Now mil 50 UTT, napambana ifike mil 65 mwaka huu

Now mil 50 UTT, napambana ifike mil 65 mwaka huu

Leta shule kuhusu hizi funds, maana wengine bado tupo gizani
Ipo hivi kuna funds za aina tatu katika uwekezaji....Kuna external traded fund mfano NICOL (hii kampuni kubwa tu hapa nchini,google it),Kuna Index fund mfano DSE Index na kuna mutual fund mfano UTT...
Ila hizo mbili za mwanzo ili uweze kuwekeza utajiandikisha kwenye mfumo wa hisa wa Soko la hisa Dar.
UTT (kwa ufupi)
-Taasisi ya serikali
-ndani yake kuna mifuko tofauti
-kila mfuko una malengo/masharti yake
-Unaweka hela
-Wao wanatumia hizo pesa kuwekeza kwenye makampuni,miradi.
-wanaikopesha serikali
-fedha yako yazaa faida
-Faida ni 9% hadi 11%,
-Hawana makato
-Mda wa kutoa hela huendana na mfuko ulipoweka pesa;kuna siku 2 hadi miaka.

Pitia ofisi zao, utapata elimu zaidi.
 
SI kama hivi... Au we huoni kama ni promo hii
Sasa Ndugu hapa watu ni wanajuzana juu ya mambo uwekezaji tu mbona.
Unaweza fika BOT au CmSA au DSE ukauliza, au nenda mjini jengo la Sukari...
Nenda ukajifunze tu,au pitia mtandaoni omba taarifa za UTT,omba taarifa za bodi, uone teuzi zao zafanywa na nani, omba taarifa zao za fedha.
 
Je ninkweli serikali Ina Nia ya dhati kuwainua wananchi was chini kiuchumi!!?au kuwafanya mateka ili watawaliwe kirahisi!!?

Au tunakusanya mitaji Kwa ajili ya manufaa ya watu wachache!!?

Hai utt nitawatafuta ili nijifunze Kwa kina !!

Hasa Nia ya serikali kwa wananchi wa chini!!

Duuh mna mioyo yani kwenye mil 7 apate 70 kwa mwezi...!!?

Kwa mwaka 840....hapana aisee
Mkuu,samahani naomba nikuulize,

Kwasasa benki ya Posta,TPL inatoa riba ya 11% kwenye fixed deposit yao...Je,ukiweka million 7,utapata kiasi gani baada ya mwaka...?

Na hiyo ishu ya benki ya posta wala sijatunga, nenda uwaulize...
 
Mkuu,samahani naomba nikuulize,

Kwasasa benki ya Posta,TPL inatoa riba ya 11% kwenye fixed deposit yao...Je,ukiweka million 7,utapata kiasi gani baada ya mwaka...?

Na hiyo ishu ya benki ya posta wala sijatunga, nenda uwaulize...
Bado ni ndogo apo ni kwenye laki 7 na kitu
 
Bado ni ndogo apo ni kwenye laki 7 na kitu
Sasa hapo hiyo faida si umepata kwa kuiweka fixed, ambapo benki huitumia kukopesha watu ....

The same na mutual fund wanavyofanya...
Mi nakushauri, kabla haujabisha fuatilia juu ya MUTUAL FUND na UTT....
Fuatilia juu ya usajili wake,Bodi yake, Ipo chini mamlaka gani, inaingizaje faida,ilianzishwa lini na nani...
 
Kwa wengi ambao wanahofia juu ya masomo ya mitaji na uwekezaji hawana makosa.Wengi wa vijana iwe wasomi au sio wasomi,bado hawana elimu juu ya masomo ya mitaji na uwekezaji.
Hii kitu ilikuwa na umuhimu wa kuwekwa kwenye mitaala ya shule japo kwa kugusia tu.
Kama ingefanyika hivyo basi hata maneno kama Hisa,Hati fungani na Mirabaha isingekuwa misamiati migumu kwa watanzania.
Maarifa yanatafutwa mkuu.
 
Habari,

Lengo sio kujitamba Bali ni kupeana chachu ya kuendelea kupambana. Leo nimefikisha 50ml lengo langu mwaka huu ni 65ml kutokana na saving zangu.

Sihitaji high return business bora nipate low return with minimal risk. Coz biashara imewahi nichakaza nikachanganyikiwa now sitaki kurudia makosa yaliopita. Kwangu UTT ni Bora zaidi! Nimewekeza Umoja, Jikimu, na Bond
Kwa hiyo sisi tufanyaje? 🙂
 
Pesa unazoweka NSSF, ni uwekezaji au sio?
Uwekezaji una vyanzo mbali mbali depends na morali ya mtu.
Mwingine anaona hawezi tunza kwenye Acc ya kawaida ya CRDB ambapo kila mwezi watakuwa wanamkata maintanance fee.
Heri aweke UTT aokote hata hiyo faida ya 1% monthly.
Mwingine anajitunzia kwenye kibubu ndani, mwingine anatunza kwenywe M pesa nk
Kwahiyo mkuu ukiweka hela UTT mil 1 unapata faida ya elfu 10k per month naomba ufafanuzi nahitaji kuweka PESA uko
 
Sijui hata unajaribu kuelezea nini kwa sababu huenda hata neno research hujui nimelitumia kwa muktadha gani. My dear, nazungumzia fact check na due deligence inayofanyika mara zote mtu anapotaka ku-invest sehemu yoyote. Huamki na kwenda kama umekatwa kichwa, kuna a, b, c za kufanya kwanza kujiridhisha ndiyo unawekeza. Shule za kukariri hizi!
Mkuu Kafanye basi due delligence uje kutuambia,maana hutusaidii kitu kwa kubisha,kama kuna kitu unajua jamvi lipo wazi
 
Back
Top Bottom