Nyalandu na uongo wake

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Kaka yangu Lazaro Nyalandu kama wajumbe walikua 30, Lissu akapata 24 ilikuaje ukamgaragaza? Hizi hesabu zako mbona hazifuati formula ya MAGAZIJUTO? Kama Lissu alipata 24 kati ya 30 it means wewe uliipata kura 6. Kwahiyo unataka kutuambia ulimgaragaza kwa kura 6?

Halafu kwa maoni yangu nadhani uache kuongelea haya mambo ya Chadema, wewe jenga chama chako. Chadema ilikupokea na ikakupa heshima ya nafasi mbalimbali za uongozi. Kwakua umeamua kuondoka sidhani kama ni sahihi kuanza kuisema vibaya.

Najua unatafuta "remedy" huko CCM ili uaminike tena. Lakini usitafute remedy kwa kuisema vibaya Chadema. Hii itakuharibia zaidi kuliko kukujenga. Kumbuka ulivyojiunga Chadema uliisema vibaya CCM, na sasa umerudi CCM unaisema vibaya Chadema. CCM watakuwa wajinga sana kama wakikuamini kwa sababu unatoa siri za Chadema, wakati wanajua ulitoa pia siri za CCM ulipoenda Chadema.

Yani hapa umejijenga ukuta wa kutokuaminika pande zote mbili. Unavyoendelea kuiponda Chadema CCM wanakuona "snitch" kwa sababu wanajua uliiponda pia CCM ulipokua Chadema. Ukiachana na mwanamke akaenda kwa mwanaume mwingine, ikatokea akarudi kwako halafu akaanza kumponda yule mwanaume mwingine, basi ujue hata wewe alikua anakuponda alipokua kwa huyo mwingine. Simple logic. USIMUAMINI TENA.!

Unavyoendelea kuikandia Chadema unawapa CCM sababu nyingi zaidi za kutokukuamini, kuliko ungekaa kimya.

Njia nzuri ya kuaminika ndani ya CCM ni kutulia na kujenga chama chako. Msaidie Mwenyekiti wenu mpya kufanya reforms za mifumo. Mmepata Katibu Mkuu bora sana, msaidieni kukujenga upya chama chenu. CCM imepoteza ushawishi sana kwa vijana, jiulizeni tatizo ni nini ili mfanyie kazi mapungufu.

Hizi porojo za kwamba ulipata kura 6 kamati kuu halafu ukamgaragaza Lissu aliyepata 24, hazikusaidii sana wala hazisaidii chama chako.!

GJ Malisa
 
huyu jamaa sikumuamini kuanzia alivyokuwa home. na sasa karudi tena, ndio kabisaa!
 
Reactions: BAK
Mkuu, wakati alipohamia chadema na kuikandia ccm mbona mlikaa kimya bila kumzuia asifanye hivyo? Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
 
Mkuu, wakati alipohamia chadema na kuikandia ccm mbona mlikaa kimya bila kumzuia asifanye hivyo? Mkuki kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu!
Lipi alililolisema alipokuwa anahamia chadema ambalo ccm wamelitekeleza hadi akaamua kurudi ? video yake bado ingalipo.
 
Inaudhi sana Mkuu kwani maudhui hayaendani kabisa.
Niliweka uzi muruwa sana hapa kuhusu jambo hili lakini waka merge kwenye uzi dhaifu sana ambao hata haukuhusiana !
 
Reactions: BAK
Lipi alililolisema alipokuwa anahamia chadema ambalo ccm wamelitekeleza hadi akaamua kurudi ? video yake bado ingalipo.
Mkuu, acha kuhamisha goal post: hoja ya msingi ni uhuru wa kusema!
Kwa hiyo aliposema mapungufu ya ccm ilikuwa sawa, lakini akisema mapungufu ya chadema siyo sawa?!
 
Bavicha mnahangaika nini?

Kwanini yeye Lisu asijibu?
 
Nyarandu Mungu akulinde kazi umeimaliza karibu home.
 
Msijifiche kwenye ka hoja kadogo, Nyalandu amezungumzia pia tabia ya kishetani ilioneshwa na viongozi wakuu wa chama kwa kushangilia kifo cha aliyekua kiongozi mkuu wa nchi.

Pili, amezungumzia demokrasia ndogo na duni iliyopo ndani ya chama. Mwenyekiti amehodhi cheo kile kwa mda mrefu. Kika anayejaribu anakutana na kisanga. Sumaye aliambiwa na Mbowe kua "sumu haionjwi" kosa la sumaye ilikua ni kutaka uwenyekiti tu.
Tatu, Tundu Lissu anongozaje chama cha siasa chenye wanachama wengi kupitia mtandao wa Twitter na wasap? Yaani wakina Heche wapo, lakini wanaongozwa na mtu aliyepo ulaya kula bata!

Nyinyi bavicha mlitakiwa kua wakali na kukisaidia chama, mpaka sasa hatujui nani atagombea 2025, hakuna hata dalili. Tutashangaa Nape akifukuzwa CCM ndio mumchukue na kumwita 'kamanda' na siku akija kuondoka mtumuita mamluki. Yaani nyinyi!
 
Tabia ya muuaji magufuli je aliyewaua Watanzania chungu nzima wasio na hatia yoyote kama vile Ben Saanane na Azory Gwanda na kuwabambikia kesi Watanzania mbali mbali unaikumbuka? Acha kuonyesha ujuha hadharani ili kumtetea huyo mchumia tumbo.
 
Tabia ya muuaji magufuli je aliyewaua Watanzania chungu nzima wasio na hatia yoyote kama vile Ben Saanane na Azory Gwanda na kuwabambikia kesi Watanzania mbali mbali unaikumbuka? Acha kuonyesha ujuha hadharani ili kumtetea huyo mchumia tumbo.
Hahaha [emoji16][emoji38] nyinyi bavicha bhana! Hapo ndio umenijibu sasa? Sasa mie na Magufuli wapi na wapi? Kama aliua si muende mahakamani? Mie nazungumza demokrasia ndani ya chama changu, kama una hoja karibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…