Ukiondoa Thermostat kuna case mbili. kama radiator fan ni mbovu basi engine lazima itaoverhit. Ila kama radiator fan inazunguka basi engine itakuwa inaoperate katika temperature ambayo iko below ile inayotakiwa na hapa huwa zinakuwepo athari kwenye utumiaji wa mafuta na pia kwenye Lubricant.
Kuna gari zinategemea Thermostat kupeleka signal kwenda kwenye ECU na kuwasha fan. Ukiiondoa Thermostat completely kwa gari yenye mfumo huo, basi ita overheat tu. Nilikuwa kwenye foleni nikaona temperature inapanda, nikahisi labda maji yamepungua feni itawaka since tayari ime sense kuwa temperature ni too high, nikaona kimya, nikaweka gari pembeni, nikahisi feni mbovu, nikawasha AC feni zote zinazunguka, nikajua sio feni. Nikazima gari, na kuchezea chezea kama kushindilia pale inapokaa switch ya thermostat, nikawasha gari, ikapata moto, mara naona feni inazunguka.
That is to say, for a car ambayo inategemea switch ya thermostat kuwasha feni, engine ita overheat, kwa sababu feni haitofanya kazi, na yale maji hayatopoozwa na kurudishwa kwenye engine yakiwa moto.
Kila Engine ina operating temperature yake na ili iwe inafanya kazi inavotakiwa basi ifikie joto linalotakiwa.
Kwenye Cold start, ECU inajua kama engine ipo baridi au moto kupiti Temperature sensor. So when it is cold, the engine needs to be n normal operating temperature, to get there, higher explosions is needed, and to get higher explosion is to add more fuel.
Cold start process, ni simply to get the engine to its normal running temp. Na sio kwa sababu mafuta yapo baridi, Petrol inapata ubaridi gani hapa TZ hata iwe baridi? Ile yote hutokea kwa sababu ECU inapata cold readings na inataka ipate warm readings ili ifanye kazi vyema.
Kuthibitisha hilo sasa, ETC sensor ikiwa imefeli na default ni cold, maanake ECU inajua engine iko baridi, itatia more fuel ili ipate moto, lakini kwa sababu sensor imefeli, hata baada ya engine kupata moto (na tujaalie hayo mafuta yamepata moto) bado cycle iko pale pale, more fuel into the engine. And by the way, ETC sensor haipimi Fuel temperature, vipi utasema kuwa Inapeleka more fuel kwa sababuthe fuel is cold?