Nunua na Aliexpress: Tuelimishane manunuzi mtandaoni

Nunua na Aliexpress: Tuelimishane manunuzi mtandaoni

Mbona mzigo wako umewahi? Mi niliagiza mwezi wa 12 tarehe 4 , mzigo umeingia jumatatu hii tarehe 27!!!
Mzigo Kama ukipitia China post ni tatizo kubwa labda Kama unapitia Singapore post
Singapore post wako fasta sana
 
Naomba kuuliza kuhusu suala la kodi. Nitajuaje kuwa kitu hicho kipo registered na hakitachajiwa kodi?
Na kingine kuhusiana na usafirishaji, je ni kampuni gani inasafirisha kwa bei ya wastani na kwa muda mfupi?
Niko njiani safarini ngoja nifike nitakujibu kwa utulivu
 
Wapendwa wa familia kubwa ya JamiiForums. Waswahel wanasema KIZURI KULA NA NDUGUYO.

Tunaingia kwenye zama za biashara na manunuzi mitandaoni, yaani muuzaji na mnunuzi hamfahamiani kabisa bali kuna mtu wa kati anayewakutanisha (dalali).

Huyu dalali amejenga uaminifu pande zote mbili kati ya muuzaji na mnunuzi, hivyo atapokea malipo ya mnunuzi atamjulisha muuzaji kuwa malipo yake anayo, muuzaji atatuma bidhaa husika. Mnunuzi akiipokea atathibitisha kuwa amepokea na dalali atapeleka malipo kwa muuzaji.

Nitaweka baadhi ya bidhaa nionazo ni unique kila wakati na utakayoipenda utaingia mtandaoni mwenyewe ama kupitia wakala.

Vilele nakaribisha maswali kuhusu manunuzi ya mtandaoni. App ninayotumia mimi ni Aliexpress lakini pia ziko nyingine nyingi.

View attachment 1521165View attachment 1521166View attachment 1521167
Nimekua mteja mzuri wa Aliexpr kutokana na andiko lako hili...shukrani sana...Jmaa waaminifu kwakiasi kikubwa
 
Mkuu naomba kufahamu kuhusu manunuzi kwanjia ya mtandao ktk mambo haya:-
1.Kuhusu kodi, TRA.
2. Mzigo naupataje Kama ni mtu wa mkoani ( kwa jumla na reja reja)
 
Sitaki kuharibu biashara ya mtu lakini kulinishinda kule ...hata hivyo haya maduka mawili ya mtandaoni inaelekea mmiliki ni mmoja
Ilianza Alibaba ilipoharibu akaja na Aliexpress nadhani....kwakuwa icloud inasoma Alibaba
By the way ulikuwa unahitaji vitu gani?
Alibaba wanauza sana large quantity Alibaba unanunua ata kamoja
 
Naomba kuuliza kama umeagiza mzigo na postal address uloandika mwanzo haupo tena hapo nikimaanisha umehama eneo Hilo.

Je kuna mfumo wa online wa posta ambao unaweza kuulizia mzigo wako kama umefika pale posta?
 
naomba kuuliza kama umeagiza mzigo na postal address uloandika mwanzo haupo tena hapo nikimaanisha umehama eneo Hilo.
je kuna mfumo wa online wa posta ambao unaweza kuulizia mzigo wako kama umefika pale posta?
Unaambatanisha na namba ya simu hivyo utapigiwa na mzigo unaweza kukaa posta hadi wiki 8
 
Soma hapo kwenye shipping fee..subiri niko safarini
Screenshot_20200730-120055.jpg
 
Back
Top Bottom