Jana nimeona katika vyombo vya habari NSSF wakijinasibu kwa ukwasi mkubwa waliotengeneza.
Jambo hilo linaonekana kama hatua ya mafanikio kwa shirika hilo lakini mimi nalifananisha na jambazi mwenye silaha za moto aliyefanikiwa kupora mali za watu na sasa anatoka hadharani kutamba kwamba amefanikiwa kuwa tajiri.
Sheria ya fao la kujitoa ilipobadilishwa imefanya watanzania wengi nikiwepo mimi tuache mamilioni ya pesa huko nssf tukisubiri umri wa miaka 55 ndipo tuwe na haki ya kuomba pesa zetu.
Na hapo sio kwamba watakupa kirahisi tu,inabidi usumbuane nao kwa kipindi kisichopungua miezi sita ndipo ufanikiwe kuzitoa.
Nilipokuwa mdogo nilikuwa naona picha za shetani ana mapembe na sura ya kutisha,siku hizi namuona live akiwa amevaa suti na sura ya kutabasamu,lakini anakuua unajiona hivi hivi.
Baada ya tangazo lao,kinachofuata ni kujiongezea posho na kupeana mikopo isiyo na riba ili wazipunguze pesa hizo,na sitashangaa hizo ndizo zitaenda kujenga maghorofa ya mikopo kwa matajiri wakiwemo wanaoingia mikataba na timu za mpira.
Sisi tunaodhulumiwa kilio chetu tunamwachia Mungu kwani hatuna jinsi ya kuwafanya hadi Mungu mwenyewe atakapoinua kizazi cha kisasi