mng'ato
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 29,200
- 49,076
Point yako ya mwisho sikubaliani nayo. Nunua mashine ya kufanya diagnosis, halafu ikiwaka check engine, ichomeke na usome uone tatizo nini (haihitaji uwe fundi kufanya diagnosis). ukishajua, mpelekee fundi wa kitaa tu wa kawaida, halafu mwambie akutengezee jambo flani (kwa mujibu wa kodi uliopata). Atakutengenezea tu na itakuwa fresh...
Hoja yako naipinga,ni vizuri kupeleka gari kwa competent mechanics mwenye diagnos tools, though mwenye gari kua na OBD-2 yake mwenyewe ni kitu kizuri lkn nakuhakikisha wewe kama ni layman kwny hio field utaenda chaka sana tu na utanunua spare mpya kwa sana tu.
Kwa mfano OBD-2 reader yako ikisoma codes P0171 (Lean Exhaust Bank 1) na P0174 (Lean Exhaust Bank 2) utakimbilia kunua Oxygen Sensors wkt unaweza kukuta kuna vacuum leak na possibly haujabadilisha Fuelt filter kwa muda mrefu saana,unanunua zako fuel filter mpya mchezo umeisha wkt sababu ulisoma codes mwenyewe bila kua na utaalam husika ungenunua Oxygen Sensors.
Unaweza kusoma codes za P0401(insuficcient EGR) ukakimbilia fasta kununua EGR Valve mpya wkt inaweza kua ni EGR control solenoids au sababu ni exhaust hose imepasuka.
So ni vizuri kupeleka gari kwa wataalam husika.