Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Nusrat Hanje, amesema taifa linahitaji kuwa na amani na kwamba uchaguzi unapaswa kufanyika bila kizuizi chochote, kwani pakikosekana amani hakuna pa kukimbilia.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Makiungu, Jimbo la Singida Mashariki, Wilayani Ikungi, Aprili 27, 2025, Nusrat amesema anashangazwa kuona mzaliwa wa eneo hilo ambaye walimwamini, anakuwa chanzo cha kutaka kuvuruga amani, huku akisisitiza kuwa wananchi wanapaswa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Kumekuwa na mazingira ambayo inaonekana kuna wengine wanataka kuvunja amani ya nchi yetu. Bahati mbaya sana, kuna wengine ambao wametoka kwenye ardhi yetu. Sisi ndio wenye mtoto ambaye anataka kuvunja amani ya nchi, na tunasema sisi tunapenda amani na tunakwenda na Dkt. Samia Suluhu Hassan," amesema Hanje.