Nunua na Aliexpress: Tuelimishane manunuzi mtandaoni

Mbona mzigo wako umewahi? Mi niliagiza mwezi wa 12 tarehe 4 , mzigo umeingia jumatatu hii tarehe 27!!!
Mzigo Kama ukipitia China post ni tatizo kubwa labda Kama unapitia Singapore post
Singapore post wako fasta sana
 
Naomba kuuliza kuhusu suala la kodi. Nitajuaje kuwa kitu hicho kipo registered na hakitachajiwa kodi?
Na kingine kuhusiana na usafirishaji, je ni kampuni gani inasafirisha kwa bei ya wastani na kwa muda mfupi?
Niko njiani safarini ngoja nifike nitakujibu kwa utulivu
 
Nimekua mteja mzuri wa Aliexpr kutokana na andiko lako hili...shukrani sana...Jmaa waaminifu kwakiasi kikubwa
 
Mkuu naomba kufahamu kuhusu manunuzi kwanjia ya mtandao ktk mambo haya:-
1.Kuhusu kodi, TRA.
2. Mzigo naupataje Kama ni mtu wa mkoani ( kwa jumla na reja reja)
 
Alibaba wanauza sana large quantity Alibaba unanunua ata kamoja
 
Naomba kuuliza kama umeagiza mzigo na postal address uloandika mwanzo haupo tena hapo nikimaanisha umehama eneo Hilo.

Je kuna mfumo wa online wa posta ambao unaweza kuulizia mzigo wako kama umefika pale posta?
 
naomba kuuliza kama umeagiza mzigo na postal address uloandika mwanzo haupo tena hapo nikimaanisha umehama eneo Hilo.
je kuna mfumo wa online wa posta ambao unaweza kuulizia mzigo wako kama umefika pale posta?
Unaambatanisha na namba ya simu hivyo utapigiwa na mzigo unaweza kukaa posta hadi wiki 8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…