Nomba uzoefu kwa wenye mzazi (wakike au kiume) mwenye watoto kutoka kwa wenzi zaidi ya wawili na wote wakiwa hai

Nomba uzoefu kwa wenye mzazi (wakike au kiume) mwenye watoto kutoka kwa wenzi zaidi ya wawili na wote wakiwa hai

Moronight walker

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2021
Posts
3,103
Reaction score
4,704
Habari jf.
Naomba uzoefu wenu watu wazima mlio na watoto au watoto ambao umezaliwa kwenye familia hii.

Ni zile familia ambazo Baba yako kazaa na wanawake hata 2 au zaidi ya 2 na wanawake aliozaa nao wapo hai pamoja na watoto pia. Hivi swala kama ilo kwako kama mtoto unaonaje kwenye familia hio au unamchuliaje Baba, funguka kutoka moyoni.

Au mama yako kazaa na wanaume 2 au pengine hata zaidi ya hao 2 na mwanaume aliyezaa nae yupo hai na mnamjua. Hivi kwenye familia ya namna hio kama mtoto mzazi wako unawaonaje moyoni mwako.

Pia kama wewe ni Baba au mama upo utu uzima sasa na watoto wako washakuwa wakubwa wanajitambua.

Hivi unajisikiaje maana watoto watajua tuu kuwa mama alizaa na mbaba flani na mtoto ndo huyu. Mama alizaa na wanaume zaidi ya 2 au 3.

Wewe kama mwanamke unalichukuliaje hilo swala.

Naombeni ushirikiano wa kutosho.
 
Au mama yako kaolewa na mwanaume mwingine na Baba yako kaoa mwanamke mwingine wewe upo katikati. Vipi issue kama hio wewe moyoni mwako unaonaje.

Funguka tuu kuna something nataka kulearn.
 
Pia kama
Wewe ni mwanamke upo utu uzima pia mwanaume uliyezaa nae kaoa mwanamke mwingine na wewe umeolewa na mwanaume mwingine na watoto wenu wanajua hilo kwa sababu ni watu wazima.

Hivi kama mzazi now na utu mzima huo unajisikiaje wewe kama wewe.
Funguka tuu.
 
Nilizaliwa na baba mwenye Wanawake watano. Na wakati yupo hai niliona kawaida na mwanaume kweli kweli.

Mantiki haswa ya swali lako ni lipi?
 
Hii kitu inaninatafuna ndani kwa ndani kama mtoto basi tu mengine acha nizikwe nayo.
 
Mpaka ukiwa mtu mzima ndo unaelewa ,unakuta labda kwa mother mpo watatu ila mtu na babaake.
 
Natamani kujua unateseka ukiwa wap?au unataka kufunua mashuka ya wazazi wako kuwa kwa nn ulikuwa hivo?na unaona aibu kwa watoto wako?sikia maisha yako sio ya wazazi wako na wala walivyo haikufanyi ww kutaka kujua saaana kama kuna kitu walikueleza mpaka kuwa hivyo chukulia hivyo hivyo usijifanye mdadisi hakuna mzazi malaya,nimezaliwa kwa baba ana wake 5 na ss kaoa wa 6 na ana mimba ilhali wapo wanae wakubwa mno Wana 50+ na mama akat anaolewa hapo alizaa watoto wa 2 na kila mtoto na baba yake na wapo hai.hiyo mm hainihusu kabisa cha kujifunza tunza ndoa yako na wanao.ova
 
Hii kitu inaninatafuna ndani kwa ndani kama mtoto basi tu mengine acha nizikwe nayo.
Inakutafuna wakati walio tena wapo huru?acha kujumua matatizo yasio yako,kufa na uzikwee waache walio anzisha hai
 
Inaua upendo pia uleta Hali ya aibu lakini ndio hivyo huwezi pingana na ilivyotokea Cha msingi ni kumuomba tu Mungu nawe usiwe hivyo
 
Back
Top Bottom