewa kiasi cha kutosha,Tumenyonywa kiasi cha kutosha. Sasa CHADEMA inatoa tamko lake kwamba,NO REFORMS NO ELECTION 2025.
Upo tayari kuikabili polisi mkuu? Wenyewe weshasema wamejipanga.
 
Nini polisi? Itaandikwa historia nyingine,kama rekodi huvunjwa na polisi wanapojipanga ni ili historia iandikwe.
Jibu kama shujaa mkuu, Upo tayari kuikabili polisi? Jibu ndio, mimi xxx..nitaikabili polisi kwa kuzuia uchaguzi.
 
Wewe una kichaa, kama hujui kusoma na kutafakari hilo ni kosa la wazazi wako
Wazazi wako wewe wamekusaidia nini zaidi ya kuwa shabbiki wa harakati za Chiba aka Tundu?
 
Jibu kama shujaa mkuu, Upo tayari kuikabili polisi? Jibu ndio, mimi xxx..nitaikabili polisi kwa kuzuia uchaguzi.
Hao hawajipangi kama mmoja,uliza,sisi wananchi? We vipi mbona upo toxic hivyo?
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Naandika majina ya mashujaa wa keyboard mkuu ili next time wapuuzwe.
Wakala wa wasiojulikana,sema kweli yako kama umeongezwa sh.ngapi? Wewe unakula bila kwenda VETA kwa degree uliyonayo ila chawa hatumii keyboard hupenda uchafu.
 
TUTAFUTA CHAMA CHENU CHA KIGAIDI UNAWEZAJE KUVUNJA KATIBA UACHWE HIVYOHIVYO?MMTAHENYA
Nasikia Tundu Lissu atapandishwa kizimbani kwa kesi isiyiyo na dhamana. REJEA post yangu Namba 1 hapa
 
Back
Top Bottom