No way Out, Matokeo ya kushangaza Leo katika gemu ya Almelekh vs Simba sc

Do or die kwa wenyeji ili kufufua matumaini yao japo game ngumu sana.....kwa kubet....unarisk kwa kumpa mwenyeji win.......or under 3goals or HT 0-0 or under 2goals
 
Kila la heri Simba Mnyama
 
Mkumbushe tushawapiga haohao melekh kwao 2 bila kabla ya half time wakatupiga mawe mechi iakavunjika wakakataa kutupa ushindi wakasema mechi irudiwe Simba wakajitoa ilikuwa robo fainal ya afrika mashariki na kati

Wewe unafikiri mtapoteza kwa kucheza fair game,hapana,waarabu hawatawaruhusu mcheze fair game,fitina mwanzo mwisho,hii game mmeshinda sana droo au mnapigwa kimoja ndiyo nitoleee
 
Mkumbushe tushawapiga haohao melekh kwao 2 bila kabla ya half time wakatupiga mawe mechi ikavunjika wakakataa kutupa ushindi wakasema mechi irudiwe Simba wakajitoa ilikuwa robo fainal ya afrika mashariki na kati
Baada ya hapo tukakutana kwenye kombe la caf tukawatoa hivi vitoto vilivyoanza kushabikia mpira enzi za manji ni shida
 
Said Swedy Scud
 
Simba leo hawataamini.Atapigwa si chini ya goli 4, baada ya mechi mtakumbuka hii post
 
Huu na nafikiri ni uzi maalumu kwa ajili ya mashabiki wa Kidimbwi fc ili kujipoza machungu.
Wameamua kujipa raha wenyewe
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wewe unafikiri mtapoteza kwa kucheza fair game,hapana,waarabu hawatawaruhusu mcheze fair game,fitina mwanzo mwisho,hii game mmeshinda sana droo au mnapigwa kimoja ndiyo nitoleee
3.30 hrs to go tusubiri muda utupatie majibu
 
Sisi Simba tunakubali matokeo yote matatu katika mpira.
Nawewe cheza Club bingwa Afrika na usifungwe.
Kafungwa bingwa mtetezi Al-Ahaly sembuse Simba.
 
Said Swedy Scud
Huyu jamaa sijui alipotelea wapi walitengeneza Partnership matata sana na Abed Mulenga japo ilikuwa ya muda mfupi na katika kucheza kwao walicheza mechi saba tu wakiwa pamoja na zote walifunga magoli.
Game yao ya kwanza ilikuwa Kenya kwenye michuano ya Tusker Abed akatupia 2 assist kutoka kwa Scud.
Abed akaondoka kurudi kwao Congo.
Msimu uliofuata walicheza na Asante Kotoko hapa hapa Dar kotoko akafa nne Abed akifunga mbili na Said moja.

Wakaingia michuano ya Kagame game dhidi ya Al Hilal ilikuwa funga kazi walipoichapa goli 6 bila Mulenga akiingia kambani mara mbili kwa assist za Said Swedy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…