kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Rais Mama Samia akiendelea hivihivi na juhudi za kujali hali za wananchi wa kawaida na kukuza demokrasia nchini lazima atapata mojawapo ya zawadi za amani za Nobel au Mo Ibrahim, Inshallah.
Watu wanasema ukimsifu sana mgema anaweza kulitia maji tembo, lakini kwa mama Samia mimi ni miongoni mwa watu wa kawaida kabisa kwenye jamii wanaoiona nia yake njema kwa wananchi na Tanzania.
Kama sisi tutashindwa kumuona na kuona anachokifanya huenda watu wa mataifa mengine wakamuona na kumpa kumpongeza.
Namuombea kwa Mungu asilitie tembo maji nchi ielekee kule waliko watu wastaarabu.
Aifikishe Tanzania mahali ambapo Watanzania wanaweza kuongozwa na chama chochote kile, kukiondoa na kukirudisha tena madarakani bila tatizo wala shida yoyote.
Yaani aondoe janjajanja za kisiana ambazo huko mbele ya safari italiletea shida kubwa taifa.
Ahakikishe kuwa hakuna hata tone moja la maji ya mito, mvua na maziwa yanakwenda baharini kabla Watanzania wote kupatiwa maji safi.
Lazima zawadi ya Nobel itakuja Tanzania, inshallah.