Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Matukio ya utekaji bado tishio nchini Tanzania kwa tukio la hivi karibuni, la kutekwa kwa Mwenyekiti wa Ngome ya vijana ya chama cha upinzani nchini Tanzania, ACT Wazalendo, Abdul Nondo ambapo kwa sasa akiwa amelazwa katika hospitali ya Agha Khan, jijini Dar es Salaam, baada ya kutekwa na kupatikana akiwa amejeruhiwa vibaya.
Nondo ameleza hali ilivyokuwa
Ilikuwa tarehe 30 novemba nilikuwa nimetokea Kigoma nikafika Dar es Salaam kwenye saa kumi alfajiri kwahiyo wakati na shughulikia usafiri ni kiwa tayari nimetoka kwenye geti la Magufuli Bus stendi, ndiyo wakatokea vijana kama sita wakanivamia wakaniambia tulia ambapo awali nilikuwa ninahisi ni vibaka.
Lakini nikaona jambo linakuwa siriazi zaidi, nikaona kuna gari limesongezwa Toyota hadtoku na milango ikiwa imefunguliwa ni nalazimishwa kungia kwenye gari. Kwahiyo mimi nilikuwa napiga kelele kupambana kuhakikisha kwamba siingii kwenye gari. Kwahiyo nikawa naomba msaada hata kwa watu wa pembeni pale nawaambia naombeni mnisaidie mimi naitwa Nondo njooni mnisaidie hakuna mtu aliyejitokeza, maana kulikuwa na bajaji pale kulikuwa na bodaboda lakini kulikuwa na watu walikuwa wanakwenye kupanda mabasi ili kusafiri kwahiyo walinizidi nguvu.
Hili tukio lilikuwa la ghafla sikuwa kabisa na fikra wala na wazo kwamba kuna mtu ananifuatilia. Watu walionikamata hawakujitambulisha wao ni wakina nani hata walipofanikiwa kuniingiza kwenye gari nilichofanikiwa kukisikia ni kwamba wakilaumia kwamba pingu zipo wapi? Baada ya kukosa pingu wakanifunga kamba kwa nguvu sana na mikono yangu walipeleka kwa nyuma ya mgongo na usoni wakanifunga kitambaa kwahiyo sikufanikiwa kuwatambua. Gari likaondoka kwa mwendo hadi likaingia sehemu likapaki wakanishusha wakanifungua kamba na wakanifunga pingu sasa na vilele wakiendelea kunifunga kitambaa machoni .
Wakanisogeza pembeni kidogo kama kuna kibalaza fulani hivi wakaanza kunipiga sana kwa kutumia magongo kwenye unyayo kwenye mabega, kwenye mapaja, kwenye magoti . Lakini pia baadae tena wakanifunga wakanininginza juu walinipitisha chuma mguu kwa mguu halafu pingu wakaiweka kwa chini huku wakiendelea kunipiga na neno kubwa waliokuwa wananiambia kwamba wewe si cha mdomo unaongea sana sasa hivi tutakuuwa mshezi wewe , yani walikuwa wananitukana matusi makubwa.
Baadae wakawasha gari na lilitemba umbali mrefu kidogo wakaenda sehemu wakalibadilisha gari na safari ikanza tena limetembea gari kwa umbali mrefu sana likafika sehemu likasimama nikatolewa jamaa akaniambia toka! Kutambea umbali kidogo kutoka usawa wa gari kwa mguu wakati natembea nikawa nahisi kama nakanya kokoto hivi na baada ya kutembea umbali kidogo hivi nikahisi mazingira kama ya bahari na mawimbi. Nikajuwa hawa watu wanaenda kunitupa baharini kwa sababu wamnifunga kamba na wamenifunga na macho wanaenda kunitupa baharini kwenye kina na kwahiyo nitakosa msaada na nitakufa.
Kwahiyo alivyonipeleka mpaka hapo akaniambia nikae chini nami nikaa akananiambia nisegeuke ukegeuka nakugonga risasi na mimi sikugeuka akachukua kama kisu akikata kamba aliokuwa amenifunga kwenye mikono na akanifungua kitambaa alichokuwa amenifunga kwenye macho kwahiyo akaniambia nikitokea hapa niende nyumbani moja kwa moja usipite sehemu yoyote na wala tusisike unahadhitia popote na wala tusisike sauti yako kwenye chombo cha Habari chochote kama tumeweza kukukamata na sasa hivi umekuwa mzima tunaweza hapahapa kukuuwa.
Pia soma: Dar: Abdul Nondo amechukuliwa na Watu wasiojulikana katika mazingira ya utatanishi Kituo cha Mabasi cha Magufuli
Nilikuwa naweza kutembea mwenyewe lakini kwa kazi sana nikatembea hadi nikatokea barabani na ilikuwa ni ufukwe wa coco nikaomba msaada kwa baadhi ya watu wakasindwa kunisaidia lakini nikakutana na bodoboda na yeye akaenda kuwaita na wenzie wakaja wakanihoji pale kutengeneza uaminifu. Bodoboda mmoja akakubali kunibeba akaniuliza nakupeleka home nikamwambia hapana nikamwambia anipeleke kwenye ofisi yetu ya chama pale magomeni kwaajili ya msaaada zaidi kwa sababu sikuwa na simu maana simu walichukua kwahiyo nikapokelewa na mlizi kwahiyo mlinzi akafanya mawasiliano na viongozi wa chama.