Nobel Prize inamnyemelea Rais Samia

Nobel Prize inamnyemelea Rais Samia

Rais Mama Samia akiendelea hivihivi na juhudi za kujali hali za wananchi wa kawaida na kukuza demokrasia nchini lazima atapata mojawapo ya zawadi za amani za Nobel au Mo Ibrahim, Inshallah.

Watu wanasema ukimsifu sana mgema anaweza kulitia maji tembo, lakini kwa mama Samia mimi ni miongoni mwa watu wa kawaida kabisa kwenye jamii wanaoiona nia yake njema kwa wananchi na Tanzania.

Kama sisi tutashindwa kumuona na kuona anachokifanya huenda watu wa mataifa mengine wakamuona na kumpa kumpongeza.

Namuombea kwa Mungu asilitie tembo maji nchi ielekee kule waliko watu wastaarabu.

Aifikishe Tanzania mahali ambapo Watanzania wanaweza kuongozwa na chama chochote kile, kukiondoa na kukirudisha tena madarakani bila tatizo wala shida yoyote.

Yaani aondoe janjajanja za kisiana ambazo huko mbele ya safari italiletea shida kubwa taifa.

Ahakikishe kuwa hakuna hata tone moja la maji ya mito, mvua na maziwa yanakwenda baharini kabla Watanzania wote kupatiwa maji safi.

Lazima zawadi ya Nobel itakuja Tanzania, inshallah.
Inaonekana hata hiyo nobel prize hujui maana yake
 
Kama hilo liko kwenye urefu wa kamba yake hamna kesi
ni nani hali kwenye urefu wa kamba yake?

Hata machinga anakula kwenye urefu wa kamba yake kwanjia ya kutolipa kodi, kutumia njia za waenda kwa miguu na kupanga bidhaa chini kwenye mavumbi na watu wananunua, bar maid anapewa tips, polisi traffic wanapata hela za dawa ya viatu, wafanyakazi wanakula rushwa, muda wa mwajiri na kuchomoa vitendea kazi, semina na workshops, mwl anauza karanga, anachotewa maji, nk hakimu ndo usiseme, dereva anakula anapunguza mafuta na matengenezo feki ya gari, nk
 
Inaonekana hata hiyo nobel prize hujui maana yake
kazi yako ni kutega sikio tu muda ukifika.

Urais wa Samia unatoka kwa Mungu, sio ule wa kupiga pushups tuliouzoea majukwaani, aliyenacho anaongezewa
 
kazi yako ni kutega sikio tu muda ukifika. Urais wa Samia unatoka kwa Mungu, sio ule wa kupiga pushups tuliouzoea majukwaani, aliyenacho anaongezewa
Mungu yupi huyo, labda wa kijijini kwenu
 
Suala ya katiba mpya siyo lake wala halimhusu bali ni la wenye nchi ambao ni wananchi.Yeye Samia yupo chini ya wenye nchi ambao ni wananchi kwa hiyo hana nguvu wala uwezo wa kukataa maagizo ya maboss wake ambao ni wananchi.
Hee, hivi ndivyo vinavyosababisha watu waseme elimu yetu imeshuka,

Nchi ilipata uhuru miaka 60 iliyopita, muungano una miaka 58 hivi, mbona katiba mpya haikuandikwa na wananchi tupo?
 
Kwani iyo nobel sifa zake ni zipi? maana mabeberu mpaka wakupe umewakuna haswa...
 
Ni mapema mno. Sasa ni mwaka 1 kati ya 4 na labda 1 kati ya 9, Hatujavuka hata nusu!
 
Anajali hali gani ili hali bidhaa muhimu zinapanda bei kila siku na hakuna lolote anafanya.
 
Rais Mama Samia akiendelea hivihivi na juhudi za kujali hali za wananchi wa kawaida na kukuza demokrasia nchini lazima atapata mojawapo ya zawadi za amani za Nobel au Mo Ibrahim, Inshallah.

Watu wanasema ukimsifu sana mgema anaweza kulitia maji tembo, lakini kwa mama Samia mimi ni miongoni mwa watu wa kawaida kabisa kwenye jamii wanaoiona nia yake njema kwa wananchi na Tanzania.

Kama sisi tutashindwa kumuona na kuona anachokifanya huenda watu wa mataifa mengine wakamuona na kumpa kumpongeza.

Namuombea kwa Mungu asilitie tembo maji nchi ielekee kule waliko watu wastaarabu.

Aifikishe Tanzania mahali ambapo Watanzania wanaweza kuongozwa na chama chochote kile, kukiondoa na kukirudisha tena madarakani bila tatizo wala shida yoyote.

Yaani aondoe janjajanja za kisiana ambazo huko mbele ya safari italiletea shida kubwa taifa.

Ahakikishe kuwa hakuna hata tone moja la maji ya mito, mvua na maziwa yanakwenda baharini kabla Watanzania wote kupatiwa maji safi.

Lazima zawadi ya Nobel itakuja Tanzania, inshallah.
Sijaelewa vizuri lengo la mada yako LAKINI nakupa heshima kubwa kwa mawazo makuu uliyotoa katika hizo aya mbili nilizobainisha kwa bold na red. Those are great notions for any knowledgeable and serious Tanzanian.

Kwanza ndipo ukamilifu wa demokrasia nchini utakapokuwa umefikiwa badala ya huu ushabiki wa kijinga unaoendelea wa watu na vyama. Hizi personality cult worships tunazoendekeza zinaonyesha jinsi tulivyo primitive.

Pili katika uzoefu wangu mrefu katika nchi za sahel zinazoishi kwa kilimo cha umwagiliaji pekee na middle east imeniwia tabu sana kuelewa jinsi uhaba wa maji unavyoendelea kuathiri maisha ya watanzania kiasi cha kuacha wengi wakiishi kijima.

Nchi iliyokithiri kwa maziwa makubwa na mito mikubwa inayovurumisha mabilioni ya lita za maji kuelekea baharini. Mvua isiponyesha msimu mmoja ni janga. Gharama ya kukusanya maji hayo (conservation) haishindikani bali uzembe, kukosekana mikakati ya muda mrefu, vipaumbele sahihi na ufujaji wa pesa za umma vinafanya miradi muhimu kama hii kutofikiriwa. Badala yake ni propaganda kuhusu maji bila mabadiliko ya msingi ndio zimetawala tangu uhuru.
 
Ni mapema mno. Sasa ni mwaka 1 kati ya 4 na labda 1 kati ya 9, Hatujavuka hata nusu!
Key word hapa ni "nyemelea" kunyemelea sio kupata, bado ana kazi ya kutosha ya kufanya kabla mabwenyenye hawajamfikiria. Lakini kwa mwendo huu I can see a light at the end of the tunnel. Kule kijijini kwetu ambako tangu uhuru hakukuwa na maji wala umeme sasa kazi inaendelea kupeleka maji na umeme. Kila mtu anachekelea kuona nguzo zinasimikwa na mtaro unachimbwa. Hao watu wana shauku kubwa ya kuona maji yamefika na umeme unawaka kwao kwa mara ya kwanza tangu miaka 60 ya uhuru ya watoto kusomea vibatali. Ukiwaambia eti miradi itachelewa kidogo kwa sababu pesa imekwenda kwenye kuandika katiba mpya watakuona chizi.

Tatizo letu ni kwamba nchi yetu ilijengwa zaidi upande mmoja kuliko pande nyingine hivyo kusababisha watu leo kuwa na level mbalimbali za maendeleo na mahitaji. ndio maana unaona ni watu wa kanda moja tu na mijini ndio wanadai zaidi katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Ndiyo maana mfano wananchi nchi wa Singida hawajaandamana wakaki mtoto wao Lisu amepigwa risasi kijingajinga mchana kweupe kwakuwa Lisu alikuwa hahangaiki na mahitaji ya msingi ya watu wa Singida, Alipofariki Mh Filikunjombe uliona watu wa kwao walivyolia na kusaga meno kwakuwa mbunge wao alikuwa anayafanya yale yanayowasibu.
 
Hee, hivi ndivyo vinavyosababisha watu waseme elimu yetu imeshuka,

Nchi ilipata uhuru miaka 60 iliyopita, muungano una miaka 58 hivi, mbona katiba mpya haikuandikwa na wananchi tupo?
Kama wananchi mpo na katiba mpya haijaandikwa ni uzembe wenu.

Kwa hiyo unataka kuficha uzembe wako kwenye mgongo fake wa kulazimisha kuwa Rais ni boss wa wananchi wakati ukweli ni kwamba boss ni wananchi na Rais ni mwajiriwa wa wananchi na kazi yake ni kutumwa na kuagizwa na wananchi?!
 
Rais Mama Samia akiendelea hivihivi na juhudi za kujali hali za wananchi wa kawaida na kukuza demokrasia nchini lazima atapata mojawapo ya zawadi za amani za Nobel au Mo Ibrahim, Inshallah.

Watu wanasema ukimsifu sana mgema anaweza kulitia maji tembo, lakini kwa mama Samia mimi ni miongoni mwa watu wa kawaida kabisa kwenye jamii wanaoiona nia yake njema kwa wananchi na Tanzania.

Kama sisi tutashindwa kumuona na kuona anachokifanya huenda watu wa mataifa mengine wakamuona na kumpa kumpongeza.

Namuombea kwa Mungu asilitie tembo maji nchi ielekee kule waliko watu wastaarabu.

Aifikishe Tanzania mahali ambapo Watanzania wanaweza kuongozwa na chama chochote kile, kukiondoa na kukirudisha tena madarakani bila tatizo wala shida yoyote.

Yaani aondoe janjajanja za kisiana ambazo huko mbele ya safari italiletea shida kubwa taifa.

Ahakikishe kuwa hakuna hata tone moja la maji ya mito, mvua na maziwa yanakwenda baharini kabla Watanzania wote kupatiwa maji safi.

Lazima zawadi ya Nobel itakuja Tanzania, inshallah.
In shaa Allah 🙏

#Siempre SSH👍
 
si Kuna checks and balance ya CAG, PCCB, Polisi, Mahakama, internal auditors, wahasibu, bunge?

wakila tutawajua na hatua kuchukuliwa. Mlimuelewa vibaya
Vyote ulivyotaja havipo Tanzania kutokana na katiba fake tuliyonayo.

Kwa katiba tuliyonayo Mahakama,Bunge na kadhalika ni vyombo vya Rais kutoka chama tawala vinavyomuwezesha kutawala bila ridhaa ya wenye nchi na wala siyo kwa ajili ya check and balance kama unavyojinasibu.
 
Sijaelewa vizuri lengo la mada yako LAKINI nakupa heshima kubwa kwa mawazo makuu uliyotoa katika hizo aya mbili nilizobainisha kwa bold na red. Those are great notions for any knowledgeable and serious Tanzanian.

Kwanza ndipo ukamilifu wa demokrasia nchini utakapokuwa umefikiwa badala ya huu ushabiki wa kijinga unaoendelea wa watu na vyama. Hizi personality cult worships tunazoendekeza zinaonyesha jinsi tulivyo primitive.

Pili katika uzoefu wangu mrefu katika nchi za sahel zinazoishi kwa kilimo cha umwagiliaji pekee na middle east imeniwia tabu sana kuelewa jinsi uhaba wa maji unavyoendelea kuathiri maisha ya watanzania kiasi cha kuacha wengi wakiishi kijima.

Nchi iliyokithiri kwa maziwa makubwa na mito mikubwa inayovurumisha mabilioni ya lita za maji kuelekea baharini. Mvua isiponyesha msimu mmoja ni janga. Gharama ya kukusanya maji hayo (conservation) haishindikani bali uzembe, kukosekana mikakati ya muda mrefu, vipaumbele sahihi na ufujaji wa pesa za umma vinafanya miradi muhimu kama hii kutofikiriwa. Badala yake ni propaganda kuhusu maji bila mabadiliko ya msingi ndio zimetawala tangu uhuru.
Tangu uhuru hakuna bajeti wala ilani ya uchaguzi isiyotaja kupeleka maji kwa wananchi lakini miaka 60 ya uhuru ni sehemu chake sana za viongozi wakora waliotuumia nafasi zao vibaya kupeleka umeme na maji kwenye majimbo na kanda zao na kuyaacha maji yote ya mvua na mito yakienda baharini. Katiba mpya kwangu ni muhimu lakini sio muhimu sana leo kuzidi maji, umeme, chakula na afya kwa watanzania wote. Kama Rais atasema wacha tutumie kila senti yetu kwa miaka 10 kuhakikisha kuwa kila kitongoji kinapata maji na umeme, kila kijiji kina shule na zahanati na barabara inayopitika kwa mwaka mzima, kila kata ina sekondari, kituo cha afya, kituo cha polisi na mahakama ya mwanzo na miradi ya kimkakati inamalizika mimi niko tayari kumuunga mkono na kumpigia kampeni nchi nzima bila malipo.

Tumeibiwa sana na hela zetu zimechezewa sana na viongozi wetu bila idhini yetu, pesa zetu nyingi zimetumika kuendesha siasa za ndani na nje ya nchi na kuacha kutumikia matatizo ya wananchi wanaozidi kuongezeka idadi kila mwaka.
 
Rais Mama Samia akiendelea hivihivi na juhudi za kujali hali za wananchi wa kawaida na kukuza demokrasia nchini lazima atapata mojawapo ya zawadi za amani za Nobel au Mo Ibrahim, Inshallah.

Watu wanasema ukimsifu sana mgema anaweza kulitia maji tembo, lakini kwa mama Samia mimi ni miongoni mwa watu wa kawaida kabisa kwenye jamii wanaoiona nia yake njema kwa wananchi na Tanzania.

Kama sisi tutashindwa kumuona na kuona anachokifanya huenda watu wa mataifa mengine wakamuona na kumpa kumpongeza.

Namuombea kwa Mungu asilitie tembo maji nchi ielekee kule waliko watu wastaarabu.

Aifikishe Tanzania mahali ambapo Watanzania wanaweza kuongozwa na chama chochote kile, kukiondoa na kukirudisha tena madarakani bila tatizo wala shida yoyote.

Yaani aondoe janjajanja za kisiana ambazo huko mbele ya safari italiletea shida kubwa taifa.

Ahakikishe kuwa hakuna hata tone moja la maji ya mito, mvua na maziwa yanakwenda baharini kabla Watanzania wote kupatiwa maji safi.

Lazima zawadi ya Nobel itakuja Tanzania, inshallah.
Ni sawa lakini woga upo. Sababu ni kwa nia yake njema inaweza kuathiri chama chake.
So atapimwa kwa matokeo hasa kuonekana kwa haki, demokrasia na amani ya kweli bila kutia shaka yoyote. Vigezo vikitimia atatunukiwa. Haiwezi kuwa maneno matupu. Katiba natume huru vitamsaidi kutimiza azma yake.
 
Back
Top Bottom