Uchaguzi 2020 Nothing lasts longer, sasa ni dhahiri CCM inaenda kuangushwa kwenye Uchaguzi huu

Kama lengo ni kuweka pressure kwa ccm, basi sawa. Ila kama kweli mnamaanisha basi mna matatizo ya akili, kwa macho ya kawaida tu upinzani hauwezi kushinda huu uchaguzi.
Mimi ningeomba baada ya uchaguzi wasiendelee na majukumu mengine zaidi ya kujiandaa kwa ajili ya 2025
Lissu ni mwanasheria asingekosa kazi lakini ndiye Rais mpya ajae wa JMT
 

Haya ndio matamanio yako.
 
Hatuna cha kukusaidia zaidi ya kukuombea , hivi ni mtanzania yupi anaweza kumpigia kura Magufuli , na kwa sababu ipi ?
 
Huu utafiti wako uliufanyia wapi? na nani alikuwa supervisor wako?

Mahera kila siku anahangaika kuwaengua wagombea wa upinzani bila sababu za msingi halafu wewe unatuletea taarabu zako hapa.
 
Mkuu Erythrocyte kuanguka kwa utawala wowote chini ya jua haitegemea wanadamu ni Mungu mwenyewe anauondoa na kuuweka utawala anaoutaka yeye.....sisi ni sehemu ndogo tu ya mafanikio hayo na kwa hali ilivyo sasa hivi ccm wenyewe ndiyo watakaosaidia Lissu kupita kwa kumpa kura nyingi....
 
Hatuna cha kukusaidia zaidi ya kukuombea , hivi ni mtanzania yupi anaweza kumpigia kura Magufuli , na kwa sababu ipi ?
Kwani kila uchaguzi mnasemaga mmeshindwa kwa kura?? Si mnaliaga bao la mkono kila uchaguzi.......safari hiii mmejiandaaje maana tume bado ni ileile....kila kitu bado kipo constant kama zilivyokua chaguzi zilizopita.................sema tu naona mnatafuta sababu mapema za kujitetea baada ya kushindwa
 
Mihadarati gani umeitumia tunaomba na sisi wengine tupatie namba ya aliyekuuzia
 
HIVI JAMAA YENU ALISHAMALIZA KUTUMIKIA ILE ADHABU KWA AJILI YA KUSEMA UONGO??
 
Hatuna cha kukusaidia zaidi ya kukuombea , hivi ni mtanzania yupi anaweza kumpigia kura Magufuli , na kwa sababu ipi ?
Mkuu sikiliza.

Sisi wengine tuko chimbo kitambo tokea kuanza kwa kampeni. Timu iko kote BARA NA ZANZIBAR.

Nguvu wanazotumia CCM kufanya kampeni ili kuaminisha kuwa wanaungwa mkono ni kubwa na haijawahi kutokea katika historia yao.

Huwezi kuamini ukiziona gharama halisi za matumizi. Utashangaa kuwa matumizi haya yanafanywa na Mwenyekiti yule tunayeaminishwa anapendwa,

Sikwambii hio nguvu ya kutumia Madaraka, kupendelewa na kutumia makada wenye dhamana serikalini.

Ukweli mchungu hadi sasa CCM imeshindwa kuungwa mkono na Raia wengi walio huru na ambao si wanufaika wa CCM.

Hicho mnachokiona ni nguvu ya Pesa, Madaraka na Uoga wa vyombo vya Habari.

Kilichoko nyuma ya Pazia sio mchezo.

Usishangae Pole Pole kujifanya mtabiri na kujifanya NEC na ZEC.

Kinachoendelea anakijua yuko kazini kuhadaa watu ili mipango yao ya Wizi ipate uhalali.

Wapinzani wanatakiwa wasirudi nyuma kote BARA na Zanzibar.

Kamba inakaribia kukatika.
 
HIVI JAMAA YENU ALISHAMALIZA KUTUMIKIA ILE ADHABU KWA AJILI YA KUSEMA UONGO??
 
Kule Zanzibar bila Wasanii ndio kunapwaya.

Vikosi vyote kuna askari maalumu wanazungushwa na Magari na kupewa Sare za CCM hii sio siri.

Wanachama wa CCM Zanzibar hawaongezeki na wakiongezeka ni kwa Ratio. Ile ile Wapinzani V/s CCM . 3: 1

ZEC kupanga Siku mbili za Kura Zanzibar hakuna Justification zaidi ya figisu.

Mara hii hali ni mbaya zaidi.

Taarifa tulizonazo hata hizo kura halali za CCM ambazo hazizidi 150,000 kwa Zanzibar, asilimia 50% zinakwenda Upinzani kutokana na Mgombea Bwana Mwinyi kukataliwa Zanzibar.

Genuine Source Zinaarifu watu wameshapiga msimamo kwa viapo kuilinda Zanzibar.

Kwenye kura halali na nje ya wizi CCM haiwezi kupenya abadani.

Kilichobaki ni vitisho kwa wafanyakazi wa Serikali, mipango ya wizi wa kuingiza kura zilizopigwa tayari siku ya kura na kufanya vurugu baadhi ya maeneo ya upinzani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…