Now mil 50 UTT, napambana ifike mil 65 mwaka huu

Baada ya kuufuatilia huu uzi kwa ukaribu. Nimejilipua, nilikua na kaakiba bank kama 20M hakazai chochote, nimekatoa nimekaweka pale UTT kwenye mfuko wa Ukwasi, ngoja tuone itakuaje.
safi sana mkuu,
nimeshangaa watu wanaona riba ya 10% et ndogo...... yani uwekeze kwenye risk free investment kwa faida ya 10% alafu uone ndogo?

wanasahau hio hela ukifanyia biashara inaweza kupotea ndani ya siku 2 na usiwe na uwezo wa kuiokoa.....

anyway, elimu ya masoko ya fedha tanzania bado sana!
 
Ndiyo.
Mfano umeanza kudeposit 1M, kila mwezi inaongezeka 1% yake.
Mwezi ufatao… ukawa na 1,001,000\= wanaweka 1% yake. Vivyo hivyo
hii nzuri sana aiseee........
sisi wenye matumizi mabaya ya visenti vijisent vikikaa benk huko utt kunatufaa
 
Sawa Mkuu ..Safi Sababu umeishasema Hautaki Risk za Biashara. Ila 50M Kwa profit ya 450 monthly, Kwa Mjasiliamali halisi asee is not Good Move!! Endelea kufikiri vema! Hizi ni Investiment Wanazofanya wastaafu baada ya kUchukua Mafao.....
Which is less than 16k per day 🙁
 
Naam, nimeona mambo yasiwe mengi, sikua najua hii kitu kabisa au pengine sikuwahi kufuatilia. Hata kama faida ndogo basi angalau itunze thamani ya pesa yako.
 
Sijui kwanini haviwekwi. Yaani kwa hapa kwetu Tanzania ni kawaida sana kukutana na msomi wa chuo kikuu na pengine yupo kazini miaka kadhaa lakini hajui nini maana ya hisa, bond, na zinafaida gani na nani anaweza kuwekeza huko

Matangazo na elimu za kubeti zina nafasi kubwa sana ya kuifikia jamii kuliko mambo ya msingi kama haya
 
Utt watu wanaweka mabilioni we unataka kujua board of directors...

Sisi wabongo tunataka tuambiwe weka milioni upate milioni nyingine ndani ya mwezi ! Hakuna kitu km hicho, ndo maana akina kalaynda wanatupiga.
Ila kuweka milioni faida elf 50 mtu anaona ni ndogo
 
Chukua hela wekeza kwenye miradi Yako uzalishe Zaid acha uvivu ww!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…