Mleta mada pole sana..
Huku Jf utapata ushauri mseto mpaka kichwa kitauma. Kuna jamaa huko juu kasema sijui itakuwa oil. Mwingine kasema charging system...
Matatizo ya gari kuleta miss husababishwa na mambo kadhaa. Tukianza na yale marahisi kwenda magumu..
1.Spark plugs...huenda moja wapo imekufa.
2. Vacuum hoses...Kuna vipipe vidogo vidogo vinavyohusiana na hewa, kakiwa kametoboka au kamechomoka unaweza kupata miss na check engine light. Mfano kuna vacuum hose moja huwa inatoka pale kwenye cylinder head cover inaingia kwenye hose kubwa kati ya throttle body na MAF sensor...hii ikiwa na tobo au ikilegea kwa magari mengi utaona miss na check engine..
3. Ignition coil....Hapa huenda zile rubber boots za coil zinazoshuka kwenye spark plugs zimemetoboka...hizi hukakamaa kutokana na joto kubwa la engine na kutoboka au kupasuka....sehemu iliyotoboka itakuwa inavujisha umeme unaotakiwa uende kuchoma spark plug na umeme huo hupotelea kwenye block engine.....hapo utapata miss isiyoisha ila ukipiga resi rmp iwe kweny 4 mpaka 5 miss inapotea..
4. Fuel filter, air filter au throttle body huenda vimechafuka sana.
5..MAF au O2 sensors...huenda moja wapo ina loose connection au imechafua sana au ndiyo inaenda kufa kabisaaa.
6.Fuel injectors huenda zimekuwa clogged zinahitaji kusafishwa...
Kama maeneo yote hayo yamekaguliwa na hayana shida., fanya vipimo vya mashine....huenda control box imepata COVID 19.
Ukifuatilia haya, utapata suluhisho. Kwa fundi mjuvi, hako katatizo wala hatahitaji diagnosis machine..
Sent using
Jamii Forums mobile app